Janga lingine; Kuporomoka kwa mfumo wa afya wa Gaza

 


  • Janga lingine; Kuporomoka kwa mfumo wa afya wa Gaza

Msemaji wa Shirika la Afya Duniani (WHO) ametangaza kwamba mfumo wa afya na matibabu wa Gaza umeporomoka, akisema: juhudi zote za shirika hili kwa ajili ya kuhifadhi mfumo wa afya katika Gaza zimeenda na maji.

Daktari Margaret Harris amesisitiza kwamba: Mashambulizi ya Israeli dhidi ya hospitali, wafanyakazi wa afya na wagonjwa hayawezi kukubalika katikka hali yoyote na yanapaswa kusitishwa.

Utawala wa Kizayuni wa Israel, kwa kupuuza sheria na maonyo yote ya kimataifa ya mashirika ya kimataifa, umelenga na kuharibu miundombinu ya afya na matibabu na aghalabu ya vituo vya afya na hospitali za Ukanda wa Gaza. Shambulio dhidi ya Hospitali ya Kamal Adwan na kuteketezwa kwake siku chache zilizopita, ni mfano wa hivi karibuni katika suala hili.

Wizara ya Afya ya Palestina katika Ukanda wa Gaza ilitangaza kuhusiana na hilo kwamba: "Baada ya kuwatishia wagonjwa na waliojeruhiwa kwa silaha, jeshi la utawala ghasibu wa Israel liliwahamisha kwa nguvu hadi Hospitali ya Indonesia ya Gaza na kuichoma moto hospitali hiyo."

Tedros Adhanom Ghebreyesus, mkuu wa Shirika la Afya Duniani, akiashiria utawala wa Kizayuni wa Israel, ameandika katika ujumbe kwenye mtandao wa kijamii wa X kwamba: "Hospitali za Gaza zimekuwa uwanja wa vita, na mfumo wa afya unakabiliwa na tishio kubwa. Sitisha mashambulizi dhidi ya hospitali. Watu wa Gaza wanahitaji kupata huduma za matibabu. Waokoaji wanahitajikka ili kutoa usaidizi wa kiafya. Sitisha mapigano."

Tangu kuanza kwa vita vya Gaza, utawala wa Kizayuni umeshaua shahidi zaidi ya madaktari na wauguzi elfu moja wa Kipalestina katika mashambulizi ya makusudi  dhidi ya wafanyakazi wa afya katika Ukanda wa Gaza, na zaidi ya wafanyakazi 300 wa matibabu wamekamatwa na kuteswa. Takwimu zinaonyesha kuwa hospitali 34 zimeshambuliwa  kutokana na mashambulizi ya Israel na vituo 80 vya afya vimeharibiwa kabisa.

Shirika la Hilali Nyekundu la Palestina linasema hadi hivi karibuni ni hospitali tatu tu ndizo zilikuwa zikifanya kazi kaskazini mwa Gaza ya mwisho ikiwa ni Hospitali ya Kamal Adwan.

Kwa mazingira haya, hali sasa imekuwa ngumu zaidi kwa wakazi wa Gaza. Pamoja na kuporomoka kwa mfumo wa matibabu, hali ya hewa ya baridi, na ukosefu wa vituo vya afya, kuenea kwa magonjwa ya kuambukiza kama vile kipindupindu kumeongezeka, na wagonjwa wengi wanaohitaji matibabu endelevu wanashindwa kuendelea na matibabu yao.

Kwa mazingira haya, hali sasa imekuwa ngumu zaidi kwa wakazi wa Gaza. Pamoja na kuporomoka kwa mfumo wa matibabu, hali ya hewa ya baridi, na ukosefu wa vituo vya afya, kuenea kwa magonjwa ya kuambukiza kama vile kipindupindu kumeongezeka, na wagonjwa wengi wanaohitaji matibabu endelevu wanashindwa kuendelea na matibabu yao.

Hospitali ya Kamal Adwan

Munir Al-Barsh, Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Afya ya Gaza, alieleza katika taarifa yake kile kinachotokea kaskazini mwa Gaza kuwa mauaji ya kimbari, ambayo yanaonyesha kushindwa kwa dhamiri ya binadamu. Alisema: "Kinachotokea Gaza leo kinapita zaidi ya jinai za kawaida na ni mauaji ya kimbari kwa maana yake kamili, yanayotekelezwa mbele ya macho ya walimwengu."

Njaa na baridi sasa vinatishia maisha ya wakaazi wa Gaza kuliko hapo awali. Shirika la Chakula Duniani (WFP) pia ulitangaza: "Njaa imeenea kote Gaza na tunaweza tu kutoa chakula kwa theluthi moja ya wahitaji huko Gaza, kwa upande mwingine, wimbi la baridi na ukosefu wa miundombinu ya msingi ya maji na umeme ni jambo ambalo limesababisha watu wengi wagonjwa na watoto kufa kutokana na baridi kali." Kulingana na takwimu zilizochapishwa, idadi ya watoto wachanga ambao wamekufa kutokana na baridi huko Gaza katika wiki iliyopita imefikia 7.

Philippe Lazzarini, Kamishna Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Kipalestina UNRWA pia alitangaza kwamba watoto huko Gaza wanaganda kama theluji kutokana na baridi na ukosefu wa makazi, na kwamba Israel hairuhusu mablanketi na vifaa vya baridi kuingia. Gaza.

Mashirika ya kimataifa ya kutoa misaada yameonya rasmi kuhusu maafa ya sasa. Kuhusiana na hili, Shirika la  Chakula Duniani lilisisitiza haja ya pande zote kuheshimu sheria za kimataifa wakati wote na kuunga mkono hospitali, vituo vya matibabu, na wafanyakazi wa misaada, na kutoa wito wa kukomeshwa mara moja kwa mapigano na utoaji wa misaada kote Gaza.

Margaret Harris msemaji wa Shirika la Afya Duniani alisema pia: Hivi karibuni timu kutoka Shirika la Afya Duniani itatumwa kwenda Gaza ili kutathmini mahitaji ya eneo hilo na upungufu wa vifaa vya hospitali.

Ukosefu wa hospitali, madaktari na wafanyakazi wa afya, uhaba wa dawa, chakula, baridi, pamoja na kufungwa kwa njia za misaada na wanajeshi wa Israel, vimekamilisha mzunguko wa uhalifu na mauaji ya kimbari ya Israel huko Gaza. Yote haya yanatokea huku nchi za Magharibi, licha ya kauli mbiu zao za kibinadamu na madai ya kujitolea kwa sheria za haki za binadamu, zikiendelea kufumbia macho uhalifu wa Israel na kuendeleza msaada wao wa kisiasa, kifedha, na kijeshi kwa utawala wa Kizayuni.

Popular posts from this blog

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni

Putin asaini mkataba wa kituo cha Mwezi na China