Posts

Showing posts with the label UCHAMBUZI

Sunak atangaza uchaguzi mkuu wa Uingereza utafanyika tarehe 4 Julai

Image
  Waziri mkuu wa Uingereza Rishi Sunak ameapa "kupigania kila kura" alipokuwa akiitisha uchaguzi mkuu wa mapema wa Uingereza Alhamisi tarehe 4 Julai. Waziri Mkuu alitoa tangazo hilo katika hotuba yake, wakati akijipigia debe kushinda muhula wa tano kwa wahafidhina. Hatua hiyo ambayo haikutarajiwa ilibadilisha matarajio ya kura, ambayo inaweza kuwa imewapa wabunge wa chama chaConservative fursa nzuri ya kuziba pengo na chama cha Labour. Sir Keir Starmer alisema ni "wakati wa mabadiliko" kuondokana na "Machafuko ya chama tawala". Chama cha Labour kimekuwa kikionyesha kuongoza katika kura za maoni za kitaifa, na kimesisitiza kuwa ina kampeni iliyoandaliwa kikamilifu na tayari kuanza. Bunge sasa litasitishwa siku ya Ijumaa, kabla ya kufungwa rasmi Alhamisi wiki ijayo kwa kampeni rasmi ya uchaguzi ya wiki tano. Ina maana kuna siku mbili tu za kupitisha sheria yoyote ambayo imesalia - hatua ambayo itamaanisha kuwa baadhi ya hatua zilizokusudiwa za serikali zital

China yaanza mazoezi ya 'adhabu' kando yaTaiwan

Image
  China imeanza mazoezi ya kijeshi kuzunguka Taiwan siku tatu tu baada ya William Lai kuapishwa kama rais mpya wa kisiwa hicho kinachojitawala. Li Xi, msemaji wa Jeshi la Ukombozi la Watu wa China, ametaja mazoezi hayo kuwa "adhabu kali" kwa "vitendo vya kujitenga". Mazoezi hayo, yaliyoanza mapema Alhamisi, yanafanyika kuzunguka kisiwa kikuu, ikiwa ni pamoja na Mlango-Bahari wa Taiwan kuelekea magharibi yake, na kuzunguka visiwa vinavyodhibitiwa na Taipei vya Kinmen, Matsu, Wuqiu na Dongyin. Wizara ya ulinzi ya Taiwan ililaani vitendo vya Beijing, na kuvitaja kuwa "uchochezi ". Taipei imetuma vikosi vya majini, anga, na ardhini "kutetea mamlaka ya [kisiwa]", wizara iliongeza. Jeshi la China limesema mazoezi yake yanalenga doria za pamoja za utayari wa kupambana na anga, mashambulizi ya usahihi katika malengo muhimu, na operesheni jumuishi ndani na nje ya kisiwa hicho ili kupima "uwezo wa pamoja wa kupambana" wa vikosi vyake.

Ireland, Norway, na Uhispania kulitambua taifa la Palestina

Image
  Mataifa matatu ya UlayaMataifa ya Ulaya, Ireland, Norway, na Uhispaniayametangaza hivi punde kulitambua taifa la Palestina Waziri Mkuu wa Uhispania Pedro Sanchez ametangaza hivi punde kwamba nchi yake italitambua jimbo la Palestina tarehe 28 Mei. Akiwa mjini Madrid, Waziri Mkuu wa Uhispania Pedro Sanchez alipigiwa makofi bungeni alipotangaza uamuzi wa taifa hilo wa Azama ya kuiunga mkono Palestina kama taifa: "Tunaenda kuitambua Palestina kwa sababu nyingi na tunaweza kuhitimisha hilo kwa maneno matatu - amani, haki na uthabiti," anasema. "Tunapaswa kuhakikisha kuwa suluhisho la serikali mbili linaheshimiwa na lazima kuwe na dhamana ya usalama ya pande zote. "Ni muhimu kwa pande hizo mbili kujadiliana kwa ajili ya amani na ni kwa sababu hii kwamba tunaitambua Palestina." Huko Dublin, waziri mkuu wa Ireland anasema suluhisho la serikali mbili ndio "njia pekee inayoaminika" kwa amani. Simon Harris anaongeza: "Tuna miongo mitatu baada ya mchakato

Ni nchi ngapi zimetambua taifa la Palestina?

