Matarajio yetu ni kuuawa shahidi; Majibu ya Ansarullah ya Yemen kwa orodha ya magaidi wa Israel

 

  • Matarajio yetu ni kuuawa shahidi; Majibu ya Ansarullah ya Yemen kwa orodha ya magaidi wa Israel

Mwanachama mmoja wa harakati ya Ansarullah ya Yemen amezungumzia hatua ya kuchapishwa orodha ya walengwa wa mashambulizi ya kigaidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel kusema: "Hatumuogopi yeyote isipokuwa Mwenyezi Mungu, na tunamuomba atuondoe duniani kwa njia ya kuuliwa shahidi."

Mohammed Al-Bakhiti, mjumbe wa Ofisi ya Kisiasa ya harakati ya Ansarullah ya Yemen amechapisha picha ya orodha ya walengwa wa mashambulizi ya kigaidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel wa Yemen katika akaunti yake ya mtandao wa X na kuandika: "Matarajio yetu ni kuuawa shahidi katika njia ya Mungu."

Al-Bakhiti ameongeza kuwa: "Tunaiambia Marekani, Uingereza na utawala wa Kizayuni kwamba tuna uwezo na ujasiri wa kulipiza kisasi na tutawalenga makamanda wenu wa kijeshi na kisiasa, tuna benki kubwa ya shabaha za kulenga, na mpira sasa uko katika uwanja wenu."

Vyombo vya habari vya utawala wa Kizayuni wa Israel vimechapisha picha ya maafisa kadhaa wa Yemen, vikitangaza kuwa ni shabaha halali za kulengwa na kuwaweka katika orodha ya magaidi ya utawala huo.

Popular posts from this blog

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni

Putin asaini mkataba wa kituo cha Mwezi na China