Rais wa Venezuela: Marekani na EU zinanyamazia kimya jinai za Kinazi za Israel huko Gaza
ay 30, 2024 02:30 UTC Rais wa Venezuela amezilaani Marekani na Umoja wa Ulaya kwa kutofanya lolote kukomesha mauaji "ya kutisha" ya Israel dhidi ya Wapalestina. Nicolas Maduro amelaani vikali mauaji yanayotekelzwa na Israel katika Ukanda wa Gaza na kuyafananisha na jinai za kutisha zaidi katika historia. Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Maduro alielezea hatua ya jeshi la Israel kulenga kambi ya watu waliokimbia makazi yao katika mji wa Rafah katika Ukanda wa Gaza mauaji ya umati na kuongeza kuwa hivi sasa katika eneo zima la Ukanda wa Gaza Israel inatekeleza mauaji ya kimbari ya kutisha zaidi ambayo ubinadamu umeshuhudia tangu wakati wa Hitler." " Amebainisha masikitiko yake kuwa Israel inaendeleza mauaji ya kimbari tika Ukanda wa Gaza mbele ya macho ya ulimwengu bila mtu yeyote kuizuia." Aliikosoa Marekani na Umoja wa Ulaya na kusema pamoja na ku