Image
  Takriban nchi 140 zimelitambua taifa la Palestina, kulingana na barua ya hivi majuzi kwa Umoja wa Mataifa. nchi hizo zinajumuisha wanachama wa Kundi la nchi 22 za Kiarabu katika Umoja wa Mataifa, Jumuiya ya Nchi 57 za Ushirikiano wa Kiislamu na Harakati Zisizofungamana na Siasa zenye wanachama 120. Uingereza na Marekani ni miongoni mwa mataifa ambayo hayaitambui rasmi taifa la Palestina. Mapema mwezi huu waziri wa mambo ya nje Bwana Cameron alipendekeza kuwa serikali, pamoja na washirika wake, inaweza "kuangalia suala la kulitambua taifa la Palestina, ikiwa ni pamoja na Umoja wa Mataifa". Israel haitambui utaifa wa Palestina na serikali ya sasa ya Israel inapinga kuundwa kwa taifa la Palestina katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na Gaza. Inasema kuwa hali kama hiyo itakuwa tishio kwa uwepo wa Israeli.

Moshi wa jenereta wawaua wanafunzi Nigeria - ripoti

Image
Takriban wanafunzi saba wa chuo kikuu wamefariki baada ya kuvuta moshi kutoka kwa jenereta katika studio ya muziki katika jimbo la Bayelsa lenye utajiri wa mafuta nchini Nigeria. Vijana hao wanasemekana kufanya kazi hadi Jumatatu usiku na kulala kwenye studio iliyofungwa huku jenereta ikiendelea kufanya kazi. Wanashukiwa kupungukiwa na hewa ya kaboni lakini polisi wanasema uchunguzi unaendelea. Biashara na kaya nyingi nchini Nigeria zinategemea jenereta zinazotumia dizeli au petroli kwa sababu ya ugavi wa umeme usiotosheleza. Miili sita ilipatikanaJumanne asubuhi, huku mmoja wao, aliyepatikana akiwa amepoteza fahamu, akikimbizwa katika hospitali ya karibu lakini akafariki baadaye, vyombo vya habari vya ndani viliripoti. Wakazi wa eneo hilo walipiga kelele walipochungulia kupitia dirisha la studio na kuona miili hiyo ikiwa imetapakaa sakafuni. Polisi walifika na kuzingira eneo hilo baada ya kuhamisha miili katika eneo la Amarata la Yenagoa - mji mkuu wa jimbo la Bayelsa.

Nchi zaidi zatangaza maombolezo ya kitaifa kufuatia kufa shahidi Rais Raisi wa Iran

Image
  May 22, 2024 02:22 UTC Kufuatia kufa shahidi Rais wa Iran Ebrahim Raisi katika ajali ya helikopta katika eneo la kaskazini-magharibi mwa nchi, nchi nyingi duniani zimetangaza maombolezo ya kitaifa, huku viongozi wa kimataifa wakiendelea kutoa salamu za rambirambi kwa serikali na taifa la Iran. Msitu wa Dizmar katika Mkoa wa Azarbaijan Mashariki ulikuwa eneo la ajali mbaya ya helikopta siku ya Jumapili, na kusababisha vifo vya Rais Raisi na ujumbe alioandamana nao. Mbali na Rais, ndani ya helikopta hiyo walikuwemo Waziri wa Mambo ya Nje Hossein Amir-Abdollahian, Gavana wa Azarbaijan Mashariki Malek Rahmati, Imamu wa Swala ya Ijumaa ya Tabriz Seyyed Mohammad Ali Al-e Hashem na mwanachama wa timu ya walinzi wa rais Mahdi Mousavi. Rubani wa helikopta, rubani mwenza na wahudumu wa ndege pia walikuwa miongoni mwa wengine waliokuwa kwenye helikopta hiyo. Huku kukiwa na hali mbaya ya

