Posts

Urusi yapinga msaada mpya wa Marekani kwa Ukraine

Image
  Sheria iliopo tangu Urusi ilipovamia Ukraine kwa kiwango kikubwa ni kwamba kile ambacho ni kizuri kwa Kyiv ni kibaya kwa Moscow. Jumamosi iliyopita ilileta habari njema kwa serikali ya Ukraine. Bunge la Wawakilishi la Marekani lilipiga kura kuunga mkono kifurushi cha msaada cha $61bn (£49bn) kwa Kyiv, ambacho kitatumika kulipatia jeshi lake silaha. Bunge pia liliidhinisha muswada ambao utaruhusu kukamatwa na kuhamishiwa Ukraine mali ya Urusi iliyohifadhiwa Marekani. Miswada hiyo sasa inapelekwa kwa Seneti ili kuidhinishwa. Haishangazi, ni kwanini hatua hii haikupokelewa vyema mjini Moscow.Rais wa zamani Dmitry Medvedev alilaani "dola bilioni 61 za umwagaji damu". Alitoa wito wa kuwepo kwa Vita vipya vya Wenyewe kwa Wenyewe kwa Waamerika ambavyo "hatimaye vitasababisha kuvunjika vibaya kwa himaya ya uovu ya Karne ya 21, Marekani". Katika kipindi chake kikuu cha televisheni cha serikali Jumapili usiku, mtangazaji Vladimir Solovyov alielezea wazo la kuhamis...

Mkuu wa Ujasusi wa jeshi la Isrel ajiuzulu

Image
    Mkuu wa kijasusi wa jeshi la Israel amejiuzulu, akisema alichukua jukumu la kushindwa kabla ya shambulio la Hamas dhidi ya Israel tarehe 7 Oktoba. Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) lilisema Meja Jenerali Aharon Haliva atastaafu pindi mrithi wake atakapochaguliwa. Katika barua, alikiri kwamba kurugenzi yake ya ujasusi "haikutimiza kazi tuliyokabidhiwa". Yeye ndiye mtu wa kwanza mkuu kujiuzulu kutokana na shambulio hilo ambalo lilikuwa baya zaidi katika historia ya Israel. Wanajeshi na maafisa wa ujasusi wa Israel walikosa au kupuuza maonyo mengi kabla ya mamia ya watu wenye silaha wa Hamas kuvunja uzio wa mpaka wa Gaza siku hiyo na kushambulia jamii za karibu za Israel, kambi za kijeshi na tamasha la muziki. Takriban Waisrael 1,200 na raia wa kigeni - waliuawa na wengine 253 walirejeshwa Gaza kama mateka, kulingana na hesabu za Israel. Israel ilijibu kwa kuanzisha vita vyake vikali zaidi kuwahi kutokea Gaza kwa malengo ya kuangamiza Hamas na kuwakomboa mateka. Zaidi ya Wapal...

Israel na Hamas: Nini kimetokea kwa Hamas baada ya miezi sita ya vita Gaza?

Image
  Chanzo cha picha, Reuters Maelezo ya picha, Kabla ya tarehe 7 Oktoba Hamas ilikadiriwa kuwa na wapiganaji wapatao 30,000. Saa 1 iliyopit Miezi sita imepita tangu shambulio la Hamas dhidi ya Israel kufanyika kwa mara ya kwanza tarehe 7 Oktoba,2023, ambapo watu 1,200 waliuawa na zaidi ya 200 kuchukuliwa mateka. Katika kukabiliana na shambulio hili, Israel iliahidi "kuliangamiza na kulimaliza kundi la Hamas" ili lisiwe tishio tena, na kuanzisha operesheni kubwa ya kijeshi huko Gaza ambayo imesababisha vifo vya watu zaidi ya 33,000, kwa mujibu wa Wizara ya Afya ya kundi hili. Israel inasema imewaua maelfu ya wapiganaji wa Hamas na kuharibu sehemu kubwa ya mahandaki ambayo wanamgambo wa Kipalestina waliyajenga chini ya Gaza na kutumika kutekeleza mashambulizi yao. Lakini je, Israel imefanikisha lengo lake la kuliangamiza kundi hilo la wanamgambo? Na Wapalestina sasa wanafikiria nini kuhusu viongozi wao na viongozi wa Hamas huko Gaza baada ya vita vya umwagaji damu ...

