Skip to main content

Tetesi za soka Jumatano: Liverpool yakataa mpango wa Real wa kumsajili Alexander Arnold

 

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Trent Alexander-Arnold

Liverpool wamekataa mpango wa Real Madrid wa kutaka kumsajili beki wa kulia wa Uingereza Trent Alexander-Arnold, 26, mwezi Januari. (Athletic - subscription required)

Juventus na Napoli wana nia ya kumsajili mshambuliaji wa Manchester United na Uholanzi Joshua Zirkzee, 23. (Mirror)

Manchester United hawana bajeti ya kuimarisha kikosi chao mwezi Januari na watalazimika kuuza wachezaji kwanza kabla ya kununua ili kuwa na faida na na sheria za uchezaji wa haki za Kifedha endelevu . (Manchester Evening News)

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mohamed Salah

Winga wa Misri Mohamed Salah, 32, na mlinzi wa Uholanzi Virgil van Dijk, 33, wote wanatarajiwa kuongeza muda wao wa kukaa Liverpool kwa miaka miwili. (David Ornstein, via Mirror)

Liverpool wako tayari kumuuza mshambuliaji wa Uruguay Darwin Nunez, 25, na wamemtambua mshambuliaji wa Inter Milan na Ufaransa Marcus Thuram, 27, pamoja na mshambuliaji wa Newcastle Uswidi Alexander Isak, 25, kama wachezaji wanaoweza kuchukua nafasi. (Teamtalk)

Liverpool wanaweza kushindana na Manchester United kwa kumsajili beki wa kushoto wa Hungary Milos Kerkez, 21 kutoka Bournemouth. (Caught Offside)

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Dani Olmo.

Arsenal, Liverpool, Chelsea na Tottenham wameungana na Manchester United na Manchester City katika kuonyesha nia ya kumnunua mshambuliaji wa Barcelona mwenye umri wa miaka 26 Dani Olmo. (Mundo Deportivo - in Spanish)

Olmo, hata hivyo, anataka kusalia Barcelona , ​​licha ya kutokuwa na uhakika juu ya usajili wake. (Fabrizio Romano, via GiveMeSport)

Real Madrid wanavutiwa na mlinzi wa Bournemouth wa Uhispania chini ya umri wa miaka 21 Dean Huijsen, 19. (Fichajes - in Kihispania)

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Cesare Casadei

Chelsea wako tayari kumuuza kiungo wa kati wa Italia Cesare Casadei, 21, ambaye amevutia klabu ya Torino ya Italia. (Talksport)

Nottingham Forest wana uhakika wa kukubaliana kandarasi mpya na beki wa pembeni wa Nigeria Ola Aina, 28, ambaye analengwa na Manchester City . (Football Insider)

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Christopher Nkunku

Barcelona wanaweza kumnunua kwa mkopo mshambuliaji wa Chelsea Christopher Nkunku mwenye umri wa miaka 27 kama watashindwa kumsajili Olmo kwa kipindi cha pili cha msimu. (Offside)

Bayern Munich wameorodhesha makipa kadhaa ambao wanaweza kuwasajili msimu wa kiangazi akiwemo mchezaji wa kimataifa wa Uholanzi wa miaka 22 Bart Verbruggen wa Brighton . (Bild - in German, subscription required)

Wolves wanatathmini dau la kumnunua beki wa Millwall Muingereza Japhet Tanganga, 25, mwezi Januari. (Express)

Popular posts from this blog

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni

Putin asaini mkataba wa kituo cha Mwezi na China