Kijana muuaji aliyenunua mapanga 79 mtandaoni atajwa jina lake

Image
  Jaji wa Mahakama ya Juu ameamua kuwa umma unafaa kuambiwa jina la kijana mfanyabiashara wa dawa za kulevya ambaye alinunua visu 79 na mapanga katika miezi kadhaa kabla ya kumdunga mtu na kumuua. Bi Justice Foster ameondoa amri ambayo iliwazuia wanahabari kufichua utambulisho wa Rayis Nibeel mwenye umri wa miaka 17, ambaye amepatikana na hatia ya kumuua Omar Khan mwenye umri wa miaka 38 huko Luton. Amri ilikuwa imetolewa chini ya sheria iliyolenga kuwalinda watoto na vijana wanaohusika katika kesi mahakamani. Lakini jaji ameondoa amri hiyo baada ya BBC kuhoji kuwa kufichua jina la Nibeel ni kwa manufaa ya umma. Mapema mwaka huu majaji walikuwa wamempata Nibeel na kijana mwingine, Umer Choudhury mwenye umri wa miaka 18, na hatia ya kumuua Bw Khan, ambaye alishambuliwa kwa kisu cha cha inchi 15 (sentimita 37.5). Walikuwa wamesikia jinsi Bw Khan, wa Leicester Road, Luton, alivyofariki katika eneo la shambulio katika eneo la Sundon Park eneo la Luton mnamo Septemba 16, 2023, baada ya kuzu

Waziri Mkuu Uingereza aahidi kulipa fidia waathiriwa wa sakata ya damu yenye maambukizi

Image
  Waziri mkuu wa Uingereza Rishi Sunak ameahidi kulipa "fidia" kwa watu walioathiriwa na kashfa ya damu yenye maambukizi. Waziri mkuu alisema serikali italipa "chochote itakachogharimu" kufuatia ripoti juu ya kashfa hiyo, ambayo watu 30,000 wameambukizwa. Uchunguzi wa umma uligundua kuwa mamlaka iliwaweka waathirika katika hatari isiyokubalika na kuficha maafa makubwa ya matibabu katika Huduma ya Afya ya Taifa. Serikali itaweka maelezo ya fidia siku ya Jumanne. Serikali itaweka maelezo ya fidia siku ya Jumanne. Mawaziri wameripotiwa kutenga karibu £10bn kwa kifurushi cha fidia. Uchunguzi wa damu Iliyoambukizwa ilishutumu madaktari, serikali na Huduma ya Afya ya Taifa kwa kuruhusu wagonjwa kuambukizwa virusi vya ukimwi na homa ya ini walipokuwa wakipokea huduma ya Huduma ya Afya ya Taifa kati ya miaka ya 1970 na 1990. Takriban 3,000 wamefariki na vifo zaidi vitaendelea kutokea kutokana na Sakata hiyo.

Korea Kusini yapiga marufuku wimbo wa 'kumtukuza' Kim Jong Un

Image
  Korea Kusini imesema itapiga marufuku wimbo wa propaganda wa Korea Kaskazini unaomsifu dikteta wa Pyongyang Kim Jong Un kama "baba rafiki" na "kiongozi mkuu". Mdhibiti wa vyombo vya habari wa Seoul alisema video hiyo ya muziki, ambayo imekuwa maarufu kwenye TikTok tangu ilipotolewa Aprili, ni ukiukaji wa Sheria ya Usalama wa Kitaifa ya nchi hiyo. "[Wimbo huo] unamsifu na kumtukuza Kim Jong Un," Tume ya Mawasiliano ya kuangazia Ubora ya Seoul ilisema katika taarifa siku ya Jumatatu. Sheria ya Usalama inazuia ufikiaji wa tovuti na vyombo vya habari vya serikali ya Korea Kaskazini, na inaadhibu tabia na hotuba zinazopendelea utawala huo. Toleo la 29 ​​la video ya wimbo wa Baba Rafiki itazuiwa, tume ilisema, lakini haikufafanua jinsi hilo lingetekelezwa. Uamuzi huo ulichochewa na ombi kutoka Huduma ya Kitaifa ya Ujasusi ya Korea Kusini, iliongeza. "Video hiyo ni maudhui ya kawaida yanayohusishwa na vita vya kisaikolojia dhidi ya Korea Kusini, na ilichap

