Ugonjwa wa ajabu wa ‘kucheza densi’ unasumbua mamia nchini Uganda
Ugonjwa wa ajabu wa ‘kucheza densi’ unasumbua mamia nchini Uganda
Takriban watu 300 wameambukizwa ugonjwa wa ajabu wa ‘kucheza ngoma’ nchini Uganda huku serikali ikianzisha uchunguzi kubainisha chanzo chake.
Wenyeji wanauita ugonjwa huo ‘Dinga Dinga,’ yaani ‘kucheza densi. Jina hilo linatokana na ukweli kwamba dalili zake ni pamoja na homa na kutetemeka hali ambayo husababisha kuwepo ugumu wa kutembea, ilisema.
Kwa sababu zisizojulikana, walioathiriwa na ugonjwa huo ni wanawake na wasichana. Wakuu wa afya nchini humo waliutambua ugonjwa huo kwa amra ya kwanza mwaka jana.
Mlipuko huo wa sasa ulioanza miezi kadhaa iliyopita, uko katika Wilaya ya Bundibugyo kusini magharibi, ambayo inapakana na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Hakuna kesi zilizoripotiwa katika maeneo mengine ya nchi hiyo.
Afisa Afya wa Wilaya, Daktari Kiyita Christopher ameliambia gazeti la Daily Monitor kuwa hadi sasa hakuna vifo vilivyotokea kutoka na Dinga Dinga.
Alisema mara nyingi ugonjwa huo ni wa kujiponya, na kuongeza kuwa kwa wale waliokuwa katika hali mbaya, madaktari walifanikiwa kuwaponya kwa kutumia dawa za antibiotiki.
Hata hivyo, daktari huyo amewaonya wenyeji dhidi ya kugeukia dawa za kienyeji ili kuponya ugonjwa huo.
Sampuli kutoka kwa walioambukizwa zimechukuliwa ili kutumwa kwa maabara zinazoendeshwa na Wizara ya Afya ya Uganda kwa uchunguzi zaidi wa ugonjwa huo.