Posts

Showing posts with the label UCHAMBUZI

Saa 3 zilizopitaUchaguzi Afrika Kusini 2024: Matokeo ya kwanza yatangazwa

Image
  Matokeo ya kwanza yametangazwa ya uchaguzi unaoonekana kuwa wenye ushindani zaidi nchini Afrika Kusini tangu chama cha African National Congress (ANC) kiingie madarakani miaka 30 iliyopita. Huku matokeo kutoka kwa zaidi ya asilimia 11 ya wilaya za wapiga kura yamehesabiwa kufikia sasa, ANC inaongoza kwa 43%, ikifuatiwa na DA yenye 26%. Chama chenye msimamo mkali cha EFF na Umkhonto weSizwe (MK Party) cha Rais wa zamani Jacob Zuma vina karibu 8%. Matokeo ya mwisho yanatarajiwa mwishoni mwa juma. Kura za maoni zinaonesha kuwa chama cha ANC kinaweza kupoteza wingi wake bungeni kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 30. Chama cha ANC kimepoteza uungwaji mkono kutokana na hasira juu ya viwango vya juu vya rushwa, uhalifu na ukosefu wa ajira. Lakini ni mapema sana kutabiri matokeo ya mwisho. Uchaguzi wa Alhamisi ulishuhudia misururu mirefu ya wapiga kura nje ya vituo vya kupigia kura hadi usiku wa manane kote nchini.

Naibu waziri wa fedha wa Marekani amewasili Ukrain

Image
  Adeyemo alisema Marekani inapanga kuchukua hatua zaidi ili kuweka shinikizo kwa uchumi wa Russia. Naibu Waziri wa Fedha wa Marekani Wally Adeyemo amewasili Kyiv siku ya Jumatano kukutana na maafisa wa Ukraine kwa mazungumzo kuhusu kuimarisha vikwazo dhidi ya Russia pamoja na msaada wa kifedha kwa Ukraine. Alisema Marekani inapanga kuchukua hatua zaidi ili kuweka shinikizo kwa uchumi wa Russia. Uchumi wa Russia umekuwa uchumi wa wakati wa vita, ambapo kila njia ya uzalishaji na viwanda sasa imejikita katika kujenga silaha za kupambana na vita vyao ilivyovichagua na uvamizi hapa Ukraine, Adeyemo alisema Jumatano katika mji mkuu wa Ukraine. “Tunahitaji kufanya kila tuwezalo ili tufanikiwe baada ya hapo”. Adeyemo amesema kipaumbele cha Hazina ni kupunguza mapato ya Russia na kuizuia Russia kupata bidhaa inazozihitaji ili kuzisaidia ngome zake za viwanda vya ulinzi, ikijumuisha bidhaa za matumizi ya nchi mbili kutoka China.

Dhahabu ya Afrika yenye thamani ya mabilioni ya dola husafirishwa kimagendo kila mwaka-ripoti

Image
  Dhahabu ya Afrika yenye thamani ya mabilioni ya dola inauzwa kwa njia ya magendo nje ya bara hilo kila mwaka, nyingi ikipelekwa Dubai kabla ya kusafirishwa kwa njia halali kwenda nchi nyingine, shirika lisilo la serikali kutoka Uswisi limesema Alhamisi. Shirika lisilo la serikali la maendeleo la Uswisi Swissaid lilichapisha ripoti likisema kwamba kati ya tani 321 na 474 za dhahabu kutoka Afrika inayozalishwa kupitia uchimbaji kwa kutumia mikono kwenye migodi midogo inasafirishwa kimagendo kila mwaka, na thamani yake ni kati ya dola bilioni 24 na bilioni 35. Afrika ni mzalishaji mkubwa wa dhahabu duniani, huku Ghana, Afrika Kusini, Mali na Burkina Faso zikiongoza kwa uzalishaji huo mwaka 2022. Kulingana na shirika hilo la Uswisi, usafirishaji wa dhahabu ya Afrika kwa njia ya magendo umeongezeka, uliongezeka maradufu kati ya 2012 na 2022.” Shirika hilo linasema madini hayo ya thamani ni “chanzo cha mapato kwa mamilioni ya wachimbaji wadogo, ni chanzo kikuu cha mapato