Mwanaume apigwa risasi hadi kufa baada ya sinagogi la Ufaransa kuchomwa moto

Image
  Polisi wa Ufaransa wamemuua mwanamume mmoja baada ya sunagogi kuchomwa moto katika mji wa kaskazini-magharibi wa Rouen. Mwanamume huyo ambaye alikuwa amejihami kwa kisu na kifaa cha chuma alipigwa risasi baada ya kuwatishia maafisa, mwendesha mashtaka wa Rouen amesema. Meya wa Rouen, Nicolas Mayer-Rossignol amesema shambulio dhidi ya sinagogi halikuathiri tu jamii ya Wayahudi, bali jiji zima "limepigwa na mshtuko". Ripoti za Ufaransa zinasema mshukiwa huyo alikuwa raia wa Algeria na alikuwa akikata rufaa dhidi ya amri ya kuondoka Ufaransa. Polisi waliitwa mwendo wa saa moja kasoro robo (04:45 GMT) baada ya moshi kuonekana ukitoka katika sinagogi. Mshambuliaji huyo alipanda juu ya pipa kubwa la taka na kurusha bomu la petroli kupitia dirisha dogo, na kulichomo moto sinagogi. Maafisa wawili wa polisi walifika eneo la tukio kwa kasi, baada ya mtu huyo kuonekana kwenye kamera za ulinzi. Mshukiwa alikuwa juu ya paa la sinagogi walipofika, kulingana na waendesha mashta

Wachezaji wanaolipwa fedha nyingi zaidi duniani 2024

Image
  Cristiano Ronaldo ameongoza orodha ya Forbes ya wanariadha wanaolipwa fedha nyingi zaidi duniani kwa mara ya nne katika maisha yake ya soka, huku Jon Rahm mcheza gofu akipanda hadi nafasi ya pili. Ronaldo pia aliongoza orodha hiyo mwaka jana baada ya kuhamia klabu ya soka ya Saudi Arabia ya Al Nassr. Jarida la biashara la Forbes linasema, mshambuliaji huyo wa Ureno mwenye umri wa miaka 39 alipata kiasi cha $260m (£205m) - kutoka $136m (£108.7m) - katika kipindi cha miezi 12 iliyopita. Mpinzani mkubwa wa Ronaldo Lionel Messi ameporomoka hadi nafasi ya tatu nyuma ya Rahm. Mchezaji gofu wa Uhispania amepanda hadi nafasi pili nyuma kabla ya kufanyika kwa safari yake ya kwenda kucheza Gofu ya LIV inayofadhiliwa na Saudia na anaripotiwa kupata $218m (£172m). Mcheza gofu huyo wa Uhispania ni mmoja wa wanariadha 22 walio na umri wa chini ya miaka 30 kwenye orodha hiyo, jambo ambalo linaweza kuashiria mabadiliko. Wachezaji waliodumu katika hiyo orodha kama vile Serena Williams,

Mawaziri 13 wa Mambo ya Nje wakiwemo 6 wa G7 waitaka Israel isitishe uvamizi wa ardhini wa Rafah

