Iran imeweza vipi kuwa na nafasi ya juu katika nyanja za afya ya wanawake wajawazito?
Moja ya masuala muhimu ambayo yameonekana katika miongo miwili iliyopita ni nafasi ya juu ya mfumo wa afya wa Iran kati ya nchi za kanda ya Asia Magharibi na dunia kwa ujumla. Ikilinganishwa na nchi nyingine katika kanda ya Asia Magharibi na kwingineko, mfumo wa afya wa Iran umepewa nafasi ya juu na bora, na nafasi hii nzuri imeweka msingi kwa Iran kuwa miongoni mwa nchi muhimu zaidi za utalii wa afya katika kanda hiyo. Kuhusiana na suala hilo, Iran imepata maendeleo makubwa katika nyanja za afya ya mama wajawazito katika miaka ya hivi karibuni. Kupungua kwa kiasi kikubwa vifo vya akinamama wajawazito ni miongoni mwa mafanikio muhimu ya nchi, na kwa mtazamo huo, Iran ni miongoni mwa nchi chache ambazo zimeweza kufikia malengo ya maendeleo na ustawi katika kupunguza vifo vya akinamama wajawazito. Iran ni miongoni mwa nchi chache zilizofanikwa kwa kiwango kikubw...