Israel inasema inadhibiti eneo la mpaka wa Gaza na Misri

Image
  Jeshi la Israel linasema kuwa limechukua udhibiti wa eneo la kimkakati kwenye mpaka kati ya Gaza na Misri, linalojulikana kama Philadelphi Msemaji wa Kikosi cha Ulinzi cha Israel (IDF) alisema kuwa takribani njia za chini kwa chini 20 zinazotumiwa na Hamas kuingiza silaha Gaza zimepatikana huko. Televisheni ya Misri ilinukuu vyanzo vinavyokanusha hilo, na kusema Israel ilikuwa inajaribu kuhalalisha operesheni yake ya kijeshi katika mji wa kusini wa Gaza wa Rafah. Tangazo hilo linakuja wakati wa mvutano mkali na Misri. "Katika siku za hivi karibuni, wanajeshi wa IDF walianzisha udhibiti wa operesheni kwenye Ukanda wa Philadelphi, kwenye mpaka kati ya Misri na Rafah," msemaji wa IDF Rear Admiral Daniel Hagari alisema Jumatano. Alielezea ukanda huo kama "uhai" kwa Hamas, ambapo kundi hilo "liliingiza silaha mara kwa mara katika Ukanda wa Gaza". Bw.Hagari baadaye alisema katika kikao na wanahabari kwamba hangeweza kuwa na uhakika kwamba njia zote zilivuka ha

Uchaguzi Afrika Kusini 2024: Shughuli ya kuhesabu kura inaendelea

Image
  Kura zinahesabiwa baada ya uchaguzi wa hapo jana nchini Afrika Kusini. Mistari mirefu ilikuwa nje ya vituo vya kupigia kura kote nchini. Afisa mmoja wa uchaguzi mjini Johannesburg aliiambia BBC kuwa misururu hiyo inakumbusha uchaguzi wa kihistoria wa 1994, wakati watu weusi walipiga kura kwa mara ya kwanza, na ambao ulishuhudia Nelson Mandela kuwa rais. Watu wengi walikuwa bado wanangoja kupiga kura wakati kura zilipofungwa rasmi saa 2100 saa za ndani (1900 GMT) lakini tume ya uchaguzi ilisema kwamba wote wataruhusiwa kupiga kura zao. Matokeo ya kwanza yataanza kutangazwa Alhamisi asubuhi na matokeo ya mwisho yanatarajiwa mwishoni mwa juma. Chama cha ANC kimepoteza uungwaji mkono kutokana na hasira juu ya viwango vya juu vya rushwa, uhalifu na ukosefu wa ajira. Kura za maoni zinaonesha kuwa huenda ikapoteza wingi wake bungeni. Sifiso Buthelezi, ambaye alipiga kura katika Joubert Park mjini Johannesburg, kituo kikubwa zaidi cha kupigia kura nchini Afrika Kusini, aliiambia BBC

Yote unayopaswa kujua kuhusu uchaguzi wa Afrika Kusini 2024

Image
  Chanzo cha picha, AFP 27 Machi 2024 Imeboreshwa Dakika 56 zilizopita Raia wa Afrika Kusini wanashiriki uchaguzi mkuu leo Mei 29, huku baadhi ya kura zikipendekeza chama tawala cha African National Congress (ANC) kinaweza kupata chini ya asilimia 50 ya kura kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 30. Ukosoaji unaoongezeka dhidi ya chama kilichoongoza vita dhidi ya ubaguzi wa rangi chini ya hayati Nelson Mandela umepunguza uungwaji mkono wake, na kuongeza uwezekano wa serikali ya mseto. Uchaguzi wa Afrika Kusini utafanyika lini? Tarehe 29 Mei, karibu wapiga kura milioni 28 wa Afrika Kusini waliojiandikisha wana nafasi ya kuchagua wawakilishi katika mabunge ya kitaifa na majimbo. Utakuwa uchaguzi mkuu wa saba wa kidemokrasia nchini humo. Umekuwa ukifanyika kila baada ya miaka mitano tangu 1994, wakati utawala wa weupe wachache ulipoisha na ANC kuingia madarakani. Ni nini kiko hatarini kwa ANC na sera zake ni zipi? Chama cha ANC ambacho sasa kinaongozwa na Rais Cyril Ramaph

Shambulio Rafah: Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kukutana kwa dharura

