Tetesi za soka Ulaya Alhamisi 31.10.2024
Tetesi za soka Ulaya Alhamisi 31.10.2024 Chanzo cha picha, Getty Images Maelezo ya picha, Wachezaji wa Man United ambao hawapo katika mpango wa Amorim Saa 3 zilizopita Ruben Amorim tayari amezungumzia mipango yake ya uhamisho na uongozi wa Manchester United na haoni winga Antony, viungo Casemiro na Christian Eriksen au beki Victor Lindelof kama sehemu ya mipango yake. (TeamTalks) Jitihada za United kupata huduma ya Amorim zimegonga mwamba baada ya Sporting kudai pauni milioni 4 kwa wafanyikazi wake pamoja na ada ya kuachiliwa kwa meneja huyo ya pauni milioni 8.3. (Times – Subscription Required) Amorim anakubali huenda akalazimika kusubiri hadi mapumziko ya kimataifa mwezi ujao ili kujiunga na United. (Telegraph – Subscription Required) Uamuzi wa West Ham kutomteua Amorim msimu uliopita ulitokana na kutokuwa na uzoefu wa kusimamia klabu kubwa, badala ya kifedha. (Daily Mail), nje Chanzo cha picha, Getty Images Maelezo ya picha, Kocha wa Sporting Amorim Barcelona wanavut...