Posts

Urusi yapinga msaada mpya wa Marekani kwa Ukraine

Image
  Sheria iliopo tangu Urusi ilipovamia Ukraine kwa kiwango kikubwa ni kwamba kile ambacho ni kizuri kwa Kyiv ni kibaya kwa Moscow. Jumamosi iliyopita ilileta habari njema kwa serikali ya Ukraine. Bunge la Wawakilishi la Marekani lilipiga kura kuunga mkono kifurushi cha msaada cha $61bn (£49bn) kwa Kyiv, ambacho kitatumika kulipatia jeshi lake silaha. Bunge pia liliidhinisha muswada ambao utaruhusu kukamatwa na kuhamishiwa Ukraine mali ya Urusi iliyohifadhiwa Marekani. Miswada hiyo sasa inapelekwa kwa Seneti ili kuidhinishwa. Haishangazi, ni kwanini hatua hii haikupokelewa vyema mjini Moscow.Rais wa zamani Dmitry Medvedev alilaani "dola bilioni 61 za umwagaji damu". Alitoa wito wa kuwepo kwa Vita vipya vya Wenyewe kwa Wenyewe kwa Waamerika ambavyo "hatimaye vitasababisha kuvunjika vibaya kwa himaya ya uovu ya Karne ya 21, Marekani". Katika kipindi chake kikuu cha televisheni cha serikali Jumapili usiku, mtangazaji Vladimir Solovyov alielezea wazo la kuhamis...

Mkuu wa Ujasusi wa jeshi la Isrel ajiuzulu

Image
    Mkuu wa kijasusi wa jeshi la Israel amejiuzulu, akisema alichukua jukumu la kushindwa kabla ya shambulio la Hamas dhidi ya Israel tarehe 7 Oktoba. Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) lilisema Meja Jenerali Aharon Haliva atastaafu pindi mrithi wake atakapochaguliwa. Katika barua, alikiri kwamba kurugenzi yake ya ujasusi "haikutimiza kazi tuliyokabidhiwa". Yeye ndiye mtu wa kwanza mkuu kujiuzulu kutokana na shambulio hilo ambalo lilikuwa baya zaidi katika historia ya Israel. Wanajeshi na maafisa wa ujasusi wa Israel walikosa au kupuuza maonyo mengi kabla ya mamia ya watu wenye silaha wa Hamas kuvunja uzio wa mpaka wa Gaza siku hiyo na kushambulia jamii za karibu za Israel, kambi za kijeshi na tamasha la muziki. Takriban Waisrael 1,200 na raia wa kigeni - waliuawa na wengine 253 walirejeshwa Gaza kama mateka, kulingana na hesabu za Israel. Israel ilijibu kwa kuanzisha vita vyake vikali zaidi kuwahi kutokea Gaza kwa malengo ya kuangamiza Hamas na kuwakomboa mateka. Zaidi ya Wapal...

Israel na Hamas: Nini kimetokea kwa Hamas baada ya miezi sita ya vita Gaza?

Image
  Chanzo cha picha, Reuters Maelezo ya picha, Kabla ya tarehe 7 Oktoba Hamas ilikadiriwa kuwa na wapiganaji wapatao 30,000. Saa 1 iliyopit Miezi sita imepita tangu shambulio la Hamas dhidi ya Israel kufanyika kwa mara ya kwanza tarehe 7 Oktoba,2023, ambapo watu 1,200 waliuawa na zaidi ya 200 kuchukuliwa mateka. Katika kukabiliana na shambulio hili, Israel iliahidi "kuliangamiza na kulimaliza kundi la Hamas" ili lisiwe tishio tena, na kuanzisha operesheni kubwa ya kijeshi huko Gaza ambayo imesababisha vifo vya watu zaidi ya 33,000, kwa mujibu wa Wizara ya Afya ya kundi hili. Israel inasema imewaua maelfu ya wapiganaji wa Hamas na kuharibu sehemu kubwa ya mahandaki ambayo wanamgambo wa Kipalestina waliyajenga chini ya Gaza na kutumika kutekeleza mashambulizi yao. Lakini je, Israel imefanikisha lengo lake la kuliangamiza kundi hilo la wanamgambo? Na Wapalestina sasa wanafikiria nini kuhusu viongozi wao na viongozi wa Hamas huko Gaza baada ya vita vya umwagaji damu ...