Image
 Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linatarajia kukutana kwa dharura leo Jumanne mchana kujadili hali ya Rafah. Mkutano huo, ambao haujafungwa, uliombwa na Algeria, mwanachama asiye wa kudumu wa Baraza, vyanzo kadhaa vya kidiplomasia vimeliambia shirika la habari la AFP.  Dakika 2 Moja ya vikao vya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, New York. ©REUTERS/Shannon Stapleton

Uhispania, Norway na Ireland kuitambua rasmi taifa huru la Palestina

Image
 Nchi tatau za Ulaya Uhispania, Norway na Ireland zitalitambua Taifa la Palestina leo Jumanne katika mkutano na waandishi wa habari mjini Brussels, tangazo lililotolewa wiki iliyopita na ambalo liliamsha hasira kwa Israel. Dakika 1 Maandamano ya kuunga mkono Palestina katika Chuo Kikuu cha Columbia huko New York, Aprili 22, 2024. REUTERS - Eduardo Munoz

Harakati za kumkutanisha rais wa Rwanda na mwenzake wa DRC zinaendelea

Image
 Mchakato wa Nairobi wa kusaka amani mashariki mwa DRC umeendelea kuingia dosari kutokana na matukio kadhaa wakati ule wa Luanda ukifufuliwa kuhakikisha viongozi wa Rwanda na DRC wanakutana.  Kinshasa inachukulia kuwa mchakato wa Nairobi ulishindwa kufikia ufanisi wake na sasa umesimama ambapo matukio ya hivi karibuni kati ya Kenya mwenyeji wa mazungumzo na DRC ndio imekuwa sababu. Viongozi wa DRC walilaani hatuwa ya Corneille NangaA kutangaza uasi akiwa katika mji mkuu wa Kenya Nairobi, jambo ambalo lilisababisha Kinshasa kumrejesha nyumbani balozi wake jijini Nairobi. Corneille Nangaa, anatuhumiwa na Kinshasa kwa kutangaza uasi akiwa jijini Nairobi. AFP - LUIS TATO Kuanzia hapo juhudi za kurejesha hali katika usawa ziliendelea kufanyika. Lakini kauli ya hivi karibuni ya rais wa Kenya William Ruto kwenye vyombo vya

Wanakijiji 160 waliripotiwa kuvamiwa na kutekwa nyara Nigeria

Image
Chanzo cha picha, BOKO HARAM Watu kumi wameuawa na takribani wanakijiji wengine 160 wametekwa nyara kutoka jamii ya mbali katika jimbo la kati la Niger nchini Nigeria, maafisa wanasema. Idadi kubwa ya watu wenye silaha, wanaoshukiwa kuwa kutoka kundi la wanamgambo wa Kiislamu wa Nigeria Boko Haram, walivamia kijiji cha Kuchi Ijumaa usiku, afisa wa eneo hilo Aminu Abdulhamid Najume aliiambia BBC. Waliotekwa nyara wengi wao walikuwa wanawake na watoto, wakati waliouawa ni pamoja na wawindaji wa eneo hilo ambao walikuwa wakitoa ulinzi katika eneo hilo, alisema. Inasemekana watu hao wenye silaha walipanda pikipiki hadi Kuchi na hata kutumia muda kupika chakula, kuandaa chai na kupora kabla ya kuondoka zaidi ya saa mbili baadaye. Bw.Najume, ambaye ni mwenyekiti wa Baraza la Maeneo ya Serikali ya Maeneo ya Munya, alisema jamii ya Wakurchi imeachwa na kiwewe na kuhangaika kusikia habari za waliochukuliwa. Ikiandika kwenye mitandao ya kijamii, Amnesty International ilionesha &q

