Viongozi wa harakati za Palaestina za Hamas na Jihad Islami wakutana Tehran
Ismail Haniyah, mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas, amekutana mjini Tehran na Katibu Mkuu wa Harakati ya Palestina ya Jihad Islami Ziyad al-Nakhaleh. Hamas ilisema katika taarifa yake siku ya Ijumaa kwamba mkutano huo ulilenga kujadili matukio ya kisiasa na ya medani kuhusiana na vita vya mauaji ya halaiki vinavyoendelezwa na utawala haramu wa Israel dhidi ya watu wa Gaza. Wajumbe wa pande zote mbili wamesifu harakati za muqawama na watu wa Gaza katika kukabiliana na uvamizi wa Israel. Taarifa hiyo imesema: "Aidha, viongozi hao wawili wamejadili juhudi za kukomesha vita, na kusisitiza kwamba mafanikio ya mazungumzo yoyote yasiyo ya moja kwa moja yanategemea mambo manne ya kimsingi: kusimamishwa kabisa vita, kuondoka kikamilifu wanajeshi vamizi wa Isarel katika ukanda wote wa Gaza; kurudi kwa watu waliokimbia makazi yao, kuingia misaada na mahitaji ya msingi kwa watu wa gaza, pamoja na kubadilishana wa...