Rais wa Iran anaitembelea Pakistan siku ya Jumatatu

Image
  Rais wa Iran, Ebrahim Raisi. March 20, 2024. (Iranian Presidency Office via AP) Tangazo kutoka wizara ya mambo ya nje ya Islamabad lilisema ziara hii itatoa fursa muhimu kuimarisha uhusiano wa nchi mbili Rais wa Iran Ebrahim Raisi atawasili katika nchi jirani ya Pakistan Jumatatu kwa ajili ya mikutano rasmi na viongozi wa taifa hilo huku kukiwa na mivutano kati ya Iran na Israel. Tangazo kutoka wizara ya mambo ya nje ya Islamabad leo Jumapili lilisema kuwa mazungumzo hayo yatatoa fursa muhimu ya kuimarisha uhusiano wa nchi mbili na ushirikiano katika biashara, mawasiliano, nishati, na kilimo. Tangazo lilisema ujumbe wa ngazi ya juu wa Raisi utawajumuisha waziri wa mambo ya nje wa Iran, mawaziri wengine na wawakilishi wa biashara. Wakati wa ziara yake ya siku tatu nchini Pakistan, rais wa Iran anatarajiwa kukutana na mwenzake, Asif Ali Zardari, na Waziri Mkuu Shehbaz Sharif, miongoni mwa wengine. Taarifa ya Pakistan imesema bila kufafanu...

Rais wa Ukraine asema nchi yake ina nafasi ya ushindi dhidi ya Russia kwa msaada mpya wa silaha

Image
  dakika 38 zilizopita Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky akiwa na wanajeshi wa Ukraine mbele ya ishara ya barabara inayoashiria lango la eneo la Donetsk, katikati ya Russia. (Ofisi ya rais wa Ukraine / AFP). Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy alisema Jumapili kwamba nchi yake ina nafasi ya ushindi dhidi ya Russia na msaada mpya wa silaha kwa wanajeshi wa Kyiv ambao unakaribia kuidhinishwa na Bunge la Marekani  na kuungwa mkono na Rais Joe Biden. Baraza la Wawakilishi la Marekani likiwa dhidi ya upinzani wa upande wa mrengo wa kulia wa chama cha Republican walio wengi katika bunge hilo, walipiga kura Jumamosi kwa dola bilioni 60.8 kama msaada mpya wa kijeshi kwa Ukraine, huku Seneti ikitarajiwa kupitisha hatua hiyo wiki hii na kisha Biden kutia saini. Nadhani msaada huu utaimarisha vikosi vya jeshi, natoa maombi ambayo tunahitaji sana, ambayo maelfu ya wanajeshi wanahitaji sana Zelenskyy aliambia kipindi cha Meet the Pres...

Hoja za ufunguzi zinatarajiwa kuanza katika kesi ya New York inayomkabili Donald Trump

Image
  Aliyekuwa Rais wa Marekani, Donald Trump akiwasili katika mahakama ya jinai ya Manhattan akiwa na timu yake ya wanasheria huko New York, NY siku ya Jumatatu, Aprili 15, 2024. Jabin Botsford.REUTERS. Hoja za ufunguzi zinatarajiwa kuanza Jumatatu katika kesi ya New York inayomkabili Donald Trump, kesi ya kwanza ya jinai kuwahi kuwasilishwa dhidi ya rais wa zamani wa Marekani. Hoja za ufunguzi zinatarajiwa kuanza Jumatatu katika kesi ya New York inayomkabili Donald Trump, kesi ya kwanza ya jinai kuwahi kuwasilishwa dhidi ya rais wa zamani wa Marekani. Katika kuwasilisha kwa jopo la mahakama la watu 12 waendesha mashtaka wana uwezekano wa kudai kwamba Trump alipanga njama mwaka 2016, kabla ya kampeni yake ya White House iliyofanikiwa, kuficha malipo ya fedha kwa wanawake wawili ili kuficha madai yao ya mahusiano nae ya kimapenzi nje ya ndoa. Waendesha mashtaka wanadai kwamba Trump alikuwa akitaka kuendelea kuficha taarifa za hatari kwake ...

Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Iran ashukuru majeshi kwa utendaji mzuri katika matukio ya hivi karibuni

Image
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa: "Vikosi vya kijeshi vimeonyesa taswira nzuri ya uwezo na mamlaka yao, na pia taswira yenye kupongezwa ya taifa la Iran, sambamba na kuthibitisha kuibuka kwa uwezo wa irada wa taifa la Iran katika uga wa kimataifa. Kwa mujibu wa kituo cha habari cha Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Khamenei katika kikao na makamanda wakuu wa Majeshi ya Iran ametoa pongezi kwa mnasaba wa Siku ya Jeshi na pia kumbukumbu ya kuasisiwa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, na kusema: "Mafanikio ya hivi karibuni ya jeshi yameibua hisia ya utukufu kuhusu Iran ya Kiislamu mbele ya walimwengu na weledi wa mambo duniani." Ayatullah Khamenei amepongeza kuwepo utaratibu wa mipango sahihi katika harakati za jeshi  na kusema: "Matukio mbalimbali yana gharama na faida,...

Abdul Malik al Houthi: Saudia imeondoa aya za Qur'ani katika vitabu vya kiada ili kuwaridhisha Wazayuni

Image
  Mkuu wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen amewatuhumu viongozi wa Saudi Arabia kuwa wameondoa baadhi ya mafundisho ya Qur'ani katika progamu za kufundishia mashuleni ili kuwaridhisha Wazayuni. Abdul Malik al Houthi amesema kuwa utawala wa Saudi Arabia umeondoa aya za Qur'ani katika vitabu vya mtaala mashuleni (Syllabus) ili kuepuka kuwakasirisha Wazayuni. Amesema, aya hizo zinazochujwa na Saudia mashuleni ni zile zinazozungumzia jinai zilizotendwa na Wayahudi.   Qur'ani Tukufu  Afisa huyo wa Yemen ameongeza kuwa utawala wa Saudi Arabia hata umeondoa kikamilifu au baadhi ya sejemu za  suna za Mtume  Muhammad (s.a.w) katika programu za kielimu mashuleni na kusema kuwa hatua hiyo ya Saudia ni dhulma kwa vizazi vijavyo.  Al Houthi ameongeza kuwa Saudia imefanya hivi sambamba na mpango wake wa kuhuisha  uhusiano na utawala wa Kizayuni....

Msaada wa kijeshi wenye thamani ya dola bilioni 26 wa Marekani kwa Israel sambamba na vita vya Gaza

Image
  Baada ya mabishano na mvutano kati ya Wademokrat na Warepublican na Hitilafu za pande hizo mbili juu ya msaada wa kigeni, Baraza la Wawakilishi la Marekani limeidhinisha kifurushi cha msaada wa dola bilioni 60 kwa Ukraine na kifurushi kiingine cha dola bilioni 26 kama msaada wa kijeshi kwa Israel kwa kura 366 dhidi ya 58. Muswada huu lazima uidhinishwe na Seneti na kisha utiwe saini na rais wa Marekani ili kuwa sheria. Kulingana na Wall Street Journal, huu ndio msaada mkubwa zaidi wa kijeshi kuwahi kutolewa na Marekani kwa Israeli tangu kuanza mashambulizi ya utawala huo haramu dhidi ya watu wa Ukanda wa gaza huko Palestina mnamo Oktoba 7 mwaka jana. Tangu baada ya Vita vya Pili vya Dunia, Israel imenufaika zaidi na msaada wa kijeshi wa Marekani kuliko nchi nyingine yoyote, na imekuwa ikiungwa mkono na vyama vya Republican na Democratic kwa muda mrefu. Tangu baada ya kuanza mash...

Kamanda Mwandamizi: Israel imeshindwa na Muqawama Ghaza, viongozi watamatishe vita

Image
  Yitzhak Barik, Jenerali mstaafu wa jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel amekiri kuwa jeshi la utawala huo haramu limeshindwa na Muqawama wa Palestina katika vita vya Ukanda wa Ghaza na kutaka viongozi wa utawala huo watangaze utamatishaji wa vita hivyo. Kwa mujibu wa ripoti ya shirika la habari la Palestina SAMA, Jenerali Barik amebainisha kuwa, malengo ya utawala haramu wa Israel yaliyopelekea kuanzisha mashambulio dhidi ya Ghaza bado hayajafikiwa na akasema, Israel inapaswa kutangaza uhitimishaji wa vita huko Ghaza.   Barik ameongeza kuwa, kuivamia kijeshi Rafah, mji wa kusini mwa Ukanda wa Ghaza, hakutausaidia vyovyote utawala huo, kwa sababu Israel imeshindwa katika vita na Muqawama.   Jenerali huyo mstaafu wa jeshi la utawala wa Israel unaofanya mauaji ya kimbari ametamka bayana kuwa, hakuna nguvu inayoweza kuuangamiza moja kwa moja Muqawama i...

