Kiribati yawa nchi ya kwanza duniani kuukaribisha mwaka 2025
Taifa la Kiribati ambalo ni kisiwa katika bahari ya Pacific ndio nchi ya kwanza duniani kuukaribisha mwaka mpya wa 2025.
Nchi hiyo inaundwa na visiwa 33, imeenea karibu kilomita 4,000 (maili 2,485) kutoka mashariki hadi magharibi na zaidi ya kilomita 2,000 kutoka kaskazini hadi kusini.
Nchi nyingine ambazo zimeshaukaribisha mwaka mpya ni New Zealand, maonyesho ya kitamaduni na fataki yanaendelea katika majiji kuashiria kuwasilia kwa mwaka mpya.
Vilevile, usiku wa manane umeingia huko Sydney, Australia na kuashiria mwanzo wa 2025 katika nchi iliyo katika bahari ya Pasifiki na bahari ya Hindi.