Posts

Iran yaitoza Marekani faini ya dola bilioni moja kwa kuunga mkono jinai za utawala wa Kipahlavi

Image
  Apr 21, 2024 02:19 UTC Idara ya Mahakama ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeitoza Marekani faini ya dola bilioni moja kwa kuunga mkono jinai za utawala wa Kipahlavi uliokuwa madarakani Iran kabla ya Mapinduzi ya Kiislamu ya mwaka 1979. Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika Rasmi la Habari la Iran (IRNA), hukumu hiyo imetolewa katika kesi iliyowasilishwa mbele ya Tawi la 55 la Mahakama ya Umma Tehran inayoshughulikia kesi za kimataifa.  Kesi hiyo ilifikishwa mbele ya mahakama na watu 15 ambalo walikuwa wafungwa wa kisiasa Iran kabla ya Mapinduzi ya Kiislamu. Serikali ya Marekani imehukumiwa faini ya dola bilioni moja kutokana na kushiriki katika kuundwa SAVAK (Idara ya Kijasusi na Usalama wa Taifa Iran wakati wa utawala wa kifalme wa Pahlavi), na halikadhalika kutokana na uungaji mkono wake utawala wa kidikteta wa Pahlavi. Fedha hizo zinalenga kuwalipa fidia kwa walioteswa na shirika hilo la SAVAK.

Hizbullah ya Lebanon yafanya mashambulio sita dhidi ya ngome na vituo vya kijeshi vya Israel

Image
  Muqawama wa Kiislamu wa Lebanon umefanya mashambulio sita dhidi ya ngome na vituo vya kijeshi vya utawala wa Kizayuni wa Israel. Kwa mujibu wa IRNA, Hizbullah ya Lebanon imetangaza katika taarifa iliyotoa leo kwamba katika kuwaunga mkono wananchi wa Palestina katika Ukanda wa Ghaza, wapiganaji wa muqawama wa Kiislamu, wamezipiga na kuziharibu kwa kutumia silaha mwafaka zana za kijasusi za kambi ya rada ya utawala wa Kizayuni katika mashamba ya Shab'aa ya ardhi ya Lebanon yanayokaliwa kwa mabavu. Hizbullah Kabla ya hapo Hizbullah ya Lebanon ilitangaza kupitia taarifa nne tofauti kwamba imefanya shambulio la makombora na mizinga dhidi ya ngome, wanajeshi na zana za kijasusi za utawala wa Kizayuni katika kambi za Bayadh Belida, Roisat Al Alam na Al Raaheb. Muqawama wa Kiislamu wa Lebanon umelishambulia pia kwa kombora gari la kijeshi la utawala wa Kizayuni katika eneo la al-Mutla na m

Je, mvutano kati ya Israel na Iran umeisha (kwa sasa) baada ya mashambulizi ya pande zote mbili?

Image
  Saa chache baada ya vyombo vya habari vya Marekani kuripoti shambulio la moja kwa moja la Israel dhidi ya Iran, bado tunapokea taarifa zinazokinzana kutoka kwa vyanzo mbalimbali kuhusu madai ya shambulio hili. Hadi kufikia Ijumaa, misimamo ya mamlaka ya kijeshi ya Iran na vyombo vya habari vinavyohusishwa na Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) wanadokeza kwamba, kwa mtazamo wa kipropaganda, msimamo wa Iran ni kwamba hakuna jambo la maana lililotokea na kwamba hakutakuwa na mashambulizi ya kulipiza kisasi. Abdolrahim Mousavi, kamanda mkuu wa Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, alijibu maswali kuhusu hatua ya Iran hukusu shambulio la Israel kwa kusema: "Mmeona majibu ya Iran hapo awali," akimaanisha shambulio la makombora la Iran mnamo tarehe 13 mwezi wa Aprili. Zaidi ya hayo, Makao makuu ya Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran yamesema: "Hakujatokea hujuma za kigeni dhidi ya nchi." Ingawa vyombo vya habari vya Irani viliripoti shughul

