Utawala wa Kizayuni wakiri kuuliwa wanajeshi wake zaidi ya 800 na kujiuwa wengine 28

 

Utawala wa Kizayuni wakiri kuuliwa wanajeshi wake zaidi ya 800 na kujiuwa wengine 28

Ikiwa imepita siku 456 tangu Israel ianzishe vita dhidi ya Gaza, utawala huo umekiri kuhusu baadhi ya maafa na vipigo ulivyopata tangu kutekelezwa Oparesheni ya Kimbunga cha al Aqsa na wanamuqawama wa Palestina.

Jeshi la utawala wa Kizayuni limetangaza katika taarifa yake kuwa wanajeshi wake zaidi ya 800 wameangamizwa vitani huko Gaza tangu kuanza vita dhidi ya eneo hilo Oktoba 7 mwaka 2023. 

Ripoti ya Israel imeeleza kuwa, wanajeshi 329 wa utawala huo waliuawa wakati wa operesheni hiyo ya Oktoba 7, na wengine 390 waliuawa wakati wa operesheni ya ardhini huko Gaza. 

Jeshi la utawala wa Kizayuni pia limekiri kuwa wanajeshi wake 50 waliangamizwa katika oparesheni ya nchi kavu huko Lebanon. 

Kwa mujibu wa tangazo la jeshi la utawala wa Kizayuni, katika kipindi kilichotajwa, askari 28 wa utawala huo wakiwemo askari 16 wa kikosi cha akiba wamejiua; na Wazayuni 11 pia waliuawa katika operesheni za  Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan. 

Wanajeshi wa Israel wachoshwa na vita na kuamua kujiuwa 

Hata hivyo duru za kujitegemea sinasema idadi ya wanajeshi wa Isarel waliouawa katika vita vya Gaza na Lebanon ni mara kadhaa zaidi kuliko ile inayotangazwa na utawala huo ambao una historia ya kuficha ukweli kuhusu takwimu za kuuliwa wanajeshi wake. 

Popular posts from this blog

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni

Putin asaini mkataba wa kituo cha Mwezi na China