Posts

Tetesi za soka Ulaya Alhamisi 31.10.2024

Image
  Tetesi za soka Ulaya Alhamisi 31.10.2024 Chanzo cha picha, Getty Images Maelezo ya picha, Wachezaji wa Man United ambao hawapo katika mpango wa Amorim Saa 3 zilizopita Ruben Amorim tayari amezungumzia mipango yake ya uhamisho na uongozi wa Manchester United na haoni winga Antony, viungo Casemiro na Christian Eriksen au beki Victor Lindelof kama sehemu ya mipango yake. (TeamTalks) Jitihada za United kupata huduma ya Amorim zimegonga mwamba baada ya Sporting kudai pauni milioni 4 kwa wafanyikazi wake pamoja na ada ya kuachiliwa kwa meneja huyo ya pauni milioni 8.3. (Times – Subscription Required) Amorim anakubali huenda akalazimika kusubiri hadi mapumziko ya kimataifa mwezi ujao ili kujiunga na United. (Telegraph – Subscription Required) Uamuzi wa West Ham kutomteua Amorim msimu uliopita ulitokana na kutokuwa na uzoefu wa kusimamia klabu kubwa, badala ya kifedha. (Daily Mail), nje Chanzo cha picha, Getty Images Maelezo ya picha, Kocha wa Sporting Amorim Barcelona wanavut...

Biden: Ikiwa wanajeshi wa Korea Kaskazini wataingia Ukraine, Ukraine inapaswa kuwashambulia

Image
  Biden: Ikiwa wanajeshi wa Korea Kaskazini wataingia Ukraine, Ukraine inapaswa kuwashambulia Chanzo cha picha, Reuters Rais wa Marekani Joe Biden ametoa maoni yake kuhusu ripoti za wanajeshi wa Korea Kaskazini kuwasili katika eneo la Kursk nchini Urusi. Alisema ana wasiwasi na ripoti hizo. Alipoulizwa ikiwa Ukraine inapaswa kujibu, Biden alijibu: "Ikiwa watavuka mpaka na kuingia Ukraine, basi ndio washambuliwe."

Marekani yasema shambulizi la anga la Israel 'ni la kutisha'

Image
  Marekani yasema shambulizi la anga la Israel 'ni la kutisha' Chanzo cha picha, Reuters Takribani watu 93 wameuawa au hawajulikani walipo baada ya mashambulizi ya anga ya Israel katika mji wa Beit Lahia kaskazini mwa Gaza, wizara ya afya inayosimamiwa na Hamas imesema, katika shambulio ambalo Marekani imelitaja kuwa la "kuogofya". Waokoaji walisema jengo la makazi la ghorofa tano lilipigwa, na video kwenye mitandao ya kijamii zilionesha miili iliyofunikwa kwa blanketi sakafuni. Jeshi la Israel lilisema "linafahamu ripoti kwamba raia walijeruhiwa leo [Jumanne] katika eneo la Beit Lahia". Imeongeza kuwa taarifa za tukio hilo zinaangaliwa. Vikosi vya Ulinzi vya Israel (IDF) vimekuwa vikifanya kazi kaskazini mwa Gaza katika muda wa wiki mbili zilizopita, hasa katika maeneo ya Jabalia, Beit Lahia na Beit Hanoun. Mkurugenzi wa hospitali ya karibu ya Kamal Adwan huko Jabalia, Hussam Abu Safia, ameliambia shirika la habari la AFP kwamba watoto walikuwa wakitibiwa...

Wanaharakati kufika mahakama za juu kupinga Tamisemi kusimamia uchaguzi

Image
  Wanaharakati kufika mahakama za juu kupinga Tamisemi kusimamia uchaguzi Wakili na wanaharakati nchini Tanzania waliokuwa wakipinga Waziri kutunga kanuni za uchaguzi wa serikali za mitaa na kuusimamia uchaguzi huo wamesema watakata rufaa kupinga uamuzi wa mahakama uliotolewa jana na kuhalalisha kanuni za uchaguzi zilizotungwa na Waziri na kuruhusu Tamisemi kuendelea kusimamia uchaguzi wa serikali za mitaa. Wakili Jebra Kambole akiwa na wanaharakati Bob Wangwe, Dr Ananilea Nkya na Bubelwa Kaiza walifungua shauri mahakamani wakihoji mamlaka ya Waziri wa Tamisemi kutunga kanuni za uchaguzi huo na pia kusimamia, kuendesha na kuratibu uchaguzi wa serikali za mitaa. Walitaka majukumu hayo yapewe Tume Huru ya Uchaguzi. “Tutakwenda mahakama ya riufaa ambayo ndiyo ya mwisho. Na yenyewe ikiwa itafanya maamuzi ya ndivyo sivyo, tutaifikia mahakama ya Afrika ya watu na binnadamu au tume ya haki za binadamu ya Afrika tunaamini huko tutapata haki kama tulivyoppata haki ya kesi ya wakurugenzi kus...

