Posts

Vito vya thamani ya £10m vyaibiwa kutoka nyumbani London

Image
  Chanzo cha picha, Met Police Bidhaa hizo ni pamoja na vipande vya Katherine Wang, De Beers na Van Cleef Vito vya thamani ya zaidi ya pauni milioni 10 pamoja na mikoba ya wabunifu yenye thamani ya £150,000 vimeibwa kutoka katika nyumba moja huko St John's Wood jijini London. Chanzo cha picha, Met Police Maelezo ya picha, Mikoba ya Hermes Crocodile Kelly yenye thamani ya £150,000 ilichukuliwa Chanzo cha picha, Met Police Maelezo ya picha, Wapelelezi wanasema vitu vingi vilivyoibiwa ni vya muundo wa kipekee Mzungu mwenye umri wa kati ya miaka 20 hadi 30 alivamia nyumba moja majira ya kati ya kumi na moja jioni na saa kumi na moja unusu jioni ambapo alipanda kupitia dirisha la ghorofa ya pili, Polisi wa London walisema. Alichukua mikoba ya Hermes Crocodile Kelly, pesa taslimu £15,000 pamoja na vito vya thamani ya pauni milioni £10.4 Wamiliki wa nyumba wametoa zawadi ya pauni 500,000 kwa habari zitakazopelekea kukamatwa na kutiwa hatiani kwa mshukiwa.

Urusi yazindua mashambulizi makubwa ya makombora dhidi ya maeneo mbali mbali ya Ukraine

Image
  Chanzo cha picha, Reuters Urusi imefanya kufanya mashambulizi mapya makubwa ya kombora dhidi ya Ukraine. Mifumo ya ufuatiliaji habari za kivita za Ukreni zinaripoti kuwa mashambulizi hayo yamehusisha makombora ya cruise na balestiki na milipuko iliyozinduliwa na Warusi katika mkoa wa Kyiv, Vasilkov katika mkoa wa Kyiv, Shostka katika mkoa wa Sumy na maeneo mengine. Aidha kuna ripoti za kurushwa kwa makombora ya aeroballistic ya Kinzhal kutoka kwenye ndege ya MiG-31. Jeshi la Ukraine pia linaripoti kuwa ndege sita za Urusi za mashambulizi ya kimkakati ya Urusi zilizosafiri kwenye anga lake zilirusha makombora. Watu saba walijeruhiwa katika eneo la Kherson kutokana na mashambulizi ya makombora ya Urusi, huku majengo kadhaa yakiharibiwa. Utawala wa kijeshi wa Kyiv unaripoti kwamba wakati wa kurudisha nyuma shambulio la kombora la Urusi, vifusi vya roketi vilianguka kwenye nyumba ya kibinafsi kusini mashariki mwa mji mkuu.

Idadi ya watoto wanaofariki kwa baridi kali Gaza yafikia sita

Image
  Maelezo ya picha, Babake Sila akiwa amebeba mwili wa kichanga hicho kwenda kuuzikwa Binti Sila alikuwa na umri wa chini ya wiki tatu wakati mama yake Nariman alipogundua kuwa hatikisiki tena. "Niliamka asubuhi na kumwambia mume wangu kuwa mtoto alikuwa hajatikisika kwa muda. Alifunua uso wake na kumkuta amekuwa wa bluu, ametafuna ulimi, huku damu zikimtoka mdomoni," anasema Nariman al-Najmeh. Katika hema lao lililo ufukweni kusini mwa Gaza, Nariman anaishi na mumewe, Mahmoud Fasih, na watoto wao wawili wadogo - Rayan, mwenye umri wa miaka minne, na Nihad, mwenye umri wa miaka miwili na nusu. Kifo cha Sila kinafanya idadi ya watoto waliofariki kutokana na baridi kali Gaza kufikia sita ndani ya kipindi cha wiki mbili kulingana na wizara ya afya ya eneo hilo. Mama yake Sila, Nariman anasema mwanawe alizaliwa katika hospitali moja katika eneo la Khan Younis akiwa na afya nzuri. "Afya yake ilikuwa nzuri, namshukuru Mungu, lakini ghafla, alianza kuathiriwa na baridi," a...

