Posts

Biden apata shinikizo la kuruhusu silaha za Marekani kuishambulia Urusi

Image
  Shinikizo linaongezeka kwa Rais wa Marekani Joe Biden kuruhusu Ukraine kutumia silaha zinazotolewa na nchi za Magharibi kushambulia eneo la Urusi. Washirika kadhaa wa Marekani wiki hii waliashiria kuwa wako tayari kwa uwezekano huu. Rais wa Urusi Vladimir Putin ameonya kuhusu "athari kubwa", hasa kwa kile alichokiita "nchi ndogo" barani Ulaya. Siku ya Jumatano, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken alisema msimamo wa Washington kuhusu suala hilo "utabadilika na kurekebishwa" kulingana na mabadiliko ya hali ilivyo vitani. Kwa sasa yuko katika mji mkuu wa Czech, Prague, kwa mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa Nato. Msemaji wa usalama wa taifa wa White House John Kirby alisema jioni Jumatano kwamba ingawa uungaji mkono wa Marekani kwa Ukraine umebadilika, "hivi sasa, pia hakuna mabadiliko katika sera yetu". Ukraine imekuwa ikijitahidi kukabiliana na mashambulizi ya Urusi mashariki mwa nchi hiyo, huku jiji la Kharkiv likikumbwa na ma

Kila mwanachama wa NATO ana wanajeshi huko Ukraine - Estonia

Image
   Kila mwanachama wa NATO ana wanajeshi huko Ukraine - Estonia Washauri na wakufunzi wa nchi za Magharibi wanaunga mkono kikamilifu vikosi vya Kiev dhidi ya Urusi, waziri wa ulinzi amesema Kila mwanachama wa NATO tayari ana wanajeshi nchini Ukraine, Waziri wa Ulinzi wa Estonia Hanno Pevkur alidai Jumatatu. Hata hivyo, kwa hali yoyote hakuna vikosi vya muungano unaoongozwa na Marekani vitashiriki katika uhasama dhidi ya Urusi, waziri huyo alisisitiza katika mahojiano na chombo cha habari cha Austria cha Die Presse. Wanajeshi wa NATO wanafanya kazi katika nchi iliyozozaniwa kama washauri na wanahusika katika kutoa mafunzo kwa wanajeshi wa Ukraine huko Poland, Uingereza na Estonia, Pevkur aliambia chombo. Maafisa wa ulinzi wa nchi za Magharibi kwa sasa wanapanga kuweka kambi za mafunzo nchini Ukraine katika jitihada za kuepuka masuala ya kuvuka mpaka na kuharakisha mchakato wa maandalizi, aliongeza. Wakati huo huo, Pevkur alisisitiza kuwa hakuna mazungumzo ya wanajeshi wa NATO kupigana m

TAZAMA mwanajeshi wa Urusi akishambulia mtaro wa Kiukreni

Picha za POV zilizopatikana na RT zinaonyesha mapigano makali ya karibu Picha za kamera za mwili zilizopatikana na RT zinaonyesha askari wa Urusi akivamia maeneo ya Ukrainia na kusafisha mitaro. Video hiyo ilirekodiwa na mtumishi mwenyewe. Klipu hiyo inaanza na askari kuingia kwenye mtaro na kufyatua bunduki ya kushambulia. Mwanamume huyo anarusha bomu na kishindo na mlio usio na sauti unasikika kwa nyuma. Askari huyo anaingia kwenye shimo, ambapo miili mitatu imelala chini karibu na makreti ya risasi na silaha ya kukinga mizinga. Kulingana na RT Russian, mfumo wa kombora unaoongozwa na Uswidi-Uingereza NLAW na kirusha guruneti cha Uswidi AT-4 zilipatikana kwenye mtaro na wanajeshi wa Urusi. Tarehe na eneo kamili ambapo video ilirekodiwa haijathibitishwa. Mwanajeshi aliyekufa aliyeonekana kwenye video hiyo alikuwa amejihami kwa bunduki ya kivita iliyotengenezwa Marekani na alikuwa amevalia sare yenye kiraka cha Kikosi cha Telemark cha Norway, RT Russian ilisema. Uraia wa mwanajeshi huy

