Mbunge aliyewasilisha hoja ya kumuondoa naibu wa rais bungeni Kenya ajipata mashakani

 

Mbunge aliyewasilisha hoja ya kumuondoa naibu wa rais bungeni Kenya ajipata mashakani

g

Chanzo cha picha, Senete Kenya/ X

Maelezo ya picha, Mbunge wa Kibwezi Magharibi Mwengi Mutuse

Mbunge wa Kibwezi Magharibi Mwengi Mutuse alijipata katika hali ngumu siku ya Jumatano wakati alipokuwa akihojiwa ndani ya Seneti katika kesi ya kuondolewa madarakani aliyowasilisha kwabunge dhidi ya Naibu Rais Rigathi Gachagua.

Naibu Rais Rigathi Gachagua kupitia mawakili wake wazoefu wanaoongozwa na Wakili Paul Mwite wanapambana kuhakikisha haondolewi mamlakani baada ya Bunge la taifa mnamo Oktoba 8 kupiga kura kuidhinisha kutimuliwa kwake.

Mutuse alipata kibarua kigumu kujibu maswali makali ya wakili wa Gachagua Elisha Ongoya ambaye aliupinga ushahidi wake mkuu dhidi ya Bw Gachagua.

Miongoni mwa tuhuma ambazo wanasheria wa Gachagua walitaka kuzifuta ni pamoja na kuihujumu serikali kwa kupinga hadharani sera zake za kuwahamisha wafanyabiashara kutoka soko la wakulima na kuwapeleka katika eneo jipya katika Barabara ya Outering na ubomoaji wa majengo katika maeneo ya mabondeni.

Timu ya Gachagua ilitumia kanda za video kuwadhihirishia maseneta kuwa alitoa matamshi akiiomba serikali kuwatendea raia utu na zile zilizoonyesha kuwa baadhi ya kauli zilizotajwa kuchochea ukabila zimekuwa zikitumiwa tangu awali pia na Rais william Ruto na kwamba zilikuwa msingi wa ugavi wa madaraka katika serikali ya sasa ya Kenya Kwanza .

Mawakili wa Gachagua walitoa video ambapo alitoa matamshi akiiomba serikali kuwatendea raia utu kwa kuzingatia ahadi zake za kabla ya kampeni.

“Naibu Rais anasema ‘Tusiwe na vita na Wananchi.’. Je, unaona jambo lolote la kuudhi katika taarifa hiyo?” Ongoya alimuuliza, Mutuse aliyejibu , hapana.

"Anatoa wito wa huruma kwa wananchi. Je, unaona jambo lolote la kukera katika sehemu hiyo?” wakili aliuliza.

g

Chanzo cha picha, Senete

Maelezo ya picha, Rigadhi gachagua alikanusha mashtaka yote dhidi yake

Wakati mmoja kesi hiyo ilipokuwa ikiendelea wakili wa Gachagua, alicheza kanda ya video ambapo Rais Ruto alionekana kwenye mkutano akiwaambia wananchi wa eneo la Mlima Kenya kuwa wana 'share' (hisa) katika serikali- kauli ambayo bunge linasema imekuwa ikitumiwa na Gachagua na inachochea ukabila. Gachagua alisema alijifunza kutumia kauli hiyo kutoka kwa Rais Ruto.

Popular posts from this blog

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni

Vita vya Urusi na Ukraine: Matukio matano muhimu ya faida na hasara kwa Putin 2024