FBI yapata kifurushi kikubwa zaidi cha vilipuzi katika shamba Virginia

 

f

Chanzo cha picha, FBI

Shirika la ujasusi la Marekani FBI linasema limegundua zaidi ya mabomu 150 wakati wa uvamizi kwenye shamba moja huko Virginia - kinachodhaniwa kuwa hifadhi kubwa zaidi ya aina hiyo iliyokamatwa na wakala wa shirika hilo katika historia yake.

Mshukiwa Brad Spafford alikamatwa tarehe 17 Disemba katika kaunti ya Wight County, maili 180 (290km) kusini mwa Washington DC, baada ya mtu mmoja kutoa taarifa kwamba alikuwa akihifadhi silaha na risasi za kujitengenezea nyumbani kwenye makazi anayoishi na mke wake na watoto wawili wadogo.

Wachunguzi wanasema baadhi ya vifaa hivyo vilipatikana katika chumba cha kulala ndani ya begi la mgongoni ambalo halina ulinzi lililoandikwa "#nolivesmatter" – alama dhahiri ya vuguvugu la mrengo wa kulia, linalopinga serikali.

Wakili wa Bw Spafford alikanusha kuwa yeye ni hatari kwa jamii na anataka mteja wake aachiliwe kutoka kizuizini kabla ya kesi yake kuanza kusikilizwa.

Popular posts from this blog

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni

Putin asaini mkataba wa kituo cha Mwezi na China