Posts

Ukraine 'itapoteza vita' - waziri wa zamani wa mambo ya nje

Image
 Ukraine 'itapoteza vita' - waziri wa zamani wa mambo ya nje Dmitry Kuleba alisema kuwa Kiev ilikuwa "bahati" kupata uungwaji mkono iliopata, lakini sasa haina uwezo wa kuishinda Urusi. Ukraine inakosa mbinu za kupata ushindi dhidi ya Urusi na "itapoteza vita" ikiwa hali itaendelea kama ilivyo, Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje wa Ukraine Dmitry Kuleba ameliambia gazeti la Financial Times, na kuongeza kuwa Rais wa Marekani Joe Biden aliogopa sana vita vya nyuklia. kuipa Kiev silaha ambayo ingehitaji kushinda. "Je, sisi leo tuna njia na zana za kugeuza meza na kubadilisha mwelekeo wa jinsi mambo yanavyofanyika? Hapana, hatufanyi hivyo," Kuleba aliliambia gazeti la Uingereza katika mahojiano yaliyochapishwa Ijumaa, na kuongeza: "Na ikiwa itaendelea hivi, tutapoteza vita." Maoni ya Kuleba yalikuja baada ya Marekani na Ufaransa kuipa Ukraine ruhusa ya kutumia makombora yao ya masafa marefu kushambulia eneo la Urusi linalotambulika kimataifa. I...

Urusi inaweza kuanza tena majaribio ya nyuklia - naibu FM

Image
 Urusi inaweza kuanza tena majaribio ya nyuklia - naibu FM Moscow imeona kusitishwa kwa hiari tangu 1990 Urusi haiondoi kurejea kwa majaribio ya nyuklia, ambayo haijafanya tangu siku za kufifia kwa Muungano wa Kisovieti, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje Sergey Ryabkov amesema. Alipoulizwa katika mahojiano na TASS Jumamosi ikiwa Moscow inazingatia chaguo hili kama jibu la hatua za kuongezeka za Merika, Ryabkov alijibu kwamba "suala liko kwenye ajenda." "Bila kujitanguliza, nitasema tu kwamba hali ni ngumu sana. Inazingatiwa kila mara katika vipengele na vipengele vyake vyote, "alisema. Licha ya kuwa na nguvu kubwa ya nyuklia, Urusi ya kisasa haijawahi kufanya jaribio la nyuklia chini ya kusitishwa kwa hiari, na la mwisho lilianzia 1990 kabla ya kuanguka kwa Umoja wa Soviet. Marekani, mpinzani mkuu wa nyuklia wa Urusi, ilifanya jaribio lake la mwisho mnamo 1992 na tangu wakati huo ilitegemea uigaji wa kompyuta na majaribio ya chini, ikimaanisha kuwa majaribio hayatumii ny...

Wakati washambuliaji walipoteka eneo takatifu la Waislamu

Image
  Wakati washambuliaji walipoteka eneo takatifu la Waislamu Chanzo cha picha, Getty Images Maelezo ya picha, Washambuliaji hao walifika Novemba 20, 1979 wakiwa wamefunga vitambaa vyekundu kwenye vichwa vyao Saa 3 zilizopita Siku ya tarehe 20 Novemba 1979. Ilikuwa ni tarehe ya kwanza ya Muharram. Msikiti mkubwa zaidi wa Makka ulijaa mahujaji wa Pakistani, Indonesia, Morocco na Yemen pamoja na wenyeji. Katika umati huu wa watu pia kulikuwa na waasi, ambao walivaa nguo nyekundu zilizofunika vichwa vyao. Baadhi yao walikuwa wamekaa msikitini kwa siku kadhaa wakiangalia muundo wake wa ndani na Barabara zake. Baadhi ya watu hao walifika Makka wakiwa na watoto wao na wake zao katika magari siku hiyo hiyo, ili vikosi vya usalama visiwashuku. Wengi wao walikuwa ni kutoka kabila la Baddus, la Saudia. Matangazo Maombi ya Fajr tayari yalikuwa yameanza. Sauti ya Imam ilisikika juu. Muda ulikuwa saa tano na dakika kumi na nane asubuhi. Yaroslav Trofimov ametoa maelezo ya kuvutia ya ...