Hizbullah yatungua ndege ya kivita isiyo na rubani ya Israel ya Hermes 450 kusini mwa Lebanon

Image
  Harakati ya Mapamabano ya Kiislamu (Muqawama) ya Hizbullah ya Lebanon imesema wapiganaji wake wameiangusha ndege ya kisasa isiyo na rubani ya kivita na kijasusi ya utawala haramu wa Israel kusini mwa Lebanon baada ya kukiuka anga ya nchi hiyo. Katika taarifa Jumapili, Hizbullah imesema imetungua ndege hiyo ya kivita ya Israel aina ya Hermes 450 katika eneo la al-Aishiya kusini mwa Lebanon. Hizbullah imeongeza katika taarifa yake kwamba ndege hiyo isiyo na rubani ya Israel iliangushwa wakati "ilipokuwa ikiwashambulia wananchi waheshimiwa na wenye kusimama kidete." Saa chache baadaye, jeshi la utawala haramu wa Israel lilikiri katika taarifa yake kwamba moja ya ndege zake zisizo na rubani ilitunguliwa kwa kombora la nchi kavu hadi angani wakati ikiwa katika operesheni kwenye anga ya Lebanon. Ndege isiyo na rubani ya Hermes 450, ambayo imetengenezwa na kampuni ya Elbit ya Israel, hutumika kwa ajili ya ujasusi na inaweza pia kubeba hadi makombora ma...

HAMAS: Msaada mpya wa Marekani kwa Israel ni kwa ajili ya kuendeleza mauaji ya umati

Image
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS imeilaani Marekani kwa kupasisha msaada mwingine kwa utawala wa Kizayuni na kusema kuwa msaada huo ni kwa ajili ya kuendeleza mauaji ya kimbari yanayofanywa na Israel dhidi ya Wapalestina. Shirika la habari la IRNA limenukuu taarifa ya HAMAS iliyotolewa jana Jumapili ikilaani vikali msaada mpya wa Washington kwa utawala wa Kizayuni na kusisitiza kuwa, hatua ya Bunge la Marekani ya kupasisha msaada huo inazidi kuonesha jinsi dola hilo la kibeberu linavyoshiriki moja kwa moja kwenye mauaji ya umati yanayofanywa na utawala wa kifashisti wa Israel dhidi ya Wapalestina wasio na hatia. Harakati ya HAMAS imeongeza kuwa, serikali ya Joe Biden huko Marekani inahusika moja kwa moja kisiasa, kisheria na kimaadili katika jinai za kivita za utawala wa Kizayuni. Wanawake na watoto wadogo wa Palestina, wahanga wakuu wa jinai za Marekani na Israel ...

Mufti Mkuu wa Russia: Kiongozi Muadhamu wa Iran anastahiki kupongezwa

Image
Mkuu wa Idara ya Masuala ya Kidini ya Waislamu ya Russia amesema kuwa, mwito unaotolewa na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei wa kuwataka watu wote duniani kuthamini masuala ya kidini na kimaadili unastahiki kupongezwa. Kwa mujibu wa shirika la habari la IRNA, Mufti Mkuu wa Russia, Sheikh Rawil Äžaynetdin (راویل عین‌الدین) ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Masuala ya Waislamu nchini humo amesema kuwa, juhudi zote za Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya nchini Iran zimeelekezwa kwenye kuleta umoja na mshikamano katika umma wa Kiislamu na kwa wanadamu wengine duniani na huko ni katika kutekeleza kivitendo amri za Mwenyezi Mungu.  Sheikh Äžaynetdin (عین‌الدین) pia amesema, msimamo wake huo unawakilisha Waislamu milioni 25 wa Russia na Baraza la Ulama la nchi hiyo kumpongeza Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya nchini Iran akimmkhu...