Ufaransa yaiunga mkono Morocco katika mzozo kuhusu Sahara Magharibi

Image
  Ufaransa yaiunga mkono Morocco katika mzozo kuhusu Sahara Magharibi Chanzo cha picha, AFP Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ameliambia bunge la Morocco kwamba anaamini Sahara Magharibi inapaswa kuwa chini ya mamlaka ya Morocco, na ameahidi kuwekeza fedha za Ufaransa huko. Sahara Magharibi ni eneo la pwani ya kaskazini-magharibi mwa Afrika ambalo limekuwa na mzozo wa miongo kadhaa. Wakati fulani lilikuwa koloni la Uhispania, na sasa linadhibitiwa zaidi na Morocco na kwa kiasi fulani na Polisario Front inayoungwa mkono na Algeria, ambayo inasema inawakilisha watu asilia wa Sahrawi na inataka taifa huru. Ufaransa ilikuwa nchi yenye nguvu ya kikoloni katika Morocco na Algeria. Inaungana na mataifa mengine ikiwemo Uhispania, Marekani na Israel kuunga mkono mpango wa Morocco. Wabunge walisimama na kumpongeza Macron Jumanne aliposema, "kwa Ufaransa, eneo hili la sasa na la siku zijazo liko chini ya mamlaka ya Morocco". Maoni yake siku ya Jumanne huko Rabat yanalingana ...

Mshindi wa taji la Urembo nchini Rwanda akamatwa kwa kuendesha gari akiwa amelewa

Image
  Mshindi wa taji la Urembo nchini Rwanda akamatwa kwa kuendesha gari akiwa amelewa Chanzo cha picha, Divine Muheto/Instagram Polisi nchini Rwanda wamemkamata mshindi wa taji la taifa la urembo kwa "kurudia" "kuendesha gari akiwa amekunywa pombe kupita kiasi" na kusababisha uharibifu wa miundombinu. Divine Muheto hana leseni ya kuendesha gari na alitoroka eneo la ajali baada ya kugonga miundombinu, polisi walisema katika taarifa. Bi Muheto hajajibu hadharani madai hayo. Bi Muheto, 21, alipata umaarufu aliposhinda shindano la urembo la Miss Rwanda mnamo 2022, kabla ya serikali kusitisha shindano hilo baada ya tuhuma za utovu wa maadili dhidi ya waandaaji. Polisi wametangaza kukamatwa kwake leo, siku chache baada ya tetesi kuwa mrembo huyo alihusika katika ajali ya barabarani na baadaye kukamatwa. Adhabu ya kuendesha ukiwa umekunywa ni faini ya faranga 150,000 za Rwanda (dola 110), na siku tano rumande. Katika miaka ya hivi karibuni maelfu ya watu walikama...

RSF, washirika wake, walifanya unyanyasaji wa kingono Sudan, ujumbe wa Umoja wa Mataifa unasema

Image
  RSF, washirika wake, walifanya unyanyasaji wa kingono Sudan, ujumbe wa Umoja wa Mataifa unasema Chanzo cha picha, Getty Images Vikosi vya Msaada wa Haraka vya Sudan (RSF) na washirika wake wamefanya viwango vya "kushangaza" vya unyanyasaji wa kingono, kuwabaka raia huku wanajeshi wakisonga mbele na kuwateka nyara baadhi ya wanawake kama watumwa wa ngono wakati wa vita vilivyodumu zaidi ya miezi 18, ujumbe wa Umoja wa Mataifa ulisema Jumanne, Reuters imeripoti. Waathirika wameanzia kati ya miaka minane hadi 75, ilisema ripoti ya ujumbe wa uchunguzi wa Umoja wa Mataifa, huku unyanyasaji mwingi wa kingono ukifanywa na RSF na wanamgambo washirika wa Kiarabu katika jaribio la kuwatisha na kuwaadhibu watu kwa kudhaniwa kuwa na uhusiano na maadui. "Kiwango kikubwa cha unyanyasaji wa kijinsia ambao tumeandika nchini Sudan ni cha kushangaza," mwenyekiti wa misheni Mohamed Chande Othman alisema katika taarifa iliyoambatana na ripoti ya kurasa 80 iliyojikita kati...

