Posts

Watu 38 wafariki baada ya mashua kuzama Yemen - maafisa

Image
  Takriban watu 38 kutoka eneo la upembe wa Afrika wamefariki baada ya mashua yao kuzama katika pwani ya Yemen, maafisa wa eneo hilo wamesema. Walionusurika wamewaambia waokoaji kuwa mashua hiyo iliyokuwa imebeba takriban watu 250 ilizama kutokana na upepo mkali. Msako unaendelea kuwatafuta karibu watu 100 ambao bado hawajapatikana. Mamlaka za mitaa huko Rudum, mashariki mwa Aden, zilisema kwamba waliokuwemo walikuwa wahamiaji, wengi wao kutoka Ethiopia, ambao hutumia Yemen kama njia ya kupita kuelekea maeneo ya Ghuba. Hadi Al-Khurma, mkurugenzi wa wilaya ya Rudum, ameliambia shirika la habari la Reuters kuwa boti hiyo ilizama kabla ya kufika ufukweni. "Wavuvi na wakaazi walifanikiwa kuwaokoa wahamiaji 78, ambao waliripoti kuwa wengine 100 waliokuwa nao kwenye boti moja hawapo. "Msako bado unaendelea, na Umoja wa Mataifa umearifiwa kuhusu tukio hilo," alisema. Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, wahamiaji 97,000 waliwasili Yemen kutoka upembe wa Afrika mwaka jana. Ongezeko h

'Mimi ni mtesaji wa wabaguzi wa rangi' - Vinicius jr

Image
Mshambulizi wa Real Madrid, Vinicius Jr anasema ni "mtesaji wa wabaguzi wa rangi" baada ya mashabiki watatu wa Valencia kuhukumiwa kifungo cha miezi minane jela kwa kosa la kumtusi kwenye mechi. Nyimbo zao za kibaguzi zilimlenga Vinicius wakati wa mchezo wa La Liga kwenye Uwanja wa Mestalla huko Valencia mnamo Mei 21, 2023. Mashabiki hao walipatikana na hatia ya "uhalifu dhidi ya uadilifu wa maadili" na "hali inayozidisha ubaguzi kulingana na nia za kibaguzi". "Mimi si mwathirika wa ubaguzi wa rangi. Mimi ni mtesaji wa wabaguzi wa rangi. Hukumu hii ya kwanza ya uhalifu katika historia ya Uhispania sio yangu. Ni ya watu wote weusi," Vinicius alichapisha kwenye X. "Wabaguzi wengine waogope, waaibike na wajifiche kwenye vivuli. Vinginevyo, nitakuwa hapa kukusanya. Asante kwa La Liga na Real Madrid kwa kusaidia na hukumu hii ya kihistoria." Ni mara ya kwanza kwa hukumu ya ubaguzi wa rangi katika mechi ya soka nchini Uhispania kutolewa na i

Waathiriwa wa msukosuko uliotokea katika shirika la ndege la Singapore kufidiwa

Image
  Shirika la ndege la Singapore limejitolea kuwalipa fidia wale waliojeruhiwa kwenye safari ya ndege ya London kwenda Singapore iliyokumbana na misukosuko mikali. Shirika hilo la ndege lilisema linajitolea kuwalipa $10,000 (£7,800) wale waliopata majeraha madogo, katika chapisho la Facebook. Kwa abiria walio na majeraha mabaya zaidi, shirika la ndege linatoa "malipo ya mapema ya $25,000 kushughulikia mahitaji yao ya haraka" na majadiliano zaidi ili kukidhi "hali zao". Abiria wa Uingereza mwenye umri wa miaka 73 alifariki na wengine kadhaa kujeruhiwa wakati ndege ya SQ 321 ilipokumbana na misukosuko nchini Myanmar na kuelekezwa Thailand mwezi Mei. Shirika la ndege la Singapore bado halijajibu ombi la BBC kuhusu ni watu wangapi wanastahili malipo hayo. Zaidi ya watu mia moja waliokuwa kwenye SQ 321 walitibiwa katika hospitali ya Bangkok kufuatia ya tukio hilo. Uchunguzi wa mapema ulionyesha kuwa ndege hiyo iliongeza kasi ya juu na chini, na kushuka karibu

Wanajeshi wa Korea Kusini wafyatua risasi za onyo baada ya wanajeshi wa Kaskazini kuvuka mpaka