Nini kinatokea kwa silaha zilizotumwa Ukraine? Marekani hawajui kabisa

Image
Wanajeshi wa Kiukreni wakipakia lori na makombora ya kuzuia tanki ya Mkuki. - Marekani ina njia chache za kufuatilia usambazaji mkubwa wa vifaru, ndege na silaha nyingine ambazo imetuma kuvuka mpaka hadi Ukraine, vyanzo vya habari vinaiambia CNN, sehemu isiyoeleweka ambayo kwa kiasi kikubwa imesababishwa na ukosefu wa buti za Marekani kwenye ardhini nchini - na kubebeka kwa urahisi kwa mifumo mingi midogo inayoingia mpakani. Ni hatari inayojulikana ambayo utawala wa Biden uko tayari kuchukua. Kwa muda mfupi, Marekani inaona uhamisho wa vifaa vya thamani ya mamia ya mamilioni ya dola kuwa muhimu kwa uwezo wa Waukraine wa kuzuia uvamizi wa Moscow. Afisa mkuu wa ulinzi alisema Jumanne kwamba "hakika ni usambazaji mkubwa zaidi wa hivi karibuni kwa nchi mshirika katika mzozo." Lakini hatari, maafisa wa sasa wa Marekani na wachambuzi wa masuala ya ulinzi wanasema, ni kwamba katika muda mrefu, baadhi ya silaha hizo huenda zikaishia mikononi mwa wanamgambo wengine na wanamgambo ambao

Ripota Maalumu wa UN ataka Israel iwekewe vikwazo

Image
  Ripota Maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu ametoa mwito wa kuwekewa vikwazo utawala wa Kizayuni wa Israel. Francesca Albanese ametoa mwito huo leo Jumamosi, kufuatia uamuzi wa Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) wa kuuamuru utawala wa Israel usitishe mara moja mashambulizi yake ya kijeshi huko Rafah, kusini mwa Ukanda wa Gaza. Albanese ameeleza bayana kuwa, utawala wa Israel hauwezi kuachana na 'uwendawazimu na uchakaramu huu' iwapo jamii ya kimataifa haitauzuia. Amesema kuna udharura wa kuiwekea Israel vikwazo vya silaha na kusimamisha uhusiano wa kidiplomasia na Tel Aviv mpaka pale itakaposimamisha hujuma zake dhidi ya Rafah. Amesisitiza kuwa, Israel inafanya mauaji ya kimbari huko Gaza, sambamba na kuwafukuza Wapalestina wa eneo hilo kwenye makazi yao. Afisa huyo mwandamizi wa UN amekuwa akikabiliwa na masham

Ulimwengu unapuuza hatari ya mauaji ya kimbari Sudan - mtaalam wa UN

Image
  Jimbo la Darfur nchini Sudan linakabiliwa na hatari kubwa ya mauaji ya halaiki huku ulimwengu ukitilia mkazo mizozo ya Ukraine na Gaza, ameonya mtaalamu wa Umoja wa Mataifa. "Tuna mazingira ambayo mauaji ya halaiki yanaweza kutokea au yametokea," Mshauri Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Kuzuia Mauaji ya Kimbari, Alice Wairimu Nderitu, amekiambia kipindi cha Newsday cha BBC. Amesema raia wengi walilengwa kulingana na kabila lao katika mji unaozingirwa nchini Sudan wa El Fasher, ambapo mapigano makali yameongezeka katika siku za hivi karibuni. Zaidi ya vifo 700 vimeripotiwa katika siku 10 na shirika la matibabu katika jiji hilo. El Fasher ni kituo kikuu cha mwisho cha mijini katika eneo la Darfur ambacho kimesalia mikononi mwa jeshi la Sudan. Wanajeshi wamekuwa wakipigana na Jeshi la Wanajeshi la Rapid Support Forces (RSF) kwa zaidi ya mwaka mmoja, katika vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyosababisha vifo vya maelfu ya watu na kuwalazimisha mamil

'Kusitisha vita dhidi ya Hamas ni kujiua hadharani' - msemaji wa Israel aiambia BBC

Image
  Msemaji wa serikali ya Israel David Mencer amekuwa akizungumza na BBC: "Hakuna mamlaka duniani ambayo itatusukuma kujitoa uhai hadharani, ili kusitisha vita vyetu dhidi ya Hamas." Mawaziri wa baraza la mawaziri la Israel wanakutana baadaye kujadili uamuzi wa mahakama ya ICJ lakini maafisa wa serikali wamesema hapo awali kwamba hakuna mamlaka yoyote duniani ambayo inaweza kuizuia Israel kuwalinda raia wake na kkukabiliana na kundi la Hamas huko Gaza. Mamlaka ya Palestina (PA) - ambayo inaendesha sehemu za Ukingo wa Magharibi unaokaliwa - na Hamas - ambayo inaendesha Gaza na kushambulia jamii za karibu za Israeli tarehe 7 Oktoba, na kusababisha vita vya sasa - wamekaribisha uamuzi huo. Hata hivyo Hamas inasema wito wa kusitisha mashambulizi unapaswa kuhusisha Gaza yote na sio Rafah pekee. Uamuzi huo "unawakilisha makubaliano ya kimataifa kumaliza vita kwenye Ukanda wa Gaza," msemaji wa rais wa PA Nabil Abu Rudeina ameliambia shirika la habari la Reuter