Tetesi za soka Ulaya: Real wamtaka Alexander-Arnold

Image
  Tetesi za soka Ulaya: Real wamtaka Alexander-Arnold Chanzo cha picha, Getty Images Maelezo ya picha, Trent Alexander-Arnold Saa 3 zilizopita Real Madrid wameifahamisha Liverpool kuhusu nia yao ya kutaka kumsajili beki wa Uingereza Trent Alexander-Arnold, 26. (TalkSport) Kocha mpya wa Manchester United Ruben Amorim ameazimia kufanya kazi na wachezaji wake wa sasa na hajatuma ombi kwa uongozi wa klabu kuhusu usajili wowote wa Januari. (Sky Sports) Chanzo cha picha, Getty Images Maelezo ya picha, Lutsharel Geertruida Tottenham wana nia ya kumsajili beki wa kulia wa RB Leipzig Mholanzi Lutsharel Geertruida, mweney umri wa miaka 24, kama kiungo mbadala wa Pedro Porro, mwenye umri wa miaka 25, ambaye analengwa na Real Madrid . (Caught Offside) Mshambuliaji wa Ipswich Town mwenye umri wa miaka 21, Liam Delap anavutiwa na vilabu kadhaa vya Ligi ya Primia. (Athletic - subscription required) Matangazo Chanzo cha picha, Getty Images Maelezo ya picha, Cunha Manchester United ...

Israel yaonya raia dhidi ya kurejea katika vijiji 60 vya Lebanon

Image
  Israel yaonya raia dhidi ya kurejea katika vijiji 60 vya Lebanon Chanzo cha picha, Reuters Jeshi la Israel limewaonya raia wa Lebanon kutorejea katika vijiji 60 kusini mwa nchi hiyo, siku tatu baada ya kusitishwa kwa mapigano baada ya zaidi ya mwaka mmoja wa mapigano na kundi la wapiganaji la Shia la Hezbollah. Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) lilichapisha ramani inayoonyesha eneo lenye kina cha maili kadhaa, ambalo lilisema wakazi hawapaswi kurudi. Yeyote atakayefanya hivyo, lilisema, atakuwa anajiweka hatarini. Zaidi ya Walebanon milioni moja wamekimbia makazi yao kutokana na mapigano hayo, wengi wao kutoka kusini. Makumi ya maelfu ya Waisraeli pia wameyakimbia makazi yao. Usitishaji wa mapigano ulianza kutekelezwa Jumatano asubuhi, ingawa maafisa wa Israeli na Lebanon wameshtumu kila mmoja kuwa tayari amekiuka. Siku ya Alhamisi, IDF ilisema vikosi vyake vilifyatua mizinga na kufanya mashambulizi ya anga dhidi ya wappiganaji kusini mwa Lebanon. Iliongeza kuwa il...

Chama cha ACT wazalendo chataka uchaguzi wa serikali za mitaa urudiwe

  Chama cha ACT wazalendo chataka uchaguzi wa serikali za mitaa urudiwe Chama cha upinzani cha ACT Wzalendo nchini Tanzania kimetaka uchaguzi wa serikali za Mitaa urudiwe na matokeo yaliyotangazwa na Wizara ya TAMISEMI kufutiliwa mbali. "ACT hatukubaliani na matokeo yaliyotangazwa na Waziri wa TAMISEMI, kwani mchakato mzima wa uchaguzi umevurungwa kwa kiwango ambacho kimepora madaraka ya wananchi kuchagua viongozi wao,' imesema sehemu ya taarifa ya chama hicho. Serikali kupitia Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ilitangaza matokeo ya uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika hivi karibuni, ambapo chama kinachoongoza nchi, Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimeshinda kwa asilimia 98.8, kikiibuka na ushindi wa nafasi 4,213 katika nafasi za serikali za mitaa. Kwa upande mwingine, chama kikuu cha upinzani, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimeshinda nafasi 36 pekee, sawa na asilimia 0.84 ya jumla ya nafasi zilizogomb...

