Posts

Biden apata shinikizo la kuruhusu silaha za Marekani kuishambulia Urusi

Image
  Shinikizo linaongezeka kwa Rais wa Marekani Joe Biden kuruhusu Ukraine kutumia silaha zinazotolewa na nchi za Magharibi kushambulia eneo la Urusi. Washirika kadhaa wa Marekani wiki hii waliashiria kuwa wako tayari kwa uwezekano huu. Rais wa Urusi Vladimir Putin ameonya kuhusu "athari kubwa", hasa kwa kile alichokiita "nchi ndogo" barani Ulaya. Siku ya Jumatano, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken alisema msimamo wa Washington kuhusu suala hilo "utabadilika na kurekebishwa" kulingana na mabadiliko ya hali ilivyo vitani. Kwa sasa yuko katika mji mkuu wa Czech, Prague, kwa mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa Nato. Msemaji wa usalama wa taifa wa White House John Kirby alisema jioni Jumatano kwamba ingawa uungaji mkono wa Marekani kwa Ukraine umebadilika, "hivi sasa, pia hakuna mabadiliko katika sera yetu". Ukraine imekuwa ikijitahidi kukabiliana na mashambulizi ya Urusi mashariki mwa nchi hiyo, huku jiji la Kharkiv likikumbwa na ma...

Kila mwanachama wa NATO ana wanajeshi huko Ukraine - Estonia

Image
   Kila mwanachama wa NATO ana wanajeshi huko Ukraine - Estonia Washauri na wakufunzi wa nchi za Magharibi wanaunga mkono kikamilifu vikosi vya Kiev dhidi ya Urusi, waziri wa ulinzi amesema Kila mwanachama wa NATO tayari ana wanajeshi nchini Ukraine, Waziri wa Ulinzi wa Estonia Hanno Pevkur alidai Jumatatu. Hata hivyo, kwa hali yoyote hakuna vikosi vya muungano unaoongozwa na Marekani vitashiriki katika uhasama dhidi ya Urusi, waziri huyo alisisitiza katika mahojiano na chombo cha habari cha Austria cha Die Presse. Wanajeshi wa NATO wanafanya kazi katika nchi iliyozozaniwa kama washauri na wanahusika katika kutoa mafunzo kwa wanajeshi wa Ukraine huko Poland, Uingereza na Estonia, Pevkur aliambia chombo. Maafisa wa ulinzi wa nchi za Magharibi kwa sasa wanapanga kuweka kambi za mafunzo nchini Ukraine katika jitihada za kuepuka masuala ya kuvuka mpaka na kuharakisha mchakato wa maandalizi, aliongeza. Wakati huo huo, Pevkur alisisitiza kuwa hakuna mazungumzo ya wanajeshi wa NATO k...

TAZAMA mwanajeshi wa Urusi akishambulia mtaro wa Kiukreni

Picha za POV zilizopatikana na RT zinaonyesha mapigano makali ya karibu Picha za kamera za mwili zilizopatikana na RT zinaonyesha askari wa Urusi akivamia maeneo ya Ukrainia na kusafisha mitaro. Video hiyo ilirekodiwa na mtumishi mwenyewe. Klipu hiyo inaanza na askari kuingia kwenye mtaro na kufyatua bunduki ya kushambulia. Mwanamume huyo anarusha bomu na kishindo na mlio usio na sauti unasikika kwa nyuma. Askari huyo anaingia kwenye shimo, ambapo miili mitatu imelala chini karibu na makreti ya risasi na silaha ya kukinga mizinga. Kulingana na RT Russian, mfumo wa kombora unaoongozwa na Uswidi-Uingereza NLAW na kirusha guruneti cha Uswidi AT-4 zilipatikana kwenye mtaro na wanajeshi wa Urusi. Tarehe na eneo kamili ambapo video ilirekodiwa haijathibitishwa. Mwanajeshi aliyekufa aliyeonekana kwenye video hiyo alikuwa amejihami kwa bunduki ya kivita iliyotengenezwa Marekani na alikuwa amevalia sare yenye kiraka cha Kikosi cha Telemark cha Norway, RT Russian ilisema. Uraia wa mwanajeshi huy...