Image
Shirika la habari la DPA la Ujerumani limeripoti kuwa mawaziri wa mambo ya nje kutoka nchi 13 wametia saini barua ya kuuonya na kuutaka utawala wa Kizayuni wa Israel usitishe uvamizi wake wa ardhini katika eneo la Rafah kusini mwa Ukanda wa Ghaza na kuruhusu misaada zaidi kuwafikia Wapalestina. Ikinukuu ripoti katika gazeti la Suddeutsche Zeitung la Ujerumani, DPA imeripoti kuwa, ukiondoa Marekani, wanachama wengine wote wa Kundi la Mataifa Saba yaliyoendelea kiviwanda (G7) wametia saini barua hiyo ya kurasa nne ambayo iliandikwa siku ya Jumatano. Katika barua iliyotumwa kwa waziri wa mambo ya nje wa utawala wa Kizayuni wa Israel Israel Katz, mawaziri hao wameitaka serikali ya Benjamin Netanyahu ipunguze hali ya uharibifu na inayozidi kuwa mbaya ya kibinaadamu huko Ghaza kwa kufungua vivuko vyote vya mpakani kwa ajili ya kuingizwa misaada, ikiwa ni pamoja na kivuko cha Rafah na Misri, ambacho

Serikali ya Tanzania yatakiwa kubuni sheria maalumu ya ukatili dhidi ya wanawake

Image
  Serikali ya Tanzania imetakiwa kubuni sheria maalumu ya kukabiliana na ukatili dhidi ya wanawake. Watetezi wa haki za binadamu nchini Tanzania wameitaka serikali ya nchi hiyo kubuni sheria maalumu kwa ajili ya kupambana na ukatili dhidi ya wanawake na wasichana kutokana na kuwepo kwa ongezeko la kubwa la ukatili katika kipindi cha hivi karibuni hali inayoendelea kutia wasiwasi. Watetezi wa haki za binadamu nchini Tanzania wanasema kuwa,  sheria iliyopo bado ina mapungufu yanayoendelea kutoa nafasi ya wanawake kuendelea kufanyiwa ukatili. Ukatili dhidi ya wanawake na wasichana ni miongoni mwa changamoto ambayo inaendelea kushuhudiwa sehemu mbali mbali nchini Tanzania, ukatili huo ukihusisha wa kimwili, kijinsia, kisaikolojia, na hata unyanyasaji wa wanandoa ambapo unaonekana kuongezeka.   Kwa mujibu wa ripoti ya Mkurugenzi wa Uchunguzi wa Jinai (DCI) ni kuwa, katika kipindi

Mwanaume mmoja aambiwa yeye si Muingereza baada ya miaka 42 kuishi Uingereza

Image
  Mwanaume mmoja - mfanyakazi mstaafu kutoka Ghana mwenye umri wa miaka 74 ambaye ameishi Uingereza kwa karibu miaka 50 - Nelson Shardey, kutoka Wallasey huko Wirral, kwa miaka mingi alikuwa akidhani amekuwa raia rasmi wa Uingereza. Aligundua kumbe sivyo mwaka 2019, licha ya kulipa ushuru maisha yake yote ya utu uzima, na sasa anakabiliwa na malipo ya maelfu ya pauni ili kukaa na kutumia huduma za afya za NHS. Ofisi ya Mambo ya Ndani ilikataa kutoa maoni kuhusu kesi hiyo ya kisheria inayoendelea. 'Sijawahi kuulizwa' Wakala wa magazeti aliyestaafu Shardey alikwenda Uingereza kwa mara ya kwanza mwaka 1977 kusomea uhasibu, kwa viza ya mwanafunzi ambayo pia ilimruhusu kufanya kazi. Baada ya mapinduzi katika nchi yake ya asili ya Ghana familia yake haikuweza tena kumtumia pesa za ada. Ndipo akaamua kufanya kazi, na anasema hakuna mtu aliyewahi kuhoji haki yake ya kuishi au kufanya kazi nchini Uingereza. Alioa mwanamke wa Uingereza na kuhamia Wallasey ili kuendesha bi