Tanzania: Wamiliki wa jengo la Kariokoo washtakiwa kwa mauaji ya kutokusudia

Image
  Tanzania: Wamiliki wa jengo la Kariokoo washtakiwa kwa mauaji ya kutokusudia Watu watatu wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam wakikabiliwa na mashtaka 31 ya kuua bila kukusudia. Washtakiwa wanaodaiwa kuwa ni wamiliki wa jengo lililoporomoka katika makutano ya Mitaa ya Mchikichi na Kongo, Kariakoo, Dar es Salaam na kusababisha vifo vya watu 29, walipandishwa kizimbani, Ijumaa, Novemba 29, 2024. Washitakiwa hao waliotambuliwa kuwa Leondela Mdete (49) mkazi wa Mbezi Beach; Zenabu Islam (61), mkazi wa Kariakoo; na Ashour Awadh Ashour (38), mkazi wa Ilala. Washitakiwa hao wanadaiwa kuwa Novemba 16, 2024 katika mitaa ya Mchikichi na Kongo, Kariakoo, Dar es Salaam, kinyume cha sheria na kwa pamoja walishindwa kutimiza wajibu wao na kusababisha vifo vya watu 29. Akitembelea eneo la Kariakoo mara baada ya kuwasili kutoka kuhudhuria Mkutano wa Viongozi wa G20 mjini Rio de Janeiro, Brazil, Rais Samia Suluhu Hassan aliridhia zoezi la kufa...

'Nilimuuzia nyumba mtu aliyekuwa akisakwa na FBI'

Image
  'Nilimuuzia nyumba mtu aliyekuwa akisakwa na FBI' Chanzo cha picha, Aled Evans Saa 4 zilizopita Mwanamume mmoja ambaye alimuuzia nyumba yake mtu ambaye alibainika kuwa kwenye orodha ya watu wanaotafutwa sana na FBI amesema kuwa hilo lilikuwa eneo linalofaa "ikiwa ungetaka kujificha. Daniel Andreas San Diego alilipa pauni 425,000 kwa ajili ya nyumba hiyo karibu na Llanrwst kaskazini mwa Wales mnamo Agosti 2023 akitumia jina la Danny Webb. Siku ya Jumatatu, Bw San Diego - ambaye kitita cha $250,000 (£199,000) kilitangazwa kwa atakayefanikisha kutoa taarifa zake,alikamatwa huko Maenan baada ya miaka 21 ya kukimbia kufuatia milipuko miwili huko San Francisco mnamo 2003 ambayo alishukiwa kuhusika. "Alifurahi sana kwa sababu kulikuwa na msitu mkubwa nyuma ya nyumba, alikuwa akiendesha baiskeli yake na hiyo ndiyo iliyomuuzia," alisema Aled Evans. "Ilionekana kama mahali pazuri alipopataka - lakini alitaka kwa sababu zake nyingine," aliiambia BBC ...

Russia: Marekani na Uingereza zinaeneza machafuko ndani ya Syria kupitia magenge ya kigaidi

Image
  Russia: Marekani na Uingereza zinaeneza machafuko ndani ya Syria kupitia magenge ya kigaidi Nov 29, 2024 11:41 UTC Russia imesema madola makubwa ya Magharibi yanayoongozwa na Marekani yanaendelea na vitendo vyao vya chuki dhidi ya Syria kwa kuwaunga mkono wanamgambo wanaoipinga serikali ya Damascus pamoja na makundi ya kigaidi ya kitakfiri katika kila pembe ya nchi hiyo ya Kiarabu. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia Maria Zakharova amezikosoa Marekani, Uingereza na baadhi ya nchi nyingine za Magharibi kwa kueneza machafuko katika kila pembe ya Syria kupitia makundi ya kigaidi.   Zakharova ameongeza kuwa, uungaji mkono wa serikali za Magharibi kwa makundi ya kigaidi yanayoendesha harakati zao katika kila pembe ya Syria si jambo lililobaki kuwa siri bali limeshafichuliwa na liko wazi hadharani.   Amesema: "majaribio ya kulilenga taifa...