Jeshi la Sudan lakataa wito wa Marekani wa kuzungumza na waasi

Image
Jeshi la Sudan limekataa wito wa kurejea kwenye mazungumzo ya usitishaji vita na kundii la waasi la RSF kufuatia mazungumzo kati ya kiongozi wa Sudan Jenerali Abdel Fattah al-Burhan na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken. Blinken alimpigia simu al-Burhan juzu ambapo alijaribu kumshawishi afanya mazungumzo na waasi wa RSF. Afisa mwandamizi wa Sudan Malik Agar amapinga uingiliaji wa Marekani na kusema: "Hatutakwenda Jeddah (Saudi Arabia) na yeyote anayetutaka atuue katika nchi yetu na kuipeleka miili yetu huko." Marekani imekuwa ikisiamamia mazungumzo hayo ya waasi na serikali ya Sudan huko Jeddah. Hatahivyo mazungumzo hayo hadi sasa hayajafanikiwa. Mapigano makali yaliendelea Jumatano katika maeneo ya kaskazini mwa mji mkuu, huku wakaazi wakiripoti mashambulizi makali ya angani na mizinga. Sudan hataivyo imekaribisha mwaliko wa Misri wa mkutano wa kilele wa makundi ...

Usajili wa wagombea wa uchaguzi mapema wa rais wa Iran waanza

Image
Iran leo imezindua mchakato wa siku tano wa usajili kwa watu wanaotarajia kugombea katika uchaguzi wa 14 wa rais kuchukua nafasi ya Ebrahim Raisi aliyekufa shahidi maisha katika ajali ya helikopta mapema mwezi huu. Rais, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Hossein Amir-Abdollahian na wengine sita walikufa shahidi Mei 19, wakati helikopta yao ilipoanguka katika hali mbaya yaa hewa ya ukungu katika milima karibu na mpaka wa kaskazini-magharibi mwa nchi. Wagombea wote lazima waidhinishwe na Baraza la Walinzi wa Katiba lenye  wanachama 12. Hicho ni chombo kikuu cha usimamizi wa uchaguzi nchini. Wizara ya Mambo ya Ndani itatangaza majina ya walioidhinishwa tarehe 11 Juni. Kufuatia kufa shahidi Rais Rasi na wenzake, wakuu wa mihimili mitatu ya dola nchini Iran walikubaliana Jumatatu kwamba uchaguzi wa rais wa haraka utafanyika tarehe 28 Juni. Kulingana na ratiba iliyotangazwa na serikali, kampe...

Makamba: Mataifa ya Afrika yawe na haki ya kuchagua washirika

Image
  Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania January Makamba Kila taifa la Afrika na bara zima lazima liwe na uwezo wa kujitegemea katika kuchagua washirika wake na kulinda maslahi yake binafsi Makamba amenukuliwa na Shirika la Habari la Sputnik la Russia akisema: "Sisi [Waafrika] tunaona inakera kushinikizwa kuchagua mshirika huyu mmoja au mwingine." Aidha amesema uhuru wa kweli na uhuru wa Afrika unaweza kupatikana kwa kujitegemea na kwa umoja. Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania pia alikosia mataifa ya kikoloni na mataifa mengine ya Magharibi kwa kujaribu kurejesha satwa yao ya kibeberu  Afrika, jambo ambalo linazifanya nchi kama Niger, Mali, na Burkina Faso "kuwafukuza" wakoloni wao wa zamani. Makamba ameendelea kusema kuwa: " Nchi za Ulaya, na hasa Marekani, hivi sasa, zinajaribu kurejea tena kwa kasi Afrika." Hivi karibuni Ufaransa imekuwa ikipata hasara kubwa ba...

