Mahakama yatoa hati ya kukamatwa kwa rais wa Korea Kusini aliyeondolewa madarakani Yoon

 

g

Chanzo cha picha, Reuters

Mahakama ya Seoul imetoa hati ya kukamatwa kwa rais aliyesimamishwa kazi wa Korea Kusini Yoon Suk Yeol kutokana na jaribio lake la kuweka sheria ya kijeshi tarehe 3 Disemba.

Hatua hiyo inajiri baada ya Yoon, ambaye anakabiliwa na uchunguzi kadhaa wa mashtaka ya uasi na uhaini, kupuuza hati tatu za kuitwa kuhojiwa kwa muda wa wiki mbili zilizopita.

Siku ya Jumapili usiku, wachunguzi waliomba kutolewa kwa hati ya kukamatwa kwa Yoon kwa tuhuma za uasi na matumizi mabaya ya mamlaka - hatua ambayo wakili wake aliitaja kuwa "haramu".

Korea Kusini imekuwa katika mzozo wa kisiasa tangu kutangazwa kwa sheria ya kijeshi kwa muda mfupi, na Yoon na mrithi wake wote wameshtakiwa na bunge.

Popular posts from this blog

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni

Putin asaini mkataba wa kituo cha Mwezi na China