Mripuko wa volkano walikumba eneo la Afar la katikati mwa Ethiopia

 

  • Mripuko wa volkano walikumba eneo la Afar la katikati mwa Ethiopia

Mripuko wa volcano umepiga katikati mwa Ethiopia katika Mlima Dofan, eneo ambalo hivi karibuni limekuwa na mitetemeko midogo midogo na ya mara kwa mara ya ardhi. Hayo ni kwa mujibu wa ripoti za jana Ijumaa za vyombo vya habari vya ndani ndani ya Ethiopia.

Mitetemeko hiyo imetokea katika eneo la Awash Fentale, ambalo liko umbali wa takriban maili 142 (kilomita 230) kutoka Addis Ababa, mji mkuu wa Ethiopia. Taarifa zinasema kuwa mitetemeko hiyo imehisika katika mji mkuu huo na kuzua taharuki kuhusu uwezekano wa kutokea maafa makubwa.

Katika wiki za hivi karibuni, zaidi ya mitetemeko midogo 12 ya ardhi imerekodiwa katika eneo la Awash Fentale na maeneo ya karibu na hivyo kuongeza wasiwasi kwa wakaazi wa maeneo hayo juu ya maafa yanayoweza kusambabishwa na mitetemeko hiyo.

Juhudi zinaendelea za kupunguza watu kujeruhiwa kupitia kuwahamisha wakaazi wa maeneo yaliyoko kwenye hatari zaidi na kuwapeleka katika maeneo salama. Hayo yameripotiwa na Shirika la Taifa la Utangazaji la Fana ambalo limemnukuu taarifa iliyotolewa na Abdu Ali, Msimamizi wa Mkoa ilikotokea mitetemeko hiyo.

Abdu Ali vile vile amesema: "Mitetemeko ya ardhi inaendelea kutokea na inazidi kuwa na nguvu zaidi. Hivi punde tu kabla ya kutoa taarifa hii, imehisika mjini Addis Ababa usiku kucha."

Popular posts from this blog

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni

Putin asaini mkataba wa kituo cha Mwezi na China