Vito vya thamani ya £10m vyaibiwa kutoka nyumbani London
Bidhaa hizo ni pamoja na vipande vya Katherine Wang, De Beers na Van Cleef
Vito vya thamani ya zaidi ya pauni milioni 10 pamoja na mikoba ya wabunifu yenye thamani ya £150,000 vimeibwa kutoka katika nyumba moja huko St John's Wood jijini London.
Mzungu mwenye umri wa kati ya miaka 20 hadi 30 alivamia nyumba moja majira ya kati ya kumi na moja jioni na saa kumi na moja unusu jioni ambapo alipanda kupitia dirisha la ghorofa ya pili, Polisi wa London walisema.
Alichukua mikoba ya Hermes Crocodile Kelly, pesa taslimu £15,000 pamoja na vito vya thamani ya pauni milioni £10.4
Wamiliki wa nyumba wametoa zawadi ya pauni 500,000 kwa habari zitakazopelekea kukamatwa na kutiwa hatiani kwa mshukiwa.