Meya na wengine 15 wauuawa katika shambulio la Israeli kwenye mkutano wa baraza la Lebanon

 

Meya na wengine 15 wauuawa katika shambulio la Israeli kwenye mkutano wa baraza la Lebanon

g

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Gavana wa Nabatieh alisema idadi ya waliofariki inaweza kuongezeka kwani bado wanasaka miili katika vifusi

Mratibu maalum wa shuguli za Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Lebanon ameikosoa Israel baada ya mashambulizi ya anga kwenye majengo ya manispaa katika mji wa kusini wa Nabatieh kumuua meya na watu wengine 15.

Jeanine Hennis-Plasschaert aameyaita mauaji ya meya Ahmad Kahil "ya kutisha" na kusema ukiukaji wowote wa sheria za kimataifa za kibinadamu "haukubaliki kabisa".

Takriban watano kati ya waliouawa katika shambulio la Jumatano walikuwa wafanyakazi wa manispaa walioratibu misaada kwa ajili ya raia waliosalia katika eneo hilo, Gavana wa Nabatiyeh Howaida Turk ameiambia BBC.

Kaimu Waziri mkuu wa Lebanon, Najib Mikati amelaani shambulio hilo, akisema "lililenga" mkutano wa baraza.

Shambulio hilo lilikuwa kubwa zaidi dhidi ya jengo la serikali ya Lebanon tangu kuongezeka kwa mapigano ya hivi karibuni, ambayo yalianza takriban wiki mbili zilizopita, na limezua wasiwasi juu ya usalama wa miundombinu ya serikali ya nchi hiyo.

Msemaji wa jeshi la Israel amesema vikosi vyake vimefanya mashambulizi yakilenga makumi ya maeneo ya Hezbollah katika eneo hilo na kuharibu handaki linalotumiwa na kundi hilo linaloungwa mkono na Iran.

"Tunajua kwamba Hezbollah mara nyingi hutumia fursa ya vituo vya kiraia," balozi wa Umoja wa Mataifa wa Israel Danny Danon alisema katika mkutano wa Umoja wa Mataifa Jijini New York Jumatano.

Popular posts from this blog

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni

Vita vya Urusi na Ukraine: Matukio matano muhimu ya faida na hasara kwa Putin 2024