Rais wa Iran anaitembelea Pakistan siku ya Jumatatu

Image
  Rais wa Iran, Ebrahim Raisi. March 20, 2024. (Iranian Presidency Office via AP) Tangazo kutoka wizara ya mambo ya nje ya Islamabad lilisema ziara hii itatoa fursa muhimu kuimarisha uhusiano wa nchi mbili Rais wa Iran Ebrahim Raisi atawasili katika nchi jirani ya Pakistan Jumatatu kwa ajili ya mikutano rasmi na viongozi wa taifa hilo huku kukiwa na mivutano kati ya Iran na Israel. Tangazo kutoka wizara ya mambo ya nje ya Islamabad leo Jumapili lilisema kuwa mazungumzo hayo yatatoa fursa muhimu ya kuimarisha uhusiano wa nchi mbili na ushirikiano katika biashara, mawasiliano, nishati, na kilimo. Tangazo lilisema ujumbe wa ngazi ya juu wa Raisi utawajumuisha waziri wa mambo ya nje wa Iran, mawaziri wengine na wawakilishi wa biashara. Wakati wa ziara yake ya siku tatu nchini Pakistan, rais wa Iran anatarajiwa kukutana na mwenzake, Asif Ali Zardari, na Waziri Mkuu Shehbaz Sharif, miongoni mwa wengine. Taarifa ya Pakistan imesema bila kufafanu...

Rais wa Ukraine asema nchi yake ina nafasi ya ushindi dhidi ya Russia kwa msaada mpya wa silaha

Image
  dakika 38 zilizopita Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky akiwa na wanajeshi wa Ukraine mbele ya ishara ya barabara inayoashiria lango la eneo la Donetsk, katikati ya Russia. (Ofisi ya rais wa Ukraine / AFP). Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy alisema Jumapili kwamba nchi yake ina nafasi ya ushindi dhidi ya Russia na msaada mpya wa silaha kwa wanajeshi wa Kyiv ambao unakaribia kuidhinishwa na Bunge la Marekani  na kuungwa mkono na Rais Joe Biden. Baraza la Wawakilishi la Marekani likiwa dhidi ya upinzani wa upande wa mrengo wa kulia wa chama cha Republican walio wengi katika bunge hilo, walipiga kura Jumamosi kwa dola bilioni 60.8 kama msaada mpya wa kijeshi kwa Ukraine, huku Seneti ikitarajiwa kupitisha hatua hiyo wiki hii na kisha Biden kutia saini. Nadhani msaada huu utaimarisha vikosi vya jeshi, natoa maombi ambayo tunahitaji sana, ambayo maelfu ya wanajeshi wanahitaji sana Zelenskyy aliambia kipindi cha Meet the Pres...

Hoja za ufunguzi zinatarajiwa kuanza katika kesi ya New York inayomkabili Donald Trump

Image
  Aliyekuwa Rais wa Marekani, Donald Trump akiwasili katika mahakama ya jinai ya Manhattan akiwa na timu yake ya wanasheria huko New York, NY siku ya Jumatatu, Aprili 15, 2024. Jabin Botsford.REUTERS. Hoja za ufunguzi zinatarajiwa kuanza Jumatatu katika kesi ya New York inayomkabili Donald Trump, kesi ya kwanza ya jinai kuwahi kuwasilishwa dhidi ya rais wa zamani wa Marekani. Hoja za ufunguzi zinatarajiwa kuanza Jumatatu katika kesi ya New York inayomkabili Donald Trump, kesi ya kwanza ya jinai kuwahi kuwasilishwa dhidi ya rais wa zamani wa Marekani. Katika kuwasilisha kwa jopo la mahakama la watu 12 waendesha mashtaka wana uwezekano wa kudai kwamba Trump alipanga njama mwaka 2016, kabla ya kampeni yake ya White House iliyofanikiwa, kuficha malipo ya fedha kwa wanawake wawili ili kuficha madai yao ya mahusiano nae ya kimapenzi nje ya ndoa. Waendesha mashtaka wanadai kwamba Trump alikuwa akitaka kuendelea kuficha taarifa za hatari kwake ...

Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Iran ashukuru majeshi kwa utendaji mzuri katika matukio ya hivi karibuni

Image
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa: "Vikosi vya kijeshi vimeonyesa taswira nzuri ya uwezo na mamlaka yao, na pia taswira yenye kupongezwa ya taifa la Iran, sambamba na kuthibitisha kuibuka kwa uwezo wa irada wa taifa la Iran katika uga wa kimataifa. Kwa mujibu wa kituo cha habari cha Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Khamenei katika kikao na makamanda wakuu wa Majeshi ya Iran ametoa pongezi kwa mnasaba wa Siku ya Jeshi na pia kumbukumbu ya kuasisiwa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, na kusema: "Mafanikio ya hivi karibuni ya jeshi yameibua hisia ya utukufu kuhusu Iran ya Kiislamu mbele ya walimwengu na weledi wa mambo duniani." Ayatullah Khamenei amepongeza kuwepo utaratibu wa mipango sahihi katika harakati za jeshi  na kusema: "Matukio mbalimbali yana gharama na faida,...