Wapiganaji wa Kiislamu Iraq walenga kambi ya jeshi la Israel kuunga mkono Wapalestina

Image
  Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Iraq imetangaza kulenga ngome "muhimu" ya utawala haramu wa Israel katika Milima ya Golan ya Syria inayokaliwa kwa mabavu na utawala huo ghasibu. Harakati hiyo inayoyaleta pamoja makundi yote ya Kiislamu yanayopambana na ugaidi Iraq imetoa taarifa ikisema imelenga ngome hiyo ya Israel kwa kutumia ndege za kivita zisizo na rubani. Harakati hiyo imesemaa operesheni hiyo  ni "katika kuendeleza vita dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel na kuunga mkono watu wetu huko Gaza wanaokabiliwa na mauaji ya kimbari yanayotekelezwa na Israel. Hivi karibuni pia Harakati ya Kiislamu ya Iraq ilitangaza kuwa imeshambulia maeneo muhimu katika mji wa Eilat, ulioko kusini mwa Palestina inayokaliwa kwa mabavu. Aidha wapiganaji hao wa Muqawama wa Kiislamu wa Iraq wamelenga Kambi ya Anga ya 'Ovda' ya Wazayuni katika maeneo yanayokaliwa kwa mabavu kwa kut...

Namibia yakosoa kura ya turufu ya Marekani kupinga uanachama wa Palestina katika Umoja wa Mataifa

Image
Namibia imeelezea kusikitishwa kwake kufuatia uamuzi wa hivi majuzi wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UNSC) kutopitisha azimio la kuipa Palestina uanachama kamili katika Umoja wa Mataifa. Katika taarifa, Peya Mushelenga, Waziri wa Mambo ya Nje wa Nambibia, ameelezea kusikitishwa kwake na kura ya turufu iliyotumiwa na Marekani, ambayo ilizuia kupitishwa azimio la kupendekeza uanachama kamili wa Palestina katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Marekani siku ya Alhamisi ilipiga kura kupinga ombi la Wapalestina la kutaka uanachama kamili wa Umoja wa Mataifa katika kikao cha Baraza la Usalama. Baraza hilo lenye wanachama 15 lilipigia kura rasimu ya azimio lililopendekeza kwa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lenye wanachama 193 kwamba "Nchi ya Palestina ikubaliwe uanachama wa Umoja wa Mataifa." Rasimu ya azimio hilo ilipata kura 12 za ndio, nchi mbili hazikushiriki na Marekani ilipi...

Mauzo ya bidhaa za Urusi barani Afrika ni zaidi ya mauzo Amerika

Image
  Bara la Afrika limeongeza kwa kiasi kikubwa uagizaji wa bidhaa kutoka Russia, na kuwashinda washirika wa kibiashara wa Moscow kutoka Amerika ya Kaskazini na Kusini. Hayo ni kwa mujibu wa data za kiuchumi zilizochapishwa na gazeti la kila siku la biashara la RBK nchini Russia. Gazeti hilo limenukulu ripoti ya Huduma ya Forodha ya Shirikisho la Russia (FCS) ikionyesha kuwa mwaka uliopita wa 2023, mchango wa bidhaa za Kiafrika katika mauzo ya nje ya Russia uliongezeka kwa asilimia 100. Wakati huo huo, mchango wa  eneo kubwa la  bara Amerika, ambayo ni pamoja na Karibiani, Amerika ya Kati, Amerika Kusini na Amerika Kaskazini, umeripotiwa kupungua kwa asilimia 2.9 mwaka huo.  Mauzo ya nje ya Russia  kwa mataifa ya Afrika yaliongezeka na kufikia dola bilioni 21.2, wakati mauzo kwa nchi za Amerika Kaskazini na Kusini yalipungua kwa asilimia 40 na kufika billioni 12.2. Ga...

Mwanamke mjamzito, watoto 10 ni miongoni mwa Wapalestina waliouawa hivi karibuni na Israel

Image
  Jeshi katili la Israel limefanya mashambulizi mapya ya anga dhidi ya Rafah, na kuwauwa takriban watu 16, akiwemo mama mjamzito, katika mji huo wenye msongamano mkubwa wa watu kusini mwa Gaza. Vyombo vya habari vya Palestina vimeripoti leo Jumapili kwamba baba, binti na mama mjamzito walipoteza maisha baada ya jeshi vamizi la Israel kulenga nyumba ya familia yao katika kambi ya al-Shaboura katikati mwa Rafah. Mwanamke huyo mjamzito, aliyefikishwa katika hospitali ya Kuwait, alikuwa tayari amekufa, lakini madaktari waliweza kumuokoa mtoto wake ambaye alikuwa tumboni. Rafah ni eneo lililoko katika mpaka wa kusini wa Ukanda wa Gaza uliofungwa na Misri, na hivi sasa eneo hilo ni makao ya Wapalestina wapatao milioni 1.5 ambao wamelazimika kuyahama makazi yao kutokana na vita vya mauaji ya halaiki vinavyoungwa mkono na Marekani katika eneo hilo. Israel ilikuwa imedai kuwa Rafah ni "eneo ...

