Venezuela yatoa donge nono kwa atakayetoa taarifa zitakazofanikisha kukamatwa kwa mgombea wa urais

 

xyz

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Edmundo González (kulia), mgombea urais aliye uhamishoni, pamoja na kiongozi wa upinzani María Corina Machado (kushoto) Julai 2024.

Serikali ya Venezuela imetangaza zawadi ya dola za kimarekani 100,000 (£81,000) kwa mtu atakayetoa taarifa zitakazofanikisha kukamatwa kwa mgombea urais wa upnde wa upinzani Edmundo González aliye uhamishoni.

Alitoroka nchini Venezuela mwezi Septemba na akapewa hifadhi ya kisiasa nchini Uhispania baada ya Venezuela kuamuru akamatwe, wakimtuhumu González kwa njama na kughushi nyaraka.

González ameapa atarejea Venezuela kabla ya kuapishwa kwa Rais Nicolas Maduro Ijumaa ijayo, akiishutumu serikali kwa kuiba kura.

Muda mfupi baada ya kitita hicho kutangazwa, González alisema anasafiri kwenda Argentina kuanza ziara yake Amerika Kusini, ambapo atakutana na Rais mkosoaji mkali wa Maduro, Javier Milei siku ya Jumamosi.

Kamati ya Haki za Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa imeiamuru Venezuela "kujizuia kuharibu" hesabu za kura za uchaguzi wa rais wa Julai 2024.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (CNE) inayoungwa mkono na serikali ilimtangaza Maduro, kuwa mshindi lakini ilishindwa kutoa hesabu za kura ili kuunga mkono ushindi huo.

Upinzani, kwa msaada wa mashahidi walioidhinishwa ulikusanya na kuchapisha zaidi ya 80% ya hesabu za kura, unasema hizo zinathibitisha kuwa mgombea wake, González, alikuwa mshindi kwa kupata wingi wa kura.

González hakuwa maarufu sana nchini Venezuela alipojiandikisha kama mgombeaji wa uchaguzi wa rais wa nchi hiyo mwezi Machi. Hakuwahi kugombea nyadhifa za umma hapo awali na hata hakujulikana sana katika duru za upinzani.

Lakini miezi kadhaa baada ya kuamua kugombea wadhifa wa juu, mwanadiplomasia huyo wa ngazi ya chini wa zamani alimshinda Maduro katika kura za maoni.

Venezuela imeshuhudia mgawanyiko kati ya serikali na wafuasi wa upinzani ukizidi kuwa mkubwa katika muongo mmoja uliopita.

Sauti ya maridhiano ya González wakati wa kampeni ya urais ilikuwa tofauti kabisa na ile ya Maduro, ambaye alionya kuhusu "umwagaji wa damu" iwapo González atashinda.

Uchaguzi wa marudio wa 2018 uliomuweka Maduro madarakani ulipuuzwa na wengi kuwa haukuwa huru na wa haki.

Popular posts from this blog

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni

Putin asaini mkataba wa kituo cha Mwezi na China