Waridi wa BBC: Namna ujauzito ulivyonisababishia usikivu hafifu

Image
  Waridi wa BBC: Namna ujauzito ulivyonisababishia usikivu hafifu Chanzo cha picha, Rukia Jamal ”Huyu hata ukimpigia simu hatapokea anakwambia tuma ujumbe, masikio yake mazito,” anaeleza Rukia Jamal ambaye ana changamoto ya usikivu hafifu akinukuu baadhi ya maneno ya wateja wake. Rukia, mwenye umri wa miaka 26 ni mama wa mtoto mmoja wa kike mwenye wafuasi wengi katika mitandao ya kijami amekuwa akikabiliana na unyanyasaji kutokana na ulemavu alio nao. Kwa baadhi ya watu katika jamii suala la ulemavu ni tiketi ya kujitumbukiza katika utegemezi wa misaada na wengine hata kuwa ombaomba. Rukia anaelezea kuwa wanajamii wana uelewa duni juu ya watu wenye usikifu hafifu. ”Zipo nyakati ambazo nilichapisha tangazo la biashara zangu mtandaoni baadhi ya watu waliandika kunikejeli kuwa masikio mazito kwa kuwa niliwahimiza kuandika ujumbe badala ya kuzungumza.” Anaongeza kuwa baadhi ya watu katika jamii humuona mwenye tatizo kubwa, lakini kwake hilo halijamzuia kumudu shughuli zak...

Video za mapishi ya kuchaganya 'mate' na 'mkojo 'katika chakula zaibua ghadhabu India

Image
  Video za mapishi ya kuchaganya 'mate' na 'mkojo 'katika chakula zaibua ghadhabu India Chanzo cha picha, Getty Images Maelezo ya picha, Mamilioni ya watu nchini India wanafurahia chakula cha mitaani, lakini maafisa wanasema kuna wasiwasi mkubwa juu ya ubora wa chakula Saa 1 iliyopita Na Srilan Mullen BBC News Baada ya video zinazoonyesha 'mate', 'mkojo' na uchafu vikichanganywa katika chakula na vinywaji kujitokeza, zimezifanya serikali za majimbo mawili ya India, Uttarakhand na Uttar Pradesh, kuanzisha sheria za utozaji faini kubwa na hukumu kali za jela dhidi ya wale waliopatikana na hatia miongoni watu wanaotengeneza chakula na vinywaji hivyo. Jimbo la kaskazini la Uttarakhand linapanga kuweka faini ya hadi laki moja kwa wakiukaji wa sheria hiyo huku wakati jimbo jirani ya Uttar Pradesh likifikiria kuanzisha sheria kali kukabiliana na tatizo hilo. Maagizo hayo ya serikali yamekuja baada ya video ambazo hazijathibitishwa kusambaa kweny...

Tetesi za soka Ulaya Jumatano 30.10.2024

Image
  Tetesi za soka Ulaya Jumatano 30.10.2024 Chanzo cha picha, Getty Images Maelezo ya picha, Mbeumo Saa 3 zilizopita Newcastle United wana nia ya kumsajili mshambuliaji wa Brentford na Cameroon Bryan Mbeumo, 25, mwezi Januari lakini Magpies wanakabiliwa na vikwazo vya matumizi. (Telegraph – Subscription Required} Liverpool na Arsenal pia wanamuwania Mbeumo, ambaye Brentford inasema ana thamani ya takriban £50m. (Newcastle Chronicle), Manchester United wanatarajia kumteua meneja wa Sporting Ruben Amorim kwa ajili ya mechi ya Jumapili ya Ligi Kuu dhidi ya Chelsea kwenye Uwanja wa Old Trafford. (Saa – Subscription Required) Hata hivyo, Manchester United wako kwenye mazungumzo na Sporting kuhusu muda wa notisi ya Amorim, ambao ni wiki kadhaa. (Mail) Chanzo cha picha, Getty Images Maelezo ya picha, Amorim Amorim bado ataendelea kuwa mkufunzi kwa mechi ijayo ya ligi ya Sporting siku ya Ijumaa, kabla ya kusafiri kwenda Manchester. (CNN Portugal) Meneja huyo wa Ureno, 39, anataka k...

