UN: Mashambulizi dhidi ya wafanyakazi wa misaada yameongezeka nchini Somalia


  • UN: Mashambulizi dhidi ya wafanyakazi wa misaada yameongezeka nchini Somalia

Shirika la moja la misaada ya kibinadamu la Umoja wa Mataifa limeelezea wasiwasi wake kutokana na kuongezeka mashambulizi dhidi ya wafanyakazi wanaosambaza misaada ya kibinadamu nchini Somalia. Mashambulizi hayo yaliongezeka katika robo ya nne ya mwaka ulioisha wa 2024.

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) imetangaza habari hiyo na kuongeza kuwa, jumla ya matukio 62 ya kushambuliwa wafanyakazi wa misaada ya kibinadamu yalitokea kati ya Oktoba na Desemba 2024 kote nchini humo, ikionesha ongezeko la asilimia 8.8 ikilinganishwa na matukio ya robo ya tatu ya mwaka 2024.

Katika ripoti yake hiyo, OCHA imesema: "Mashambulizi dhidi ya wafanyakazi wa misaada ya kibinadamu, mali na vifaa vyao yameendelea kuwa mengi na kupita yale yaliyotokea katika robo ya tatu ya mwaka huo." "Usalama wa wafanyakazi hao ni mdogo nchini Somalia," imesema taarifa hiyo. 

Kwa mujibu wa OCHA, wakati hali jumla ya mashambulizi imeendelea kuwa thabiti, lakini kumeshuhudiwa ongezeka katika mambo yanayozuia kufikishwa misaada hiyo, katika robo ya nne ya mwaka 2024. 

Shirika hilo la Umoja wa Mataifa limeongeza kuwa, idadi ya operesheni za kijeshi na uadui unaoendelea unakwamisha juhudi za kibinadamu na unazuia kuwafikia watu wenye mahitaji muhimu na ya dharura. 

Kwa mtazamo wa shirika la OCHA kuna wajibu wa kuongezwa jitihada za kulindwa usalama wa wafanyakazi wa misaada ya kibinadamu nchini Somalia na kupunguzwa kadiri inavyowezekana; kiwango cha mashambulizi dhidi ya mashirika ya kutoa misaada nchini humo. 

Popular posts from this blog

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni

Putin asaini mkataba wa kituo cha Mwezi na China