Zoezi la kuhesabu kura Afrika Kusini laendelea huku ANC ikikabiliwa na uwezekano wa kupoteza viti

Image
Zoezi la kuhesabu kura linaendelea Afrika Kusini baada ya uchaguzi wa Jumatano uliokuwa na ushindani mkali huku chama tawala ANC kikikabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa wanasiasa waliojiondoa katika chama hicho. Matokeo ya awali yanaonyesha ANC itapoteza wingi wa viti bungeni. Tume Huru ya Uchaguzi (IEC) imesema upigaji kura wa dakika za mwisho katika miji mikubwa ulipelekea kuongezwa muda wa kupiga kura. Chama cha ANC kimetawala siasa za Afrika Kusini tangu 1994 wakati kiongozi wa ukombozi Shujaa Nelson Mandela aliposhinda uchaguzi wa kwanza wa kidemokrasia nchini humo. Kura za maoni zinaonyesha kuwa ANC inaweza kushinda takribani asilimia 40 ya kura, kutoka asilimia 57 mwaka 2019, lakini hakuna chama cha upinzani kinachotarajiwa kupata zaidi ya asilimia 25 ya viti. Iwapo ANC itafanya vyema na kupata karibu asilimia 50 inaweza kushirikiana na baadhi ya vyama ndogo na vyama vya kikanda...

Mtandao mkubwa wa uhalifu kwa njia ya kompyuta wafungwa duniani: Marekani

Image
Idara za kipolisi kote ulimwenguni kote zimefunga mtandao wa kimataifa wa programu ambao uliiba $5.9bn (£4.65bn) na unahusishwa na uhalifu mwingine, Wizara ya Sheria ya Marekani (DOJ) imesema. DOJ ilishirikiana na FBI na mashirika mengine ya kimataifa ili kuondoa kile kinachowezekana kuwa mtandao wa kompyuta zilizoathiriwa na programu ambazo ziko chini ya udhibiti wa mtu mmoja. Raia wa China YunHe Wang, ambaye pia ni mkazi wa St Kitts na Nevis citizen ameshtakiwa kwa kuunda na kuendesha mtandao huo. Bw Wang anashtakiwa kwa njama ya kufanya ulaghai kwa njia ya mtandao wa kompyuta, njama ya kufanya ulaghai kwa njia ya mtandao na kula njama ya kutakatisha pesa. Iwapo atapatikana na hatia kwa makosa yote, anakabiliwa na adhabu ya juu zaidi ya miaka 65 jela. Kulingana na shtaka, kati ya 2014 hadi 2022, Bw.Wang na wengine waliunda na kuendesha mtandao uitwao 911 S5, kutoka kwa seva 150 kote ulimwenguni. Mtandao huo ulidukuliwa katika zaidi ya anwani milioni 19 za Itifaki ya Mtan...

Watu weusi walishtaki shirika la ndege, American Airlines kwa ubaguzi wa rangi

Image
Wanaume watatu weusi wamewasilisha kesi ya ubaguzi wa rangi dhidi ya shirika la ndege la American Airlines, wakidai kuwa ndege hiyo iliwaondoa kwa muda kutoka kwa ndege baada ya malalamiko kuhusu harufu ya mwili. Wanaume hao, ambao hawakuketi pamoja na hawakujuana, wanasema kuwa kila mtu mweusi aliondolewa kwenye ndege ya Januari 5 kutoka Phoenix, Arizona, hadi New York. "American Airlines ilitutenga kwa kuwa watu Weusi, ilituaibisha, na ilitudhalilisha," watu hao walisema katika taarifa ya pamoja siku ya Jumatano. Shirika hilo la ndege lenye makao yake makuu Texas, lilisema kuwa linachunguza suala hilo kwani madai hayo hayaendani na maadili yake. Kulingana na kesi iliyowasilishwa na kundi la kutetea wateja la Public Citizen, watu hao walikuwa tayari wameketi na walikuwa wakijiandaa kuondoka Phoenix wakati mhudumu wa ndege alipomwendea kila mmoja wao na kuwataka watoke nje ya ndege. Alvin Jackson, Emmanuel Jean Joseph, na Xavier Veal wanadai kuwa, walipokuwa ...

