Mtandao mkubwa wa uhalifu kwa njia ya kompyuta wafungwa duniani: Marekani
Idara za kipolisi kote ulimwenguni kote zimefunga mtandao wa kimataifa wa programu ambao uliiba $5.9bn (£4.65bn) na unahusishwa na uhalifu mwingine, Wizara ya Sheria ya Marekani (DOJ) imesema. DOJ ilishirikiana na FBI na mashirika mengine ya kimataifa ili kuondoa kile kinachowezekana kuwa mtandao wa kompyuta zilizoathiriwa na programu ambazo ziko chini ya udhibiti wa mtu mmoja. Raia wa China YunHe Wang, ambaye pia ni mkazi wa St Kitts na Nevis citizen ameshtakiwa kwa kuunda na kuendesha mtandao huo. Bw Wang anashtakiwa kwa njama ya kufanya ulaghai kwa njia ya mtandao wa kompyuta, njama ya kufanya ulaghai kwa njia ya mtandao na kula njama ya kutakatisha pesa. Iwapo atapatikana na hatia kwa makosa yote, anakabiliwa na adhabu ya juu zaidi ya miaka 65 jela. Kulingana na shtaka, kati ya 2014 hadi 2022, Bw.Wang na wengine waliunda na kuendesha mtandao uitwao 911 S5, kutoka kwa seva 150 kote ulimwenguni. Mtandao huo ulidukuliwa katika zaidi ya anwani milioni 19 za Itifaki ya Mtan