China yaandaa mashambulizi ya makombora ya kuiga ya dhidi ya Taiwan

Image
  China imefanya mashambulio ya makombora ya kuiga na kutuma ndege za kivita zilizobeba makombora ya moja kwa moja na vilipuzi siku ya Ijumaa, televisheni ya taifa CCTV ilisema, kama sehemu ya mazoezi ya siku mbili ambayo Beijing imesema yalizinduliwa kumuadhibu rais mpya wa Taiwan, Lai Ching-te. Washambuliaji hao waliunda safu kadhaa za mashambulizi katika maji mashariki mwa Taiwan, wakifanya mashambulizi ya mfano kwa ushirikiano na meli za jeshi la majini, iliongeza, wakati China ikijaribu uwezo wake wa "kunyakua mamlaka" na kudhibiti maeneo muhimu ya Taiwan. Mazoezi ya siku mbili katika Mlango wa bahari wa Taiwan na kuzunguka vikundi vya visiwa vinavyodhibitiwa na Taiwan karibu na pwani ya China, ambayo afisa wa Taiwan alisema pia ni pamoja na kuiga ulipuaji wa meli za kigeni, ilianza siku tatu tu baada ya Lai kuchukua madaraka Jumatatu. Taiwan imelaani vitendo vya China. Uchina inaiona Taiwan inayotawaliwa kidemokrasia kama eneo lake yenyewe na inashutumu Lai kama "m

Miili mingine mitatu ya mateka wa Israel yapatikana Gaza

Image
  Miili ya mateka wengine watatu wa Israel imeopolewa kutoka Gaza, Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) limesema. Ni wale wa Hanan Yablonka, Michel Nisenbaum na Orion Hernandez, ilisema katika taarifa yake. IDF ilisema miili hiyo ilipatikana katika mji wa kaskazini wa Jabalia katika operesheni ya pamoja na shirika la kijasusi la Israel iliyofanyika usiku kucha. Hii inakuja wiki moja baada ya miili mingine mitatu ya mateka kupatikana huko Gaza. Mateka waliouawa walikuwa miongoni mwa watu 252 waliotekwa nyara wakati wapiganaji wenye silaha wa Hamas waliposhambulia Israel tarehe 7 Oktoba, na kuua takriban watu 1,200. Kuna takriban mateka 130 ambao bado wanashikiliwa huko Gaza, Israel inasema.

Majeshi ya Israel yawaua makumi ya Wapalestina katika mashambulizi ya Gaza

Image
  Vikosi vya Israel viliwaua Wapalestina 60 katika mashambulizi ya anga na ardhini katika Ukanda wa Gaza siku ya Alhamisi na kupigana kwa karibu na wanamgambo wanaoongozwa na Hamas katika maeneo ya mji wa kusini wa Rafah, maafisa wa afya na vyombo vya habari vya Hamas wamesema. Vifaru vya Israel vilisonga mbele katika kusini mashariki mwa Rafah, kuelekea wilaya ya magharibi ya mji wa Yibna na kuendeleza operesheni yake katika vitongoji vitatu vya mashariki, wakaazi walisema. Reuters imezungumza na mkaazi mmoja ambaye alisema, "Majeshi ya Israel yanajaribu kusonga mbele zaidi kuelekea magharibi, yapo kwenye ukingo wa Yibna, ambako kuna watu wengi. Bado hawajaivamia," mkazi mmoja alisema, akiomba jina lake lisitajwe. "Tunasikia milipuko na tunaona moshi mweusi ukitoka katika maeneo ambayo jeshi limevamia. Ulikuwa usiku mwingine mgumu sana," aliambia Reuters kupitia programu ya mazungumzo. Israel ilianzisha mashambulizi yake huko Gaza kufuatia shambulio lililoongozwa n

