SADC yataka kuhitimisha uhasama haraka iwezekanavyo nchini Msumbiji

 

  • SADC yataka kuhitimisha uhasama haraka iwezekanavyo nchini Msumbiji

Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) jana Jumanne ilitoa wito wa kuhitimishwa mara moja uhasama na mivutano inayoendelea huko Msumbiji ambapo watu 278 wameuawa tangu chama kikuu cha upinzani kipinge matokeo ya uchaguzi wa Rais wa mwezi Oktoba.

Chama kikuu cha upinzani nchini Msumbiji kilitaja matokeo ya uchaguzi wa rais kuwa yaligubigwa na udanganyifu. 

Rais Samia Suluhu Hassan wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ni Mwenyekiti wa sasa wa Jumuiya ya SADC amesema kuwa jumuiya hiyo imesikitishwa sana na kuendelea kupoteza maisha raia, kujeruhiwa watu na kuharibiwa mali za watu binasfi na miundombinu ya umma. 

Rais Samia Suluhu Hassan amesema kuwa SADC inatoa wito kwa pande zote huko Msumbiji kujizuia na kujiepusha na vitendo vinavyozidisha ghasia na machafuko.  

"SADC ipo tayari kutoa mchango wake kupitia njia zinazofaa ili kupata ufumbuzi wa  amani wa changamoto zilizopo," amesema Mwenyekiti wa jumuiya ya SADC. 

Raia wa Msumbiji wamekuwa wakiandamana tangu Tume ya Uchaguzi  ya nchi hiyo imtangaze Daniel Chapo mwenye umri wa miaka 47 aliyekuwa mgombea wa chama tawala cha Frelimo, kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais wa Oktoba 9. Chapo aliibuka na ushindi wa asilimia 71 ya kura dhidi ya mgombea wa upinzani Venancio Mondlane aliyepata asilimia 20 ya kura.

Popular posts from this blog

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni

Putin asaini mkataba wa kituo cha Mwezi na China