Uchaguzi wa Marekani 2024: Je, Marekani itaendelea kuiunga mkono au kuitelekeza Ukraine baada ya uchaguzi?

Image
  Uchaguzi wa Marekani 2024: Je, Marekani itaendelea kuiunga mkono au kuitelekeza Ukraine baada ya uchaguzi? Rais ajaye wa Marekani ataamua kuhusu matarajio ya Ukraine kuingia NATO, kuendelea na usambazaji wa silaha za Magharibi na masharti ya mazungumzo ya amani kati ya Kyiv na Moscow. Wafuatiliaji wa mambo wanakubali kwamba ushindi wa Kamala Harris utapokelewa vizuri zaidi huko Kyiv kuliko muhula wa pili wa Donald Trump. Diplomasia ilikuwa sehemu ya jukumu la Harris kama makamu wa rais katika utawala wa Biden, alipewa kazi ya kufanya mazungumzo na viongozi mbalimbali. Pia unaweza kusoma Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini? 25 Februari 2022 Siri ya silaha ya siri ya urusi iliyoanguka Ukraine 12 Oktoba 2024 Uchaguzi wa Marekani 2024: Je, Trump na Harris wana sera gani? 24 Oktoba 2024 Mipango ya Harris Chanzo cha picha, Getty Images Maelezo ya picha, Mwaka 2022, Congress ilimkaribisha Zelensky kwa shangwe Mwaka 2022, Urusi ilifanya uvamizi nchini Ukraine, ...

Naim Qassim: Mfahamu kiongozi mpya wa Hezbollah

Image
  Naim Qassim: Mfahamu kiongozi mpya wa Hezbollah Chanzo cha picha, Getty Images Saa 6 zilizopita Hezbollah imetangaza uteuzi wa Amin Qassem kama katibu mkuu wa chama, kumrithi Hassan Nasrallah, mwezi mmoja baada ya mauaji yake katika uvamizi wa Israel ambao ulilenga makao makuu ya uongozi wa kundi hilo kusini mwa mji mkuu wa Lebnon, Beirut mwishoni mwa Septemba. Naim Qasim ni nani? Kwa mujibu wa kanuni za ndani za Hezbollah, naibu katibu mkuu wa chama humwakilisha katibu mkuu iwapo kutatokea dharura yoyote ya kisiasa au kiusalama. Ikitokea kifo cha katibu mkuu, naibu wake ameidhinishwa kutekeleza majukumu yake hadi mkutano wa dharura wa Shura utakapofanyika ambapo kiongozi mpya atachaguliwa kushika nafasi ya katibu mkuu wa chama. Kwa sasa Qassem anashikilia wadhifa wa Naibu Katibu Mkuu wa Hezbollah, chama cha kisiasa, kijeshi na kijamii ambacho kina msingi maarufu na ushawishi mkubwa miongoni mwa jamii ya Washia nchini Lebanon. Soma pia: Hezbollah inamchaguaje kiong...

Waziri wa Israel asema uteuzi wa kiongozi mpya wa Hezbollah ni 'wa muda'

Image
  Waziri wa Israel asema uteuzi wa kiongozi mpya wa Hezbollah ni 'wa muda' Chanzo cha picha, EPA-EFE/REX/Shutterstock Kwingineko, Waziri wa Ulinzi wa Israel Yoav Gallant, ameweka ujumbe kwenye mtandao wa X kuhusu kiongozi mpya wa Hezbollah Sheikh Naim Qassem, na kusema: "Uteuzi huo ni wa muda. Sio wa kudumu." Kauli ya Gallant inawadia baada ya wanajeshi wa Israel kuua idadi kubwa ya viongozi wa Hezbollah katika wiki chache zilizopita, akiwemo kiongozi wa muda mrefu Hassan Nasrallah, ambaye aliuawa katika shambulio kubwa la anga la Israel huko Beirut mwezi Septemba. Hezbollah ilitangaza uteuzi wa Qassem mapema leo, ikimtaja kama "aliyebeba bendera iliyobarikiwa katika maandamano haya".