Shambulizi la Israel Iran: Uharibifu waonekana katika kambi ya anga ya Isfahan

Image
      Picha za satelaiti zilizotolewa kkatika kipindi cha saa 24 zilizopita zimefichua ushahidi wa uharibifu ambao huenda ulifanyika katika kambi ya wanahewa ya Iran kufuatia shambulio la Israel mapema asubuhi ya Ijumaa. BBC Verify imechambua picha mbili zinazoonyesha sehemu ya mfumo wa ulinzi wa anga katika uwanja wa ndege huko Isfahan uliharibiwa. Maafisa wa Marekani wanasema Israel ilifanya shambulizi la kombora ingawa Israel haijathibitisha rasmi. Mvutano kati ya wapinzani hao mkali ulizidi katika wiki za hivi karibuni. Shambulio la awali linaloshukiwa kuwa la Israel dhidi ya ubalozi mdogo wa Iran nchini Syria mwanzoni mwa mwezi lilifuatiwa na shambulio la kulipiza kisasi lililofanywa na Iran dhidi ya Israel tarehe 13 Aprili. Tangu habari za shambulio la Ijumaa la Israel huko Isfahan - kituo cha mpango wa nyuklia wa Iran - kumekuwa na uvumi kuhusu uwezekano wa kutokea kwa uharibifu. Iran imesema shambulio hilo lilihusisha ndege zisizo na rubani ambazo hazikutekelez...

Marekani kuisaidia Ukraine kupunguza kasi ya mashambulizi ya Urusi

Image
  Rais Volodymyr Zelensky ameshukuru Baraza la Wawakilishi la Marekani kwa kuidhinisha msaada mpya wa kijeshi wa dola bilioni 61 kwa Ukraine baada ya mpango huo kucheleshwa kwa miezi kadhaa. Alisema msaada huo unaweza kuokoa maelfu ya maisha. Ingawa si jambo la kawaida kwa mustakabali wa nchi kuamuliwa na wanasiasa, uwepo wa taifa unaotegemea kura umbali wa maili 5,000 ni wa ajabu kama inavyosikika. Kwa Ukraine, muda wa miezi sita wa kusubiri msaada huo wa kijeshi umekuwa wa gharama kubwa na wa umekuwa wa kukatisha tamaa Risasi zinazopungua zimegharimu maisha na eneo. Katika kipindi hiki cha kuongezeka kwa nadra kwa Kyiv, hii ilikuwa shida kubwa - kuwasili kwa silaha za Amerika kutaruhusu askari wake waliopigwa marufuku kufanya zaidi ya kushikilia. Lakini sio risasi ya fedha.

Maafisa wa jeshi la majini la Japan hawajulikani walipo baada ya ajali ya helikopt

Image
  Afisa mmoja wa jeshi la majini la Japan amefariki na wengine saba hawajulikani walipo baada ya helikopta mbili kuanguka wakati wa mazoezi ya usiku katika Bahari ya Pasifiki. Mitsubishi SH-60K za injini mbili zilikuwa kwenye mafunzo ya kupambana na manowari karibu na Visiwa vya Izu, kilomita 600 kusini mwa Tokyo, maafisa walisema. Rekoda mbili za safari za ndege zilipatakana karibu na kila mmoja kama uchafu ikiwa ni pamoja na sehemu za blade za rotor. Waziri wa Ulinzi Minoru Kihara alisema chanzo cha ajali hiyo hakijajulikana. "Kwanza tunafanya tuwezavyo kuokoa maisha," Bw Kihara alisema akiongeza kuwa helikopta hizo "zinafanya mazoezi ya kukabiliana na nyambizi usiku". Mwanachama wa wafanyakazi alichukuliwa kutoka kwa maji lakini ilithibitishwa kuwa amekufa. Mawasiliano na helikopta moja yalipotea saa 22:38 saa za Japan nje ya kisiwa cha Torishima, mtangazaji wa NHK anaripoti