Macron akiri ilichofanya Ufaransa 1944 kwa askari wa Afrika Magharibi ni "mauaji ya halaiki"

Image
  Macron akiri ilichofanya Ufaransa 1944 kwa askari wa Afrika Magharibi ni "mauaji ya halaiki" Nov 29, 2024 11:41 UTC Kwa mara ya kwanza, Rais wa Ufaransa ameyatambua mauaji ya wanajeshi wa Afrika Magharibi yaliyofanywa na Jeshi la Ufaransa mwaka 1944 kuwa ni "mauaji ya halaiki. Macron amechukua hatua hiyo kupitia barua aliyoziandikia Mamlaka za Senegal. Hayo yamethibitishwa na Rais Bassirou Diomaye Faye wa Senegal katika kipindi cha mahojiano aliyofanyiwa na televisheni ya taifa ya Ufaransa kilichorushwa hewani jana Alkhamisi.   Hatua ya Macron inakuja katika mkesha wa kuadhimisha miaka 80 ya mauaji ya Vita vya Pili vya Dunia huko Thiaroye - kijiji cha wavuvi nje kidogo ya mji mkuu wa Senegal, Dakar.   Waafrika Magharibi walikuwa askari wa kitengo kilichoitwa Tirailleurs Senegalais, kikosi cha askari wa miguu katika Jeshi la kikoloni la Ufaransa. ...

Israel yakiuka makubaliano ya kusitisha vita Lebanon, yaendelea kuua Wapalestina Ghaza

Image
  Israel yakiuka makubaliano ya kusitisha vita Lebanon, yaendelea kuua Wapalestina Ghaza Nov 29, 2024 11:42 UTC Jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel limefanya mashambulizi mapya dhidi ya Lebanon kinyume na makubaliano ya kusitisha mapigano liliyofikia na harakati ya Muqawama ya Hizbullah; na wakati huohuo limeshaddisha mashambulizi yake ya kinyama ya anga katika Ukanda wa Ghaza. Taarifa iliyowekwa na jeshi la Lebanon kwenye mtandao wa X imesema, vikosi vya jeshi vamizi la Israel vimekiuka mara kadhaa makubaliano ya kusitisha mapigano baada tu ya kuanza kutekelezwa, na pia siku iliyofuata.   Taarifa hiyo imeongezea kwa kusema: "ukiukaji huu unajumuisha ukiukaji wa angani na mashambulizi katika ardhi ya Lebanon kwa kutumia silaha mbalimbali".   Jeshi la utawala ghasibu wa Israel limethibitisha kuwa lilifanya shambulio la anga jana Alhamisi kusini m...

Daktari aangua kilio wakati anasimulia unyama wa Israel dhidi ya Wapalestina wa Ghaza

Image
  Daktari aangua kilio wakati anasimulia unyama wa Israel dhidi ya Wapalestina wa Ghaza Nov 29, 2024 11:42 UTC Daktari Tanya Haj-Hassan, ameangua kilio katika mkutano wa Umoja wa Mataifa alipokuwa akisimulia tajiriba aliyopitia katika Ukanda wa Ghaza unaoendelea kushuhudia vita vya kinyama na mauaji ya kimbari yanayofanywa na jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina wa eneo hilo lililowekewa mzingiro. Haj-Hassan ambaye alikuwa akihutubia kwa mnasaba wa Siku ya Kimataifa ya Mshikamano na Watu wa Palestina inayoadhimishwa kila mwaka Novemba 29, amesimulia kumbukumbu za mateso wanayopata Wapalestina aliyoyashuhudia kwa macho yake wakati alipokuwa Ghaza.   Daktari Tanya Haj-Hassan amesema: "ninataka ulimwengu wote ujue kuwa baada ya yote, mimi ni mwanadamu, si kalamu iandikayo kwenye karatasi. Si kiumbe nisiyejulikana. Mimi ni mwanadamu ...