Mwanafunzi wa miaka 85 asoma shahada yake ya nne

Image
  Mwanafunzi mwenye umri wa miaka 85 ambaye anasoma shahada yake ya nne ya chuo kikuu anasema "hawezi kuketi tu". Lucille Terry kutoka Cirencester alimaliza shahada yake ya kwanza, katika taaluma ya dawa, katika Chuo Kikuu cha Manchester mnamo 1962. Atamaliza shahada yake ya nne, ya tatu katika Chuo Kikuu Huria, atakapokuwa na umri wa miaka ya tisini. Bi Terry alitunukiwa katika sherehe katika kanisa la parokia yake siku ya Jumatatu. Bi Terry, ambaye alifanya kazi ya ualimu, kwa sasa anasomea shahada ya masomo ya kidini, falsafa na maadili. Mkazi wa Siddington Park pia ana shahada ya masuala ya ubinadamu, saikolojia na ubinadamu na masomo ya kidini, na alifanya masomo ya msingi ya sayansi katika Chuo Kikuu Huria mnamo 1972, kabla ya kusomea cheti chake cha ualimu. Bi Terry aliamua kwamba hakutaka "kucheza tu mchezo wa mafumbo ya maneno" wakati wa kustaafu kwake. "Siwezi kuketi tu, bila kufanya chochote na kutazama televisheni wakati wote," alisema. ...

Saa 3 zilizopitaUchaguzi Afrika Kusini 2024: Matokeo ya kwanza yatangazwa

Image
  Matokeo ya kwanza yametangazwa ya uchaguzi unaoonekana kuwa wenye ushindani zaidi nchini Afrika Kusini tangu chama cha African National Congress (ANC) kiingie madarakani miaka 30 iliyopita. Huku matokeo kutoka kwa zaidi ya asilimia 11 ya wilaya za wapiga kura yamehesabiwa kufikia sasa, ANC inaongoza kwa 43%, ikifuatiwa na DA yenye 26%. Chama chenye msimamo mkali cha EFF na Umkhonto weSizwe (MK Party) cha Rais wa zamani Jacob Zuma vina karibu 8%. Matokeo ya mwisho yanatarajiwa mwishoni mwa juma. Kura za maoni zinaonesha kuwa chama cha ANC kinaweza kupoteza wingi wake bungeni kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 30. Chama cha ANC kimepoteza uungwaji mkono kutokana na hasira juu ya viwango vya juu vya rushwa, uhalifu na ukosefu wa ajira. Lakini ni mapema sana kutabiri matokeo ya mwisho. Uchaguzi wa Alhamisi ulishuhudia misururu mirefu ya wapiga kura nje ya vituo vya kupigia kura hadi usiku wa manane kote nchini.

Rais Ruto: 'Marafiki wa Kenya' walilipia ndege yangu kwenda Marekani

Image
  Rais wa Kenya William Ruto amesema ndege yake aliyosafiri nayo kwenda Marekani iligharmiwa na walipa kodi wa Kenya kiasi cha chini ya milioni 10 Ruto amesema kuwa baadhi ya marafiki wa Kenya ambão hakuwataja, walitoa ndege hiyo, baada ya kusema kuw angesafiri na ndege ya shirika la Ndege la Kenya. ‘’Nilipoona mjadala Kenya kuhusu ni kwa namna gani nilisafiri kwenda Marekani na gharama mbalimbali zikielezwa kuwa….hii imegharimu milioni 200, hakuna namna ninayoweza kutumia sh milioni 200. Acha niwaambie hapa, hii imeigharimu kiasi cha chini ya shilingi milioni 10’’, alisema Rais Ruto.