Image
Wanajeshi wa Korea Kusini walifyatua risasi za onyo baada ya wanajeshi wa Korea Kaskazini kuvuka mpaka kimakosa, jeshi la Seoul lilisema Jumanne. Tukio hilo lililotokea katika eneo lisilo la kijeshi (DMZ) siku ya Jumapili linajiri huku mvutano ukiendelea kuongezeka kati ya mataifa hayo ya Korea. Kundi dogo la wanajeshi wa Korea Kaskazini lililokuwa limebeba vifaa vya shambani ikiwemo shoka liliingia Korea Kusini saa 12:30 kwa saa za huko (05:30 GMT), jeshi la Seoul liliripoti. Walikuwa miongoni mwa watu 20 waliokuwa katika eneo la mpaka wakati huo. Walirudi nyuma mara tu baada ya Wakorea Kusini kufyatua risasi za kutoa onyo. Katika wiki za hivi karibuni, Kaskazini imepeperusha mamia ya puto zilizojaa taka hadi miji ya mpakani Kusini. Seoul imejibu kwa kutangaza propaganda na muziki wa K-pop hadi Kaskazini kwa kutumia vipaza sauti. Wanaharakati pia wamerusha puto za propaganda kuelekea Kaskazini. Hakukuwa na harakati mashuhuri kutoka Kaskazini mwa DMZ baada ya wanajeshi wake kurudi Jum

Watu wenye silaha Nigeria wamewauwa watu 25 katika uvamizi wa kijiji - Maafisa

Image
  Takriban watu 25 wameuawa na wengine kutekwa nyara na watu wenye silaha katika jimbo la Katsina kaskazini magharibi mwa Nigeria, mamlaka zimesema. Makumi ya watu waliokuwa na bunduki wakiwa na pikipiki walivamia eneo la Yargoje huko Kankara Jumapili jioni, kamishna wa masuala ya usalama wa serikali, Nasiru Babangida Mu'azu, aliambia BBC Hausa. Mashambulizi ya magenge yenye silaha - yanayojulikana kama majambazi - kaskazini-magharibi na katikati mwa Nigeria yamekuwa ya kawaida, na mamlaka inaonekana kukosa uwezo wa kuyazuia, licha ya madai ya serikali na vikosi vya usalama kwamba wanafanya kazi kumaliza ukosefu wa usalama ulioenea. Wakazi waliambia BBC kwamba makumi ya watu waliokuwa na bunduki wakiwa kwenye pikipiki waliingia katika jamii, wakifyatua risasi kiholela na kupora maduka kabla ya kuwateka nyara idadi isiyojulikana ya wanakijiji." Watu waliouawa na majambazi ni zaidi ya 50, kwa sababu baadhi ya maiti bado zinatolewa porini," alisema mkazi mmoja

Hamas kuunga mkono makubaliano ya amani ya Gaza ni 'ishara ya matumaini' - Marekani

Image
  Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken alisema Jumanne tamko la Hamas la kuunga mkono azimio la Umoja wa Mataifa linalounga mkono pendekezo la kusitishwa kwa vita vya Gaza ni "ishara ya matumaini" ingawa taarifa kutoka kwa uongozi wa kundi hilo ilikuwa muhimu. Mazungumzo kuhusu mipango ya Gaza baada ya vita vya Israel na Hamas kumalizika yataendelea Jumanne mchana na katika siku chache zijazo, Blinken alisema mjini Jerusalem baada ya mazungumzo na viongozi wa Israel. "Ni muhimu kuwa na mipango hii." Blinken alikutana na maafisa wa Israel siku ya Jumanne katika msukumo wa pamoja wa kumaliza vita vilivyodumu kwa miezi minane siku moja baada ya pendekezo la Rais Joe Biden la kusitisha mapigano kupitishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Kabla ya safari ya Blinken, Israel na Hamas zote mbili zilirudia misimamo mikali ambayo imedhoofisha upatanishi wa hapo awali wa kumaliza mapigano, wakati Israel inaendelea na mashambulio katikati na kusini mwa Gaz

Urusi yaanza hatua ya pili ya mazoezi ya kimkakati ya silaha za nyuklia na Belarus

Image
  Urusi ilisema Jumanne kwamba wanajeshi wake wameanza hatua ya pili ya mazoezi ya kupeleka silaha za nyuklia pamoja na wanajeshi wa Belarusi baada ya kile Moscow ilisema ni vitisho kutoka kwa madola ya Magharibi. Urusi inasema Marekani na washirika wake wa Ulaya wanaisukuma dunia kwenye ukingo wa makabiliano ya nyuklia kwa kuipa Ukraine silaha zenye thamani ya mabilioni ya dola, baadhi ya silaha hizo zikitumiwa dhidi ya ardhi ya Urusi. Tangu kutuma maelfu ya wanajeshi nchini Ukraine mnamo Februari 24 2022, Rais Vladimir Putin amesema mara kwa mara Urusi inaweza kutumia silaha za nyuklia kujilinda katika hali mbaya zaidi, maoni ambayo mataifa ya Magharibi yamepuuzilia mbali kuwa ni makelele. Urusi mwezi uliopita ilihusisha kwa uwazi majaribio ya nyuklia yaliyoagizwa na Putin na kile ilichosema ni "kauli za uchochezi na vitisho vya maafisa fulani wa Magharibi dhidi ya Shirikisho la Urusi". Katika hatua ya kwanza ya mazoezi hayo, wanajeshi wa Urusi walipata mafunzo ya jinsi ya