Takriban watu 93 wameuawa katika shambulizi la Israel huko Gaza - Hamas

Image
  Takriban watu 93 wameuawa katika shambulizi la Israel huko Gaza - Hamas Chanzo cha picha, Reuters Takriban watu 93 wamefariki au hawajulikani walipo baada ya kutokea kwa mashambulizi ya anga ya Israel katika mji wa Beit Lahia kaskazini mwa Gaza, wizara ya afya inayoendeshwa na Hamas imesema. Waokoaji walisema jengo la makazi la ghorofa tano lilishambuliwa, na video kwenye mitandao ya kijamii zilionyesha miili iliyofunikwa kwa blanketi sakafuni. Hakujakuwa na maoni ya mara moja kuhusu shambulizi hilo kutoka kwa jeshi la Israel, ambalo lilianza mashambulizi mapya katika eneo hilo mapema mwezi huu baada ya kusema Hamas inajipanga upya huko. Vikosi vya Ulinzi vya Israel vimekuwa vikiendesha shughuli zake kaskazini mwa Gaza katika muda wa wiki mbili zilizopita, hasa katika maeneo ya Jabalia, Beit Lahia na Beit Hanoun.

Sean 'Diddy' Combs akabiliwa na kesi mpya za kuwanyanyasa wavulana kingono

Image
  Sean 'Diddy' Combs akabiliwa na kesi mpya za kuwanyanyasa wavulana kingono Chanzo cha picha, Reuters Sean 'Diddy', Rapa mwenye umri wa miaka 54 anadaiwa kumpiga mvulana mmoja ambaye alisafiri na familia yake kwa ajili ya mikutano na wakuu wa tasnia ya muziki, katika chumba cha hoteli mjini New York mwaka 2005. Sean "Diddy" Combs ameshtakiwa kwa kumpa dawa za kulevya na kumdhalilisha kingono mvulana wa miaka 10 katika kesi mpya. Rapa huyo mwenye umri wa miaka 54, anadaiwa kumvamia mvulana huyo katika chumba cha hoteli mjini New York mwaka wa 2005. Kesi ya pili mpya inamtuhumu gwiji huyo wa muziki wa hip-hop anayeshikiliwa jela kwa kumshambulia kijana mwenye umri wa miaka 17 ambaye alishiriki katika kipindi cha televisheni cha Making the Band mwaka wa 2008. Ni shutuma za hivi karibuni katika wimbi la kesi ambapo washtaki wanadai walinyanyaswa kingono na Combs kwenye karamu na mikutano katika kipindi cha miongo miwili iliyopita. Wanasheria wa Combs wal...

Lebanon inasema watu 60 wameuawa katika shambulio la Israel kwenye bonde la mashariki

Image
  Lebanon inasema watu 60 wameuawa katika shambulio la Israel kwenye bonde la mashariki Chanzo cha picha, Getty Images Takriban watu 60 wameuawa katika mashambulizi ya Israel kwenye Bonde la Bekaa Mashariki mwa Lebanon, wizara ya afya ya Lebanon imesema. Watoto wawili walikuwa miongoni mwa waliouawa katika shambulio hilo ambalo lililenga maeneo 16 katika eneo la Baalbek, maafisa walisema. Wizara hiyo ilisema watu 58 walijeruhiwa, na kuongeza kwamba juhudi za uokoaji bado zinaendelea katika bonde hilo, ambalo ni ngome ya Hezbollah. Jeshi la Israel bado halijatoa tamko lolote. Israel imefanya maelfu ya mashambulizi ya angani kote Lebanon katika muda wa wiki tano zilizopita, ikilenga kile inachosema ni maafisa wa Hezbollah, miundombinu na silaha. Gavana wa Baalbek Bachie Khodr aliyataja mashambulizi hayo kuwa ya "mabaya zaidi" katika eneo hilo tangu Israel ilipozidisha mzozo dhidi ya Hezbollah mwezi uliopita. Video ambayo haijathibitishwa iliyotumwa kwenye mitandao ya ki...