Mwanaume afariki dunia kwenye injini ya ndege Amsterdam

Image
  Mtu mmoja afariki dunia baada ya kuishia kwenye injini ya ndege ya abiria ya KLM katika uwanja wa ndege wa Schiphol mjini Amsterdam. Kifo hicho kilitokea wakati ndege ya KL1341 ilipokuwa ikijiandaa kuondoka kuelekea Billund, Denmark, Jumatano alasiri. Shirika hilo la ndege limesema linawahudumia abiria na wafanyakazi walioshuhudia tukio hilo na linaendelea na uchunguzi. Polisi wa kijeshi wa Netherland pia walisema kuwa wameanza uchunguzi. Kikosi cha Royal Netherlands Marechaussee kiliongeza katika ujumbe kwenye mtandao wa X kwamba abiria na wafanyikazi wote wameondolewa kwenye ndege. Marehemu bado hajatambuliwa na ni mapema mno kusema ikiwa ilikuwa ajali au aina ya kujitoa uhai, msemaji aliliambia shirika la habari la Reuters. Vyombo mbalimbali vya habari vya Uholanzi vimependekeza mwathiriwa anaweza kuwa mfanyakazi anayehusika katika kuelekeza ndege kurudi nyuma kabla ya kupaa. Picha zilizopatikana na shirika la utangazaji la taifa la Uholanzi NOS zinaonyesha huduma za dharura z...

Uchunguzi wa helikopta ya Raisi unazua maswali zaidi - Iran

Image
Sababu nyingi za ajali mbaya zimekataliwa na wachunguzi Wachunguzi wa Iran bado hawajabaini kilichosababisha ajali ya helikopta iliyomuua Rais Ebrahim Raisi, lakini wamefutilia mbali hujuma, shirika la utangazaji la serikali IRIB liliripoti Jumatano. Helikopta ya Bell 212 iliyotengenezwa na Marekani iliyokuwa imembeba Raisi na Waziri wa Mambo ya Nje Hossein Amir-Abdollahian ilianguka Mei 19 katika jimbo la Azerbaijan Mashariki la Iran na kuua kila mtu aliyekuwa ndani yake. Wafanyikazi Mkuu wa jeshi la Iran wamepewa jukumu la kuchunguza sababu. "Mlipuko ambao unaweza kutokea kutokana na hujuma wakati wa safari ya ndege, au sekunde chache kabla ya kugongana na mteremko wa kilima umekataliwa," ilisema taarifa iliyotolewa na Wafanyakazi Mkuu, kama ilivyoripotiwa na IRIB. Baada ya kuchunguza nyaraka na rekodi zinazohusiana na ndege ya rais, "hakuna dosari ambazo zingeweza kuathiri ajali zilipatikana katika suala la ukarabati na matengenezo," jeshi liliongeza. Kadhalika, ...

Rais wa Venezuela: Marekani na EU zinanyamazia kimya jinai za Kinazi za Israel huko Gaza

Image
 ay 30, 2024 02:30 UTC Rais wa Venezuela amezilaani Marekani na Umoja wa Ulaya kwa kutofanya lolote kukomesha mauaji "ya kutisha" ya Israel dhidi ya Wapalestina. Nicolas Maduro amelaani vikali mauaji yanayotekelzwa na Israel katika Ukanda wa Gaza na kuyafananisha na jinai za kutisha zaidi katika historia. Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Maduro alielezea hatua ya jeshi la Israel kulenga kambi ya watu waliokimbia makazi yao katika mji wa Rafah katika Ukanda wa Gaza mauaji ya umati na kuongeza kuwa hivi sasa katika eneo zima la Ukanda wa Gaza Israel inatekeleza mauaji ya kimbari ya kutisha zaidi ambayo ubinadamu umeshuhudia tangu wakati wa Hitler." " Amebainisha masikitiko yake kuwa Israel inaendeleza mauaji ya kimbari tika Ukanda wa Gaza mbele ya macho ya ulimwengu bila mtu yeyote kuizuia." Aliikosoa Marekani na Umoja wa Ulaya na kusema pamoja na ku...

Ubalozi wa Israel nchini Mexico wateketezwa moto katika maandamano ya kupinga mauaji ya Rafah

Image
Waandamanaji waliokuwa na hasira wameuchoma ubalozi wa utawala haramu Israel katika jiji la Mexico City nchini Mexico wakati wakibanisha malamiko yao kuhusu mauaji ya kimbari yanaotekelezwa na Israel huko Gaza. Waandamanaji wanaounga mkono Wapalestina walishiriki katika "Hatua ya Dharura Kwa Ajili ya Rafah" na walielezea hasira zao mbele ubalozi wa utawala ghasibu Israel. Waandamnaji waliokuwa na hasira walivurumisha mabomu ya kujitengenezea ya Molotov Cocktail katika jengo la ubalozi huo wa Israel. Aidha waandamanaji waliwarushia mawe polisi wa kutuliza ghasia ili kulipiza kisasi baada ya kurushiwa  mabomu yakuwarushia vitoa machozi. Mexico, siku ya Jumanne, iliwasilisha tamko la kujiunga na kesi ya Afrika Kusini dhidi ya utawala haramu wa Israel katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) ikiishutumu Israel kwa kutekeleza "mauaji ya kimbari" Gaza. Maandamano kama hayo...