MIFUMO YA VIWANJA VYA NDEGE UINGEREZA YADUKULIWA

Image
 Viwanja vya ndege vya Uingereza vimelemazwa na kukatika kwa mfumo wa nchi nzima (VIDEOS) Hitilafu katika mifumo ya kuingia kiotomatiki ilisababisha fujo za usafiri kote nchini Viwanja vya ndege kote Uingereza vilikumbwa na ucheleweshaji Jumanne jioni baada ya "suala la kiufundi" la nchi nzima kusababisha hitilafu ya mifumo ya kielektroniki ya Jeshi la Mipaka la Uingereza kwa zaidi ya saa nne. Video zinazoshirikiwa mtandaoni zinaonyesha mistari mirefu huku huduma zikipungua hadi kutambaa. Baadhi ya wateja walilalamika kuwa laini hizo zimekuwa zikisumbua vifaa hivyo inadaiwa kuwafanya baadhi ya wateja kukosa maji ya kutosha na vyoo. Klipu zingine zinaonyesha skrini tupu kwenye eGates. Viwanja vya ndege vya Heathrow, Gatwick, Birmingham, Bristol, Manchester, Newcastle, na Edinburgh vilithibitisha matatizo na mfumo wa Kikosi cha Mipaka, ambayo yalisababisha ucheleweshaji wa muda mrefu kwa wasafiri siku ya Jumanne, shirika la utangazaji la serikali ya Uingereza BBC iliandika. Su

Maafisa wa jeshi la majini la Japan hawajulikani walipo baada ya ajali ya helikopt

Image
  Afisa mmoja wa jeshi la majini la Japan amefariki na wengine saba hawajulikani walipo baada ya helikopta mbili kuanguka wakati wa mazoezi ya usiku katika Bahari ya Pasifiki. Mitsubishi SH-60K za injini mbili zilikuwa kwenye mafunzo ya kupambana na manowari karibu na Visiwa vya Izu, kilomita 600 kusini mwa Tokyo, maafisa walisema. Rekoda mbili za safari za ndege zilipatakana karibu na kila mmoja kama uchafu ikiwa ni pamoja na sehemu za blade za rotor. Waziri wa Ulinzi Minoru Kihara alisema chanzo cha ajali hiyo hakijajulikana. "Kwanza tunafanya tuwezavyo kuokoa maisha," Bw Kihara alisema akiongeza kuwa helikopta hizo "zinafanya mazoezi ya kukabiliana na nyambizi usiku". Mwanachama wa wafanyakazi alichukuliwa kutoka kwa maji lakini ilithibitishwa kuwa amekufa. Mawasiliano na helikopta moja yalipotea saa 22:38 saa za Japan nje ya kisiwa cha Torishima, mtangazaji wa NHK anaripoti

Watu 1,300 wa Myanmar wamekimbilia Thailand

Image
  Takriban watu 1,300 wamekimbia kutoka mashariki mwa Myanmar kuelekea Thailand, maafisa wamesema Jumamosi, wakati mapigano mapya yakizuka katika mji wa mpakani ambao hivi karibuni ulitekwa na wapiganaji wa msituni wa kikabila. Wapiganaji kutoka kabila la walio wachache la Karen wiki iliyopita waliiteka ngome ya mwisho ya jeshi la Myanmar ndani na kuzunguka Myawaddy, ambayo imeungana na Thailand kwa madaraja mawili katika Mto Moei. Mapigano ya karibuni kabisa yalizuka asubuhi wakati wapiganaji wa msituni wa Karen walipoanzisha mashambulizi dhidi ya wanajeshi wa Myanmar waliokuwa wamejificha karibu na daraja la pili la urafiki la Thailand na Myanmar, kivuko kikuu cha biashara na Thailand, alisema mkuu wa polisi Pittayakorn Phetcharat katika wilaya ya Mae Sot nchini Thailand. Alikadiria kuwa akriban watu 1,300 walikimbilia Thailand.