Khatibu wa Sala ya Ijumaa: Magharibi iwezeshe kufanyika mazungumzo kwa kuheshimu haki za taifa la Iran

Image
  Khatibu wa Sala ya Ijumaa: Magharibi iwezeshe kufanyika mazungumzo kwa kuheshimu haki za taifa la Iran Nov 29, 2024 12:08 UTC Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya mjini Tehran amesema: "ikiwa Magharibi itarekebisha mwenendo wake na pande mbili zikaheshimiana, itaweza kuandaa mazingira ya kufanyika mazungumzo na kufikia makubaliano na Iran". Hujjatul-Islam Wal-Muslimin Mohammad Hasan Abu Turabi Fard amesema Iran yenye nguvu daima iko tayari kwa majadiliano na mazungumzo ya kimantiki na ya kielimu, na akaongezea kuwa, ikiwa Magharibi itarekebisha mwenendo wake na pande mbili zikaheshimiana; na ikazingatia haki za taifa adhimu na lenye nguvu la Iran itaweza kuandaa mazingira ya kufanywa mazungumzo na kufikia makubaliano.   Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya Tehran ameongeza kuwa: Umoja wa Ulaya haunufaiki na sifa ya kuwa taasisi huru na inayojitegemea, kwa sababu maslahi ...

China yamfunga mwandishi wa habari aliyepatikana na hatia ya ujasusi

Image
  China yamfunga mwandishi wa habari aliyepatikana na hatia ya ujasusi Chanzo cha picha, Reuters Mwanahabari wa zamani wa vyombo vya habari vya serikali ya China amehukumiwa kifungo cha miaka saba jela kwa kosa la ujasusi, familia yake imethibitishia kwa BBC. Dong Yuyu, 62, ambaye amekuwa kizuizini tangu 2022, alikuwa akifanya kazi katika nchini Marekani na Japan na alikutana mara kwa mara na wanadiplomasia wa kigeni. Alikuwa akila chakula cha mchana na mwanadiplomasia wa Japan mjini Beijing alipokamatwa na polisi. Wakati wa kuzuiliwa kwake, Dong alikuwa mfanyakazi mkuu wa gazeti la Guangming Daily, mojawapo ya magazeti makuu matano yanayohusishwa na Chama cha Kikomunisti cha China. Mnamo Februari 2022, Dong alikamatwa akiwa anakula chakula cha mchana na mwanadiplomasia wa Japan siku moja baada ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi kumalizika huko Beijing, kwenye mgahawa ambapo mara nyingi alikuwa akikutana na marafiki wa kigeni. Mwanadiplomasia huyo pia alizui...

Mashirika ya ndege ya India yamekumbwa na vitisho 1,000 vya uongo vya mabomu

Image
  Mashirika ya ndege ya India yamekumbwa na vitisho 1,000 vya uongo vya mabomu Chanzo cha picha, Getty Images Mashirika ya ndege na viwanja vya ndege vya India vilipokea vitisho 999 vya uongo mashambulio ya mabomu mwaka huu kufikia tarehe 14 Novemba, naibu waziri wa usafiri wa anga wa nchi hiyo aliliambia bunge lake. Hii ilikuwa karibu mara 10 zaidi ya vitisho vilivyopokelewa mnamo 2023, Bw Murlidhar Mohol alisema. Zaidi ya vitisho 500 vya mwaka huu vilipokelewa katika wiki mbili zilizopita za mwezi Oktoba. Ongezeko kubwa la vitisho vya uongo lilikuwa limesababisha uharibifu kwenye ratiba za ndege, na kusababisha usumbufu mkubwa katika mpango wa utoaji huduma. Vitisho vya hivi majuzi vyote ni uwongo, Bw Mohol alisema, na "hakuna tishio halisi lililogunduliwa katika viwanja vya ndege nchini India". Polisi wamepokea malalamiko 256 na watu 12 wamekamatwa kuhusiana na vitisho hivi, waziri alisema. Lakini visa hivyo vinaashiria ongezeko ambalo halijawahi kushuhudiwa vya ...