Utawala Afrika Kusini watofautiana kuhusu mkataba wa visa ya Ukraine

Image
  Utawala Afrika Kusini watofautiana kuhusu mkataba wa visa ya Ukraine Chanzo cha picha, Serikali ya Afrika Kusini Makubaliano yenye utata ya kuwawezesha wanadiplomasia wa Ukraine kuingia nchini Afrika Kusini bila visa yamezua hasira katika ulimwengu wa kisiasa nchini humo. Waziri wa Mambo ya Ndani wa Afrika Kusini Leon Schreiber, ambaye ni chama tofauti na rais, alitangaza mpango huo siku ya Jumapili, akiitaja Ukraine "mshirika wa thamani". Lakini ofisi ya rais imemkosoa Schreiber kwa kutangaza makubaliano hayo bila idhini rasmi kutoka kwa Rais Cyril Ramaphosa. Wakosoaji wanauchukulia mpango huo kama ukiukaji wa uhusiano wa muda mrefu wa Afrika Kusini na Urusi - ingawa nchi hiyo haijaegemea upande wowote katika mzozo wa Ukraine. Chama cha African National Congress (ANC) kimetofautiana vikali na chama cha Democratic Alliance (DA), mshirika wake mkubwa wa muungano kuhusu uhusiano wa nchi hiyo na Urusi. Chama cha ANC, ambacho kimetawala Afrika Kusini tangu kumalizika kwa utawa...

Hezbollah yamtangaza Naim Qassem kuwa kiongozi wake mpya

Image
  Hezbollah yamtangaza Naim Qassem kuwa kiongozi wake mpya Hezbollah imetangaza kuwa naibu katibu mkuu wa kundi hilo atakuwa mkuu wake mpya. Naim Qassem anachukua nafasi ya kiongozi wa muda mrefu Hassan Nasrallah, ambaye aliuawa katika shambulio la anga la Israel huko Beirut mwezi uliopita. Ni mmoja wa viongozi wachache waandamizi wa Hezbollah ambao wamesalia hai, baada ya Israel kuua viongozi wengi wa kundi hilo katika mfululizo wa mashambulizi. Uteuzi huo unafanyika huku mzozo nchini Lebanon ukiendelea kuongezeka katika wiki za hivi karibuni. Kwa zaidi ya miaka 30, Naim Qassem alikuwa naibu katibu mkuu wa Hezbollah na mmoja wa watu wanaotambulika zaidi katika kundi hilo. Hezbollah ilisema alichaguliwa na Baraza la Shura, kwa mujibu wa kanuni za kundi hilo. Hata hivyo, hajulikani mahali alipo huku baadhi ya ripoti zikionyesha kuwa amekimbilia Iran, ambayo ni mfuasi mkubwa wa Hezbollah. Ikitangaza kupandishwa cheo kwa Qassem, Hezbollah ilitoa taarifa ikimuelezea kama "aliyebeba be...

'Tutaishi vipi bila chakula' – Raia wa Gaza wahofia ukosefu wa msaada baada ya Unrwa kupigwa marufuku

Image
  'Tutaishi vipi bila chakula' – Raia wa Gaza wahofia ukosefu wa msaada baada ya Unrwa kupigwa marufuku Chanzo cha picha, Getty Images BBC Arabic imezungumza na Wapalestina katika Ukanda wa Gaza kuhusu hatua ya kupiga marufuku Unrwa. Om Yousef "Uamuzi wa kuzuia Unrwa kufanya kazi huko Gaza ni mbaya kwa sababu tunapata chakula kupitia wao na watoto wetu wanasomeshwa katika shule zao. "Elimu ni jambo muhimu zaidi. Natumai uamuzi huu hautatekelezwa kwa sababu sio sahihi." Om Sohay "Ni uamuzi mbaya. Kwa sababu hii, hatutapata unga na mafuta. "Hii ni ngumu sana. Tutaishi vipi bila unga, kitu pekee ambacho kinapatikana hapa nchini ni unga na bei ya mfuko mmoja ni shekeli 200 ($54) na hatuwezi kumudu, na chupa moja ya mafuta inauzwa shekeli 35 ($9). "Kinachoendelea ni kibaya. Hatuna chochote katika nchi hii isipokuwa unga kutoka Unrwa. Tunatumai uamuzi huu utasitishwa na kufutwa kwa sababu hii ni ngumu sana." Mohamed "Mimi ni Mohamed niliyefukuz...