Tunachofahamu kuhusu shambulio la Israel dhidi ya Iran

Image
  Maafisa wa Marekani wanasema Israel iliipiga Iran kwa kombora usiku wa kuamkia leo, katika kile kinachoonekana kuwa ni shambulio la kulipiza kisasi baada ya majuma kadhaa ya mvutano unaoongezeka kati ya nchi hizo mbili. Kuna madai yanayoshindana kuhusu ukubwa wa shambulio katika eneo la Isfahan na kiwango cha uharibifu, huku vyombo vya habari vya Iran vikipuuza umuhimu wake. Inakuja baada ya wiki kadhaa za mvutano unaoongezeka kati ya wapinzani wa kikanda, ambao tayari wameshuhudia shambulio la Israeli kwenye ubalozi wa Iran huko Syria, na Iran kuanzisha shambulio ambalo halijawahi kushuhudiwa dhidi ya Israeli. Hapa kuna kila kitu tunachojua kuhusu tukio la hivi punde hadi sasa. Tunajuaje kuwa kumekuwa na shambulio? Israel haikiri mara kwa mara hatua zake za kijeshi, ambazo zimelenga makundi yenye silaha yanayoungwa mkono na Iran nchini Syria na Iraq mara nyingi. Hata hivyo, maafisa wa Marekani wameithibitishia mshirika wa BBC, CBS News kwamba kombora la Israel liliipig

Je,shambulio la Israel dhidi ya Iran linaonyesha nchi hizo hazifahamu uwezo wa kila mmoja kijeshi?

Image
  Mashambulizi ya Israel dhidi ya Iran hayakuwa jibu kali ambalo Rais wa Marekani Joe Biden na viongozi wengine wa mataifa ya magharibi walihofia. Wamekuwa wakiitaka Israel kukomesha hatua za kuzuia msururu wa matukio hatari yaliyoanza na Israel kumuua jenerali mkuu wa Iran mjini Damascus tarehe 1 Aprili. Zaidi ya miezi sita baada ya mashambulizi ya Hamas dhidi ya Israel, vita vinaendelea huko Gaza na vimeenea katika eneo hilo kila upande wa mpaka wa Lebanon na Israel na Ghuba. Hofu ni kwamba Mashariki ya Kati iko ukingoni mwa vita vya nje, na hatari za kimataifa na za kikanda. Wairani wanadharau umuhimu wa kile kilichotokea huko Isfahan. Ripoti za awali zilisema hakukuwa na shambulio lolote. Baadaye, mchambuzi katika runinga ya serikali alisema ulinzi wa anga ulikuwa umeondoa ndege zisizo na rubani ambazo zilikuwa zimerushwa na "wapenyezaji". Vyombo rasmi vya habari vimechapisha picha za utani za ndege ndogo zisizo na rubani. Israel ilikuwa ikijibu mashambulizi J

Mkuu wa Majeshi na makamanda tisa waandamizi wa Kenya wafariki katika ajali ya helikopta

Image
  Kenya inaomboleza kifo cha Mkuu wa Majeshi (KDF), Jenerali Francis Omondi Ogolla ambaye ameaga dunia katika ajali ya helikopta iliyotokea jana Alkhamisi katika eneo la Sindar kwenye mpaka wa Kaunti ya Pokot Magharibi na Elgeyo Marakwet. Jenerali Ogolla alifariki dunia pamoja na maafisa wengine tisa waandamizi wa jeshi la Kenya waliokuwemo ndani ya helikopta ya KDF iliyokuwa na maafisa wengine 11 wa jeshi hilo wakati ajali hiyo ilipotokea dakika chache baada ya saa tisa alasiri. Rais William Ruto ametangaza siku tatu za kumuombeleza Jenerali Ogolla na maafisa wengine waliofariki wakiwa kazini. Rais Ruto aliambia taifa akiandamana na makamanda wakuu wa KDF na waziri wa Ulinzi Aden Duale katika Ikulu ya Nairobi: "ni siku ya huzuni. Leo nchi yetu imekumbwa na ajali mbaya iliyomuua Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Kenya, Jenerali Francis Omondi Ogolla”. Maafisa hao walikuwa wakitoka katika ziar