Ukraine inasonga mbele katika maeneo mengi huko Kursk - Zelensky
Ukraine inasonga mbele katika maeneo mengi huko Kursk - Zelensky Rais Volodymyr Zelensky anasema kuwa vikosi vya Ukraine vinaendelea kusonga mbele zaidi katika eneo la Kursk nchini Urusi. Katika ujumbe kwenye mitandao ya kijamii, kiongozi huyo wa Ukraine anasema vikosi vimesonga mbele umbali wa kilomita moja hadi mbili katika maeneo mbalimbali leo. BBC haiwezi kuthibitisha hili kwa uhuru na haina uhakika ni kiasi gani hasa eneo la Urusi limetwaliwa.