Iran yalaani vikali shambulizi linalohusishwa na Daesh nchini Marekani

 

  • Esmail Baqaei
    Esmail Baqaei

Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imelaani vikali shambulio la kigaidi lililotokea nchini Marekani na kusababisha vifo vya watu 15.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Esmail Baqaei amelaani shambulizi hilo la kigaidi katika taarifa yake iliyotolewa jana Ijumaa.

Watu wasiopungua 15 wameuawa na wengine wapatao 35 wamejeruhiwa katika shambulio la gari na bunduki lililotokea usiku wa manane wa kuamkia siku ya kwanza ya mwaka mpya katika mji wa New Orleans nchini Marekani ambapo sherehe za mwaka mpya zilikuwa zikifanyika.

Polisi ya upelelezi ya Marekani FBI imetangaza kuwa tukio hilo lilikuwa la kigaidi na kwamba bendera ya kundi la Daesh (ISIS) ilipatikana kwenye gari lililokuwa likiendeshwa na mshambuliaji ambaye ni mzaliwa wa nchi hiyo.

Polisi wa FBI wakikagua eneo la hujuma ya kigaidi, New Orleans

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesisitiza msimamo wa Jamhuri ya Kiislamu wa kulaani ugaidi katika aina zake zote, bila kujali mahali ulipofanyika na wale waliohusika nao.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran pia ametoa mkono wa pole kwa walionusurika.

Jina la mshambuliaji huyo limetajwa kuwa ni Shamsud Din Jabbar na imebainika kwamba ni raia wa Marekani mwenye umri wa miaka 42 anayetokea jimbi la Texas. Jabbar ni mwanajeshi mstaafu wa jeshi la Marekani na amehudumia jeshi hilo huko Afghansitan kwa muda wa miaka 13.

Wahanga wa hujuma hiyo walikuwa wakisherehekea kuwasili kwa 2025, wakati shambulio hilo lilipotokea.

Popular posts from this blog

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni

Putin asaini mkataba wa kituo cha Mwezi na China