UN yasema mashambulizi ya Israel katika hospitali za Gaza yanaelekea kusambaratisha huduma za afya

 

fd

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Ambulensi iliyoharibika nje ya hospitali ya Kamal Adwan kaskazini mwa Gaza Oktoba 2024

Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa imesema mashambulizi ya Israel katika hospitali na kandokando ya hospitali yanaisukuma miundombinu ya afya ya Gaza kufikia katika "ukingo wa kusambaratika moja kwa moja" na kuibua wasiwasi mkubwa kuhusu uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu.

Ripoti mpya inaeleza kuwa msururu wa mashambulizi ya majeshi ya Israel, kuzingira, na kuwahamisha watu katika hospitali kwa nguvu, yanasababisha wagonjwa kuufa au kuuawa.

Ofisi hiyo inatambua madai ya Israel kwamba hospitali zimekuwa zikitumiwa na makundi yenye silaha ya Palestina, lakini inasema ushahidi wake "haueleweki."

Jeshi la Israel halijatoa tamko lolote. Lakini daima husisitiza vikosi vyake vinazingatia sheria za kimataifa na kuchukua hatua za kupunguza madhara kwa raia na huduma za matibabu.

Ripoti hiyo inakuja siku chache baada ya hospitali ya mwisho inayofanya kazi katika eneo la kaskazini mwa Gaza, kuzingirwa na kuvamiwa na jeshi la Israel, ambalo lilisema inatumika kama kituo cha kamandi cha Hamas.

Israel ilianzisha mashambulizi ya kuiangamiza Hamas kujibu mashambulizi ya kundi hilo kusini mwa Israel tarehe 7 Oktoba 2023, ambapo takriban watu 1,200 waliuawa na wengine 251 walichukuliwa mateka.

Zaidi ya watu 45,500 wameuawa na 108,300 kujeruhiwa huko Gaza tangu wakati huo, kulingana na wizara ya afya ya eneo hilo inayoendeshwa na Hamas.

Popular posts from this blog

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni

Putin asaini mkataba wa kituo cha Mwezi na China