Mamia ya Wamarekani waamua kurejea kwao barani Afrika


  • Mamia ya Wamarekani waamua kurejea kwao barani Afrika

Mamia ya Wamarekani wenye asili ya Afrika ambao hawahesabiwi kuwa ni raia wa daraja la kwanza huko Marekani, wameamua kurejea kwao barani Afrika na tayari wamepewa uraia rasmi nchini Ghana.

Taarifa za vyombo mbalimbali vya habari zinasema kuwa, wiki iliyopita, nchi ya Ghana ya magharibi mwa Afrika ilipokea kwa sherehe mamia ya raia wapya ambao ni idadi kubwa zaidi katika historia yake, walioitikia mwito wa kuwataka Wamarekani "Weusi" kurudi nyumbani. Mmoja wa Wamarekani hao ni Nykisha Madison Keita wa Germantown.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Wamarekani 524 wenye asili ya Afrika walipewa rasmi uraia wa Ghana wakati wa sherehe zilizofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Accra mji mkuu wa nchi hiyo.

Taarifa hiyo imesema kwamba, wimbi la Wamarekani wenye asili ya Afrika wanaorejea kwao barani Afrika linaongezeka siku baada ya siku.

Mamia ya Wamarekani wenye asili ya Afrika wapewa uraia nchini Ghana

 

Mmarekani mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Bowers amesema: "Mimi ni mwanamke wa Kiafrika, Uafrika ndio utambulisho wangu. Mtu unaangalia ngozi yako. Kwa hivyo hata sikuhitaji (uraia) kuniambia kuwa mimi ni Mwafrika. Huwa ninakasirika sana kwa jinsi watu wanavyonitaza popote ninapokwenda ulimwenguni kwa sababu nahisi ananidhalilisha. Watu hawaniangalii kwa jicho la Mmarekani, wananiangalia kwa ngozi yangu ya Kiafrika." 

Vilevile amesema: "Babu zangu walikuwa na hamu ya kufa ya kurudi kwao Afrika. Lakini mababu zangu hao hawakuwahi kurudi.  Walishindwa kutimiza hamu yao ya kufa ya kurejea kwao Afrika. Lakini mimi nimetimiza ndoto yao."

Serikali ya Ghana imekuwa ikiwahimiza sana Wamarekani wenye asili ya Afrika wahamie nchini humo. 

Hivi karibuni Ghana ilifanya kumbukumbu ya miaka 400 tangu watumwa wa Kiafrika walipoanza kupelekwa kwa nguvu huko Marekani. Serikali hiyo inaendesha kampeni ya "Beyond the Return" ambao ni mpango wa kiuchumi, unaolenga kuvutia uwekezaji kutoka kwa watu wanaoishi nje ya Ghana, lakini kwa wengine wengi wenye historia sawa na Bowers na familia yake, ni  fursa ya kuunganishwa tena na mizizi yao ya asili.

Dejiha Gordon, raia mwingine wa Marekani mwenye asili ya Afrika, alihamia Ghana mwaka 2019 na kufungua lori la chakula kwa ajili ya kupika chakula cha Jamaica.

Dejiha Gordon anasema: "Ninajisikia vizuri kuwepo Afrika. Kuwa na uhusiano na nchi ya Afrika kama Mwafrika sio Mmarekani, kunanifurahisha sana. Kwa sababu huko Marekani, hatuna chochote cha kufuatilia mizizi yetu, lakini Afrika ndiko iliko mizizi yetu. Hapa ninaamini kwamba nimefanya kitu cha sawa kurejea kwetu Afrika." 

Popular posts from this blog

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni

Putin asaini mkataba wa kituo cha Mwezi na China