Mbu waliobadilishwa vinasaba waachiliwa nchini Djibouti kupambana na malaria

Image
  Makumi ya maelfu ya mbu waliobadilishwa vinasaba (GMO) wameachiliwa nchini Djibouti katika juhudi za kukomesha kuenea kwa spishi vamizi wanaosambaza malaria. Mbu dume wasiouma aina ya Anopheles stephensi mbu waliotengenezwa na Oxitec, kampuni ya teknolojia ya kibayoteknolojia yenye makao yake makuu nchini Uingereza, hubeba jeni inayoua watoto wa kike kabla ya kukomaa. Mbu jike pekee ndio wanaouma na kusambaza malaria na magonjwa mengine ya virusi. Ni mara ya kwanza kwa mbu wa aina hiyo kutolewa Afrika Mashariki na mara ya pili barani humo. Teknolojia kama hiyo imetumika kwa mafanikio nchini Brazil, Visiwa vya Cayman, Panama, na India, kulingana na Vituo vya Marekani vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (CDC). Zaidi ya mbu kama hao bilioni moja wameachiliwa kote ulimwenguni tangu 2019, CDC inasema. Kundi la kwanza la mbu hao waliachiliwa hewani siku ya Alhamisi huko Ambouli, kitongoji cha jiji la Djibouti. Ni hatua ya majaribio katika ushirikiano kati ya Oxitec Ltd, serikali ya Djibouti n

Papa aashiria uwezekano wa 'mshawishi wa Mungu' kuwa mtakatifu

Image
  Kijana mzaliwa wa London - ambaye ustadi wake wa kueneza mafundisho ya kanisa katoliki mtandaoni ulimfanya aitwe "mshawishi wa Mungu" - anatarajiwa kuwa mtakatifu. Carlo Acutis alifariki dunia mwaka wa 2006, akiwa na umri wa miaka 15, ikimaanisha kuwa angekuwa milenia wa kwanza - mtu aliyezaliwa mapema miaka ya 1980 hadi mwishoni mwa miaka ya 1990 - kutangazwa kuwa mtakatifu. Inafuatia Papa Francis kuhusisha muujiza wa pili kwake. Ilihusisha uponyaji wa mwanafunzi wa chuo kikuu huko Florence ambaye alikuwa na damu kwenye ubongo baada ya kuumia kichwa. Carlo Acutis alikuwa ametangazwa mwenye heri - hatua ya kwanza kuelekea utakatifu - mnamo 2020, baada ya kuhusishwa na muujiza wake wa kwanza - kumponya mtoto wa Brazil kutokana na ugonjwa wa kuzaliwa ulioathiri kongosho yake. Muujiza wa pili uliidhinishwa na Papa kufuatia mkutano na idara ya watakatifu ya Vatican. Bado haijajulikana ni lini atatangazwa kuwa mtakatifu. Carlo Acutis alifariki dunia huko Monza, nchini Italia, ba

Aliyekuwa kiongozi wa kijeshi Chad aapishwa kuwa rais

Image
Rais mteule wa Chad Mahamat Idriss Deby (katikati) alipowasili katika shughuli za kuapishwa kwake Mei 23, 2024. Picha na Joris Bolomey / AFP. Jenerali Mahamat Idriss Deby Itno aliyeongoza Chad kijeshi kwa takriban miaka mitatu iliyopita ameapishwa Alhamis baada ya kushinda katika uchaguzi mkuu uliokuwa na ushindani mkali baina yake na vyama vya upinzani. Baada ya kula kiapu, Deby aliwahutubia viongozi saba kutoka mataifa ya Afrika Magharibi na wageni wa heshima pamoja na wananchi wa Chad. Alitoa wito kwa Wachad wote waliompigia kura na wapinzani wake kufanyakazi nae na kwamba ataheshimu uwamuzi wao ambao ni muhimu kiatika kuendeleaza demokrasia nchini mwao. Deby alipata asilimia 61 za kura katika uchaguzi uliofsnyika Mei 6 ambapo mashirika yasiyo ya kiserikali yalisema haukuwa wa kuaminika wala huru na ambapo mpinzani wake kuu aliuita uchaguzi huo kuwa uliokuwa na udanganyifu. Sherehe hizo za kuapishwa kwa kiongozi huyo kunafikisha kikom