Wataalamu zaidi ya 50 wa UN wataka Israel iwekewe vikwazo na marufuku ya silaha

Image
Wataalamu zaidi ya 50 wa Umoja wa Mataifa wametoa mwito wa kuchukuliwa "hatua madhubuti kimataifa" baada ya kuelezea walivyokasirishwa na shambulio la kinyama la jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel ambalo liliua Wapalestina wasiopungua 45 waliokuwa wametafuta hifadhi kwenye kambi ya muda huko Rafah, kusini mwa Ukanda wa Ghaza. Wataalamu hao wa UN wamesema: "picha za kutisha za uharibifu, watu kubaki bila makazi na vifo zimeibuka kutoka Rafah, zikiwemo za watoto wachanga walioraruliwa vipandevipande na watu kuteketezwa wakiwa hai". Kundi hilo la wataalamu zaidi ya 50 wa Umoja wa Mataifa limeendelea kueleza katika taarifa yake kwamba, ripoti zilizotoka kwenye eneo lililolengwa zinaonyesha kuwa shambulio la jeshi la Kizayuni lilikuwa la kiholela na lisilo na mlingano, na lilifanywa wakati watu wakiwa wamekwama ndani wakiungua kwenye mahema ya plastiki, na kusababisha vifo v...

Kamati Kuu ya kuchunguza ajali ya helikopta iliyombeba Shahidi Ebrahim Raisi yatoa ripoti ya pili

Image
  May 30, 2024 03:40 UTC Kituo cha Mawasiliano cha Kamandi Kuu ya Majeshi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kimetoa ripoti ya pili ya Kamisheni Kuu ya kuchunguza sababu za ajali ya helikopta iliyosababisha kifo cha Rais Seyed Ebrahim Raisi, na ujumbe ulioandamana naye. Helikopta iliyokuwa imembeba Rais Raisi, Waziri wa Mambo ya Nje Amir-Abdollahian, Imamu wa Swala ya Ijumaa ya Tabriz Ayatullah Mohammad Ali Al-e-Hashem, Gavana wa Azarbaijan Mashariki Malek Rahmati, kamanda wa kikosi cha walinzi wa rais, marubani wawili na walinzi ilianguka mkoa wa kaskazini-magharibi wa Azarbaijan Mashariki mnamo Mei 19, 2024. Miili yao ilipatikana siku ya Jumatatu baada ya msako wa usiku mzima katika eneo lililokuwa na hali mbaya ya hewa. Wote waliokuwamo ndani ya helikopta hiyo walipoteza maisha na kupata daraja ya juu ya kufa shahidi. Kwa mujibu wa ripoti ya pili iiliyotangazwa Jumatano na Kamati Kuu y...

Ndege nyingine isiyo na rubani ya MQ-9 ya Marekani iliyodunguliwa na Yemen wakati wa kampeni ya kuiunga mkono Palestina

Image
    Ndege nyingine isiyo na rubani ya MQ-9 ya Marekani iliyodunguliwa na Yemen wakati wa kampeni ya kuiunga mkono Palestina Yemen imeangusha ndege nyingine ya kisasa isiyo na rubani ya jeshi la Marekani wakati kampeni yake ya kuunga mkono Palestina ikipanuka katikati ya vita vya kikatili vya Israel dhidi ya Gaza. Vikosi vya jeshi la Yemen vilitoa taarifa siku ya Jumatano vikisema kuwa Vikosi vyake vya Ulinzi wa Anga viliidungua ndege isