Je, mzozo kati ya Israel na Iran unaweza kusababisha Vita vya Tatu vya Dunia?-Gazeti la The Independent
Tunaanza ziara ya magazeti ya leo na gazeti la The Independent la Uingereza, ambalo lilihoji ni kwa kiasi gani mwelekeo wa mzozo wa sasa kati ya Israel na Iran unaweza kupanuka na kugeuka kuwa vita vya tatu vya dunia. Mtaalamu wa masuala ya Mashariki ya Kati, David B. Roberts, alielezea hofu yake juu ya uwezekano wa vita vya kikanda kugeuka kuwa kitu kikubwa zaidi, kinachohitaji kuingilia kati kwa nguvu za kikanda pamoja na nchi za nje ya ukanda kama vile Marekani na Uingereza. Amesisitiza kuwa, Tehran ilitoa onyo la kutosha kwa Israel na Marekani kuhusu mpango huo, na kuruhusu muungano wa dharura kujiandaa kwa mashambulizi yanayokaribia, na Tehran haikuiomba Hizbullah kutumia makombora yake 150,000. Mwandishi anasema kwamba uongozi wa Iran ulitaka kulipiza kisasi dhidi ya Israeli, lakini bila kupiga pigo kubwa kwa kiwango ambacho kingesababisha kisasi kikubwa cha Israeli na labda ushiriki wa Marekani. Wasiwasi unaongezeka sana kuhusiana na hali ambapo Israel inalenga m