Jeshi la Sudan lakataa wito wa Marekani wa kuzungumza na waasi

Image
Jeshi la Sudan limekataa wito wa kurejea kwenye mazungumzo ya usitishaji vita na kundii la waasi la RSF kufuatia mazungumzo kati ya kiongozi wa Sudan Jenerali Abdel Fattah al-Burhan na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken. Blinken alimpigia simu al-Burhan juzu ambapo alijaribu kumshawishi afanya mazungumzo na waasi wa RSF. Afisa mwandamizi wa Sudan Malik Agar amapinga uingiliaji wa Marekani na kusema: "Hatutakwenda Jeddah (Saudi Arabia) na yeyote anayetutaka atuue katika nchi yetu na kuipeleka miili yetu huko." Marekani imekuwa ikisiamamia mazungumzo hayo ya waasi na serikali ya Sudan huko Jeddah. Hatahivyo mazungumzo hayo hadi sasa hayajafanikiwa. Mapigano makali yaliendelea Jumatano katika maeneo ya kaskazini mwa mji mkuu, huku wakaazi wakiripoti mashambulizi makali ya angani na mizinga. Sudan hataivyo imekaribisha mwaliko wa Misri wa mkutano wa kilele wa makundi

Usajili wa wagombea wa uchaguzi mapema wa rais wa Iran waanza

Image
Iran leo imezindua mchakato wa siku tano wa usajili kwa watu wanaotarajia kugombea katika uchaguzi wa 14 wa rais kuchukua nafasi ya Ebrahim Raisi aliyekufa shahidi maisha katika ajali ya helikopta mapema mwezi huu. Rais, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Hossein Amir-Abdollahian na wengine sita walikufa shahidi Mei 19, wakati helikopta yao ilipoanguka katika hali mbaya yaa hewa ya ukungu katika milima karibu na mpaka wa kaskazini-magharibi mwa nchi. Wagombea wote lazima waidhinishwe na Baraza la Walinzi wa Katiba lenye  wanachama 12. Hicho ni chombo kikuu cha usimamizi wa uchaguzi nchini. Wizara ya Mambo ya Ndani itatangaza majina ya walioidhinishwa tarehe 11 Juni. Kufuatia kufa shahidi Rais Rasi na wenzake, wakuu wa mihimili mitatu ya dola nchini Iran walikubaliana Jumatatu kwamba uchaguzi wa rais wa haraka utafanyika tarehe 28 Juni. Kulingana na ratiba iliyotangazwa na serikali, kampeni z

Makamba: Mataifa ya Afrika yawe na haki ya kuchagua washirika

Image
  Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania January Makamba Kila taifa la Afrika na bara zima lazima liwe na uwezo wa kujitegemea katika kuchagua washirika wake na kulinda maslahi yake binafsi Makamba amenukuliwa na Shirika la Habari la Sputnik la Russia akisema: "Sisi [Waafrika] tunaona inakera kushinikizwa kuchagua mshirika huyu mmoja au mwingine." Aidha amesema uhuru wa kweli na uhuru wa Afrika unaweza kupatikana kwa kujitegemea na kwa umoja. Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania pia alikosia mataifa ya kikoloni na mataifa mengine ya Magharibi kwa kujaribu kurejesha satwa yao ya kibeberu  Afrika, jambo ambalo linazifanya nchi kama Niger, Mali, na Burkina Faso "kuwafukuza" wakoloni wao wa zamani. Makamba ameendelea kusema kuwa: " Nchi za Ulaya, na hasa Marekani, hivi sasa, zinajaribu kurejea tena kwa kasi Afrika." Hivi karibuni Ufaransa imekuwa ikipata hasara kubwa ba

Zoezi la kuhesabu kura Afrika Kusini laendelea huku ANC ikikabiliwa na uwezekano wa kupoteza viti

Image
Zoezi la kuhesabu kura linaendelea Afrika Kusini baada ya uchaguzi wa Jumatano uliokuwa na ushindani mkali huku chama tawala ANC kikikabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa wanasiasa waliojiondoa katika chama hicho. Matokeo ya awali yanaonyesha ANC itapoteza wingi wa viti bungeni. Tume Huru ya Uchaguzi (IEC) imesema upigaji kura wa dakika za mwisho katika miji mikubwa ulipelekea kuongezwa muda wa kupiga kura. Chama cha ANC kimetawala siasa za Afrika Kusini tangu 1994 wakati kiongozi wa ukombozi Shujaa Nelson Mandela aliposhinda uchaguzi wa kwanza wa kidemokrasia nchini humo. Kura za maoni zinaonyesha kuwa ANC inaweza kushinda takribani asilimia 40 ya kura, kutoka asilimia 57 mwaka 2019, lakini hakuna chama cha upinzani kinachotarajiwa kupata zaidi ya asilimia 25 ya viti. Iwapo ANC itafanya vyema na kupata karibu asilimia 50 inaweza kushirikiana na baadhi ya vyama ndogo na vyama vya kikanda