Simulizi za wanawake waliozuiliwa katika jela mbaya ya Evin ya Iran

Image
  Maelezo kuhusu taarifa Author, BBC 100 Women Nafasi, Saa 6 zilizopita Akiwa ameketi peke yake chini, ndani ya seli ndogo isiyo na madirisha, Nasim alisikia sauti za mateso kutoka kwa wafungwa wengine. Mlinzi angegonga mlango wake na kusema: "Unasikia hicho kichapo? Jiandae, wewe ndiye unafuata." Alikuwa "akichunguzwa kwa saa 10 hadi 12 kila siku" na alitishiwa mara kwa mara na adhabu ya kuuawa. Mahabusu hiyo ilikosa vifaa vya msingi, kama vile kitanda au choo, na ilikuwa na ukubwa wa mita mbili tu. Miezi minne ya kifungo cha peke yake ilikuwa ni utangulizi wa Nasim, msusi mwenye umri wa miaka 36, katika jela maarufu ya Evin. Aliishi akiwaona tu waliokuwa wakimuadhibu. Aliamini kwamba "atafariki na hakuna atakayejua." Tumekusanya simulizi kutoka vyanzo mbalimbali vya kuaminika ili kuunda picha ya maisha ya kila siku kwa Nasim na wanawake wengine, ambao sasa wanashikiliwa katika jela ya Evin. Wengi wao walikuwa miongoni mwa maelfu ya watu wali...

Wizara ya fedha ya Marekani yasema ilidukuliwa na China katika 'tukio kubwa'

Image
  Chanzo cha picha, Getty Images Mdukuzi anayefadhiliwa na serikali ya China ameingia katika mifumo ya Wizara ya fedha ya Marekani, na kuweza kuvifikia vituo vya kazi vya wafanyakazi na baadhi ya nyaraka ambazo hazijaainishwa, maafisa wa Marekani walisema Jumatatu. Udukuzi huo ulifanyika mwanzoni mwa Disemba na uliwekwa wazi katika barua iliyoandikwa na wizara ya fedha kwa wabunge kuwaarifu kuhusu ya tukio hilo. Wizara hiyo iliutaja udukuzi huo kama "tukio kubwa", na lkuongeza kuwa limekuwa likifanya kazi na FBI na mashirika mengine kuchunguza athari za udukuzi huo. Msemaji wa ubalozi wa China mjini Washington DC aliiambia BBC News kwamba shutuma hizo ni sehemu ya "mashambulizi yaliyolenga kuharibu sifa" na yalifanywa "bila msingi wowote". Pamoja na FBI, idara hiyo imekuwa ikifanya kazi na Wakala wa Usalama wa mtandao na miundombinu na wachunguzi wa mahakama wa ili kubaini athari ya jumla ya udukuzi huo.

Mahakama yatoa hati ya kukamatwa kwa rais wa Korea Kusini aliyeondolewa madarakani Yoon

Image
  Chanzo cha picha, Reuters Mahakama ya Seoul imetoa hati ya kukamatwa kwa rais aliyesimamishwa kazi wa Korea Kusini Yoon Suk Yeol kutokana na jaribio lake la kuweka sheria ya kijeshi tarehe 3 Disemba. Hatua hiyo inajiri baada ya Yoon, ambaye anakabiliwa na uchunguzi kadhaa wa mashtaka ya uasi na uhaini, kupuuza hati tatu za kuitwa kuhojiwa kwa muda wa wiki mbili zilizopita. Siku ya Jumapili usiku, wachunguzi waliomba kutolewa kwa hati ya kukamatwa kwa Yoon kwa tuhuma za uasi na matumizi mabaya ya mamlaka - hatua ambayo wakili wake aliitaja kuwa "haramu". Korea Kusini imekuwa katika mzozo wa kisiasa tangu kutangazwa kwa sheria ya kijeshi kwa muda mfupi, na Yoon na mrithi wake wote wameshtakiwa na bunge.

Hospitali katika Gaza ni "uwanja wa vita," na watu waliohamishwa wanajiuliza: Tunaenda wapi?

Image
  Chanzo cha picha, Reuters Maelezo ya picha, Wapalestina waliondoka katika Hospitali ya Kamal Adwan kaskazini mwa Gaza baada ya vikosi vya Israeli kuvamia hospitali hiyo Mkuu wa shirika la afya Ulimwenguni (WHO), ametoa wito wa kukomeshwa kwa "mashambulizi katika hospitali" huko Gaza. Bwana Tedros Adhanom alisema kuwa hospitali za Gaza kwa mara nyingine tena zimekuwa "uwanja wa vita" na kwamba mfumo wa afya uko chini ya "tishio kubwa." Madai ya Adhanom yanakuja baada ya kushambuliwa na kuhamishwa kwa Hospitali ya Kamal Adwan na jeshi la Israel Ijumaa iliyopita, ambacho ni kituo kikubwa cha mwisho cha afya kinachofanya kazi kaskazini mwa Ukanda wa Gaza, licha ya mashambulizi katika hospitali mbili katika mji wa Gaza siku ya Jumapili. Jeshi la Israel linasema kuwa maeneo mawili kati ya haya yanatumiwa na Hamas kama "vituo vya kutoa amri," jambo ambalo vuguvugu hilo limekanusha mara kwa mara. Mkurugenzi wa Shirika la Afya Ulimwenguni ...