Wachunguzi wa Korea Kusini wamtaka kaimu rais arahisishe kukamatwa kwa Rais Yoon

 


g

Chanzo cha picha, Reuters/Tyrone Siu

Maelezo ya picha, Polisi wakijaribu kuwazuia watu wakati wa maandamano ya kumpinga Rais wa Korea Kusini Yoon Suk Yeol, karibu na makazi yake rasmi huko Seoul, Korea Kusini, 4, Januari 2025.

Wachunguzi wa Korea Kusini wamemtaka tena kaimu rais wa nchi hiyo Jumamosi kuamuru idara ya usalama ya rais kufuata agizo la kukamatwa kwa Rais aliyeondolewa madarakani Yoon Suk Yeol.

Siku ya Ijumaa Idara ya usalama, pamoja na wanajeshi, waliwazuia waendesha mashtaka kumkamata Yoon Suk Yeol katika mzozo uliodumu kwa saa sita ndani ya makazi ya Yoon.

Wachunguzi walipata hati ya kumkamata Yoon kutokana na tamko lake la muda mfupi la sheria ya kijeshi mwezi uliopita.

Ofisi ya Uchunguzi wa Ufisadi kwa Maafisa wa Vyeo vya Juu, ambayo inachunguza kesi hiyo, ilisema Jumamosi ilimtaka tena kaimu Rais Choi Sang-mok, waziri wa fedha wa taifa hilo, kuamuru idara ya usalama ya rais kuonyesha ushirikiano na agizo la kibali hicho.

Msemaji wa wizara ya fedha alikataa kutoa maoni yake.

g

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Kimekua kibarua kigumu mkukamata Rais Yoon Suk Yeol

Polisi walimtaka mkuu wa huduma ya usalama ya rais, Park Chong-jun, kufika kuhojiwa siku ya Jumanne, shirika la habari la Yonhap News liliripoti.

Tangazo la kijeshi la Yoon la Desemba 3 liliishangaza Korea Kusini na kupelekea kutolewa kwa hati ya kwanza ya kukamatwa kwa rais aliye madarakani.

Popular posts from this blog

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni

Putin asaini mkataba wa kituo cha Mwezi na China