Kombora la Yemen lashambulia kambi ya kijeshi ya Wazayuni katika mji wa Ramallah
Vyombo vya habari vya Kizayuni vimetangaza kuwa komboralililovurumishwa kutoka Yemen limeipiga kambi ya kijeshi ya Israel huko Ramallah, katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu.
Vyombo hivyo vya Kizayuni vimeripoti leo kuwa kombora lililovurumishwa kutoka Yemen limeipiga kambi ya kijeshi ya Modi'in katika mji wa Ramallah.
Wakati huo huo jeshi la Israel limekiri kushindwa kulizuia kombora hilo kutoka Yemen na kueleza wa kombora moja liliingia katika anga ya Israel na kwamba walifanya kila wawezalo kuzuia vitisho dhidi yao.
Nayo televisheni ya Israel imeripoti kuwa walowezi 12 wamejeruhiwa katika shambulio hilo wakati wakihaha kutafuta sehemu ya kujificha na kwamba wengine tisa walipelekwa katika vituo vya afya kwa ajili ya matibabu baada ya kukumbwa na hofu na wasiwasi.
Ripoti nyingine kutoka ardhi zinazokaliwa kwa mabavu zinaeleza kuwa safari za ndege katika uwanja wa ndege wa Ben Gurion zimeakhirishwa.
Vikosi vya ulinzi vya Yemen (YAF) katika
siku za karibuni vimevurumisha makomora kadhaa ya masafa marefu na
ndege zisizo na rubani (droni) kuelekea katika shabaha na maeneo
mbalimbali ya Israel katika kuendelea kuwahami na kuwaunga mkono
wananchi madhulumu wa Palestina nakujibu jinai na mashambulizi ya
Israel dhidi ya Yemen.