Iran imeweza vipi kuwa na nafasi ya juu katika nyanja za afya ya wanawake wajawazito?

 

  • Iran imeweza vipi kuwa na nafasi ya juu katika nyanja za afya ya wanawake wajawazito?

Moja ya masuala muhimu ambayo yameonekana katika miongo miwili iliyopita ni nafasi ya juu ya mfumo wa afya wa Iran kati ya nchi za kanda ya Asia Magharibi na dunia kwa ujumla.

Ikilinganishwa na nchi nyingine katika kanda ya Asia Magharibi na kwingineko, mfumo wa afya wa Iran umepewa nafasi ya juu na bora, na nafasi hii nzuri imeweka msingi kwa Iran kuwa miongoni mwa nchi muhimu zaidi za utalii wa afya katika kanda hiyo. Kuhusiana na suala hilo, Iran imepata maendeleo makubwa katika nyanja za afya ya mama wajawazito katika miaka ya hivi karibuni. Kupungua kwa kiasi kikubwa vifo vya akinamama wajawazito ni miongoni mwa mafanikio muhimu ya nchi, na kwa mtazamo huo, Iran ni miongoni mwa nchi chache ambazo zimeweza kufikia malengo ya maendeleo na ustawi katika kupunguza vifo vya akinamama wajawazito.

Iran ni miongoni mwa nchi chache zilizofanikwa kwa kiwango kikubwa katika kupunguza vifo vya akinamama wajawazito.

Waziri wa Afya, Tiba na Elimu ya Tiba wa Iran, Mohammad-Reza Zafarghandi, anasema Jamhuri ya Kiislamu ni miongoni mwa nchi 3 zinazoongoza duniani katika kupunguza kiwango cha vifo vya akinamama wajawazito, na fahari hiyo ni matokeo ya miaka mingi ya bidii na juhudi kubwa.

 Dr. Mohammad Raiszadeh, Mkuu wa Shirika la Mfumo wa Matibabu la Iran pia anasema: Lengo la Shirika la Afya Duniani (WHO) mwaka 2030 ni kupunguza kiwango cha vifo vya uzazi duniani hadi chini ya visa 70 kwa kila watoto 100,000 wanaozaliwa wakiwa hai, wakati takwimu hizo kwa sasa nchini Iran ni vifo 22 kati ya kila watoto laki moja wanaozaliwa. 

Ni muhimu kwa akinamama kuwanyonyesha watoto kwa uchache kwa miezi sita na kuendelea hadi miaka miwili.

Ni wazi kwamba, mafanikio haya ni matokeo ya juhudi kubwa za serikali, vituo vya afya na mashirika ya Iran. Hapa tunataja baadhi ya hatua muhimu zaidi zilizochukuliwa hapa chini katika uwanja huo:

1- Ni ustawishaji wa miundombinu ya afya ikiwa ni pamoja na kujenga na kuandaa vituo vya afya vyenye zana na vifaa vya kisasa vinavyohitajika vya tiba katika mikoa mbalimbali nchini, hasa maeneo yaliyokuwa na uhaba wa vifaa hivyo. Vifaa vya uchunguzi na matibabu ni muhimu kwa ajili ya huduma za akinamama wajawazito katika vituo vya afya.

2- Programu za uchunguzi wa magonjwa ya vinasaba. Huku kunahusiana na kufanya vipimo vya uchunguzi ili kugundua magonjwa ya kinasaba katika fetasi na uchunguzi wa magonjwa ya kuambukiza kwa wakati na matibabu ya magonjwa ya kuambukiza kama vile homa ya ini na UKIMWI kwa mama wajawazito.

3- Mafunzo na taarifa. Kufanya warsha na madarasa ya kutoa mafunzo kwa kinamama wajawazito kuhusu lishe bora, utunzaji wa ujauzito, uzazi wa kawaida na unyonyeshaji. Jambo jingine ni kutumia vyombo vya habari vya mawasiliano ili kuongeza uelewa wa umma kuhusu umuhimu wa afya ya uzazi.

4- Kuhimiza uzazi wa kawaida. Kifungu hiki kinahusiana na kuhimiza akina mama kujifungua kwa njia ya kawaida na kupunguza idadi ya upasuaji usio wa lazima na kuboresha ujuzi na maarifa ya wakunga ili kinamama wajawazito wajifungue kwa njia salama.

5- Ugavi bure wa dawa na virutubisho vya chakula kama madini ya chuma na folic acid, kuzuia upungufu wa damu kwa mama wajawazito na kutoa bure virutubisho vingine muhimu na kukidhi mahitaji ya lishe kwa mama wajawazito.

6- Ni kutoa bima ya afya kwa wote, kulipa gharama za wajawazito na za kujifungua, kupunguza mzigo wa kifedha kwa familia na kuongeza upatikanaji wa huduma za afya.

7- Ni programu za lishe na ugawaji wa chakula kwa akinamama wajawazito katika maeneo yenye mazingira magumu, kutoa elimu ya lishe bora na kuinua uelewa wa kinamama kuhusu lishe bora wakati wa ujauzito.

Lishe bora ni muhimu kwa mama wajawazito

8- Kusaidia akinamama wanaonyonyesha. Ni kuhimiza unyonyeshaji wa maziwa ya mama pekee hadi miezi sita na kuendelea hadi umri wa miaka miwili, na kuwafundisha akinamama kuhusu mbinu sahihi za unyonyeshaji.

Mwishoni ifahamike kuwa, kuboreka nafasi ya Iran katika mfumo wa afya ikiwemo masuala ya afya ya wanawake wajawazito, kumekuwa na manufaa mengi. Ubora wa hali ya afya nchini Iran na miundombinu imara ya mfumo wa afya vimeifanya Iran kuwa mojawapo ya maeneo ya afya yanayotegemewa, yanayofikika kirahisi, nafuu na ya kutegemewa kwa ajili ya utalii wa afya.

Popular posts from this blog

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni

Putin asaini mkataba wa kituo cha Mwezi na China