Mtu mwenye umri mkubwa zaidi duniani Tomiko Itooka afariki akiwa na umri wa miaka 116
Chanzo cha picha, Getty Images Mwanamke wa Kijapani, anayetambuliwa kama mtu mzee zaidi duniani na Guinness World Records, amefariki akiwa na umri wa miaka 116. Tomiko Itooka alifariki katika makazi ya wazee katika jiji la Ashiya, Mkoa wa Hyogo, kulingana na maafisa. Alikua mtu mzee zaidi ulimwenguni baada ya Maria Branyas Morera wa Uhispania kufariki mnamo Agosti 2024 akiwa na umri wa miaka 117. "Bi Itooka alitupa ujasiri na matumaini kupitia maisha yake marefu," meya wa Ashiya mwenye umri wa miaka 27 Ryosuke Takashima alisema katika taarifa. "Tunamshukuru kwa hilo." Bi Itooka alizaliwa Mei 1908 - miaka sita kabla ya Vita vya Kwanza vya Dunia na mwaka huo huo gari la Ford Model T lilizinduliwa nchini Marekani. Alithibitishwa kuwa mtu mzee zaidi duniani mnamo Septemba 2024 na akakabidhiwa cheti rasmi cha GWR katika sikukuu ya kuheshimu wazee, ambayo ni sikukuu ya umma ya Japani inayoadhimishwa kila mwaka ili kuwaenzi wazee wa nchi hiyo. Bi Itooka, ...