Isfahan - mji wa kimkakati wa Iran ambapo milipuko ilisikika

Image
  Video zilizotumwa kwa BBC Kiajemi na wakaazi kutoka Isfahan zilionyesha milipuko juu ya mji wa Isfahan nchini Iran. Mji huu unajulikana kwa majumba yake, misikiti ya vigae na minara, Isfahan - ambapo milipuko ilisikika usiku kucha - pia ni kituo kikuu cha tasnia ya kijeshi. Ni mji wa tatu kwa ukubwa nchini Iran, unaoitwa "Nesf-e-Jahaan" au nusu ya dunia, uko katikati ya nchi karibu na milima ya Zagros. Jiji na eneo lake ni makao ya viwanda vya droni na makombora ya balestiki. Karibu nao kuna kituo cha nyuklia cha Natanz, kituo muhimu zaidi cha mpango wa kurutubisha nyuklia wa Iran. Jina Isfahan likiwa na mafungamano na vituo vya nyuklia vya Iran, ishara ya shambulio hilo haitapita bila kutambuliwa. Ikiwa hili lilikuwa shambulio la Israeli inaonekana kuwa serikali ya Benjamin Netanyahu ilikuwa ikituma ujumbe kwa Iran kwamba ina uwezo wa kushambulia maeneo nyeti katika jimbo hilo huku ikijizuia kufanya hivyo katika hatua hii. Maafisa wa Irani hawakuharakisha ku

Kambi ya jeshi la Iraq inayohifadhi wanamgambo wanaoiunga mkono Iran yashambuliwa, duru za usalama zimesema

Image
  Duru za usalama nchini Iraq zinasema kuwa mlipuko mkubwa umepiga kambi ya kijeshi ambayo ina wanamgambo wanaoiunga mkono Iran. Mjumbe wa kundi la Popular Mobilization Forces ameuawa na wengine wanane kujeruhiwa katika mlipuko huo. Makao makuu ya ulinzi ya Marekani Pentagon yaliharakisha kusema kwamba hawakuhusika katika tukio hilo. Hakuna mtu mwingine aliyesema pentagon ilihusika kwa sasa, na vyanzo vya usalama nchini Iraq bado havijasema ni nani wanaamini kuwa huenda alipanga shambulio hilo. Hii inakuja wakati kukiwa na tahadhari kubwa katika Mashariki ya Kati, wakati makabiliano ya muda mrefu kati ya Israel na Iran yameingia katika awamu mpya. Siku ya Ijumaa, shambulio linalodhaniwa kuwa la Israel lilifanyika karibu na mji wa Isfahan nchini Iran - katika jibu dhahiri la shambulio kubwa la ndege isiyo na rubani na kombora ambalo Tehran ililitekeleza dhidi ya Israeli siku sita zilizopita. Shambulio hilo pia lilikuwa ni kulipiza kisasi kwa shambulio la awali dhidi ya makamanda wakuu w

Jibu la Iran litakuwa la 'mara moja' ikiwa Israel itashambulia

Image
      Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Hossein Amirabdollahian amesema Iran itatoa jibu la haraka iwapo kutakuwa na shambulio kubwa kutoka kwa Israel. Katika mahojiano na NBC News siku ya Ijumaa, Amirabdollahian alisema ikiwa Israel itachukua hatua kinyume na maslahi ya Iran, "jibu linalofuata la nchi yake litakuwa la haraka na litakuwa katika kiwango cha juu zaidi". Amirabdollahian alipuuza shambulio linalodhaniwa kuwa la ndege zisizo na rubani za Israel dhidi ya Isfahan katikati mwa Iran, akihoji iwapo Israel ilihusika. Alisema droni ndogo zilizoshambulia zilikuwa "kama wanasesere wanaotumiwa na watoto wetu kuchezea".

Marekani yakubali kuondoa wanajeshi kutoka Niger

Image
  Taifa linaloongozwa na junta limegeukia Urusi badala yake Wanajeshi wote wa Marekani wanatazamiwa kuondoka Niger, na hivyo kumaliza jukumu lao katika mapambano dhidi ya waasi wa Kiislamu. Viongozi wa kijeshi katika taifa hilo la Afrika Magharibi wametafuta uhusiano wa karibu na Urusi tangu kutwaa mamlaka katika mapinduzi mwaka jana. Siku ya Ijumaa Marekani pia ilitangaza kuwa imekubali kufunga kituo chake cha ndege zisizo na rubani karibu na Agadez, katika jangwa la Sahara. Niger iko katika eneo la Sahel barani Afrika, ambalo linachukuliwa kuwa kitovu kipya cha kimataifa cha kundi la Islamic State. Marekani imeitegemea Niger kama ngome yake kuu katika kufuatilia shughuli za kikanda za wanamgambo wa jihadi. Ujumbe wa Marekani utaelekea katika mji mkuu wa Niger, Niamey ndani ya siku chache, ili kupanga kuwaondoa kwa utaratibu wanajeshi wake zaidi ya 1,000. Tangazo la Ijumaa linafuatia mazungumzo mjini Washington kati ya naibu waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Kurt Campbell, na Waziri