Chad yasitisha makubaliano ya kijeshi na Ufaransa

Image
  Chad yasitisha makubaliano ya kijeshi na Ufaransa Chanzo cha picha, AFP Maelezo ya picha, Takriban wanajeshi 1,000 wa Ufaransa kwa sasa wako nchini Chad Chad imesema inasitisha makubaliano muhimu ya ushirikiano wa kiulinzi na Ufaransa, na hivyo kuzua maswali kuhusu kupungua kwa ushawishi wa Paris katika eneo linalokabiliwa na mzozo la Sahel barani Afrika. Waziri wa Mambo ya Nje wa Chad Abderaman Koulamallah alisema ni wakati wa nchi yake "kudai mamlaka yake kamili". Tangazo hilo limekuja saa chache baada ya mwenzake wa Koulamallah wa Ufaransa, Jean-Noel Barrot, kukutana na Rais wa Chad Mahamat Deby. Chad ni mshirika mkuu katika mapambano ya nchi za Magharibi dhidi ya wanamgambo wa Kikijihadi katika eneo la Sahel huko Afrika Magharibi. Lakini kabla ya uchaguzi wa rais mwezi Mei, mamlaka ya Chad iliamuru kuondolewa kwa wanajeshi wa Marekani nchini humo, kuashiria kujiwtengai na washirika wa jadi wa nchi hiyo wa Magharibi. Ufaransa kwa sasa ina takriban wanajeshi 1...

Israel yaonya raia dhidi ya kurejea katika vijiji 60 vya Lebanon

Image
  Israel yaonya raia dhidi ya kurejea katika vijiji 60 vya Lebanon Chanzo cha picha, Reuters Jeshi la Israel limewaonya raia wa Lebanon kutorejea katika vijiji 60 kusini mwa nchi hiyo, siku tatu baada ya kusitishwa kwa mapigano baada ya zaidi ya mwaka mmoja wa mapigano na kundi la wapiganaji la Shia la Hezbollah. Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) lilichapisha ramani inayoonyesha eneo lenye kina cha maili kadhaa, ambalo lilisema wakazi hawapaswi kurudi. Yeyote atakayefanya hivyo, lilisema, atakuwa anajiweka hatarini. Zaidi ya Walebanon milioni moja wamekimbia makazi yao kutokana na mapigano hayo, wengi wao kutoka kusini. Makumi ya maelfu ya Waisraeli pia wameyakimbia makazi yao. Usitishaji wa mapigano ulianza kutekelezwa Jumatano asubuhi, ingawa maafisa wa Israeli na Lebanon wameshtumu kila mmoja kuwa tayari amekiuka. Siku ya Alhamisi, IDF ilisema vikosi vyake vilifyatua mizinga na kufanya mashambulizi ya anga dhidi ya wappiganaji kusini mwa Lebanon. Iliongeza kuwa il...

Emmanuel Wanyonyi: Kutoka kuchunga ng'ombe hadi kuwa bingwa wa Olimpiki

Image
  Emmanuel Wanyonyi: Kutoka kuchunga ng'ombe hadi kuwa bingwa wa Olimpiki Chanzo cha picha, BBC Sport Africa Maelezo ya picha, Tangu ashinde medali ya dhahabu kwenye Michezo ya Olimpiki ya Paris 2024, Emmanuel Wanyonyi amerejea nyumbani kwa familia yake mjini Kitale kusaidia majukumu ya kila siku. Maelezo kuhusu taarifa Author, Kelvin Kimathi Nafasi, BBC Sport Africa, Nairobi Saa 2 zilizopita Alikulia katika umaskini uliokithiri katika kijiji kidogo magharibi mwa Kenya, maisha ya kila siku ya Emmanuel Wanyonyi yalikuwa magumu. Alipolazimika kuacha shule akiwa na umri wa miaka 10, alifanya kazi ya kulisha ng'ombe kwa muda mrefu. Wakati mwingine alipata chini ya $2 kwa mwezi. Wanyonyi alivumilia mateso na kutumiwa vibaya, akibadili kazi mara kwa mara baada ya wakati mwingine kutolipwa, lakini mwanamume ambaye alikuja kuwa bingwa wa Olimpiki wa mita 800 alivumilia kwa sababu makazi na chakula vilitolewa. "Maisha, na kuchunga ng'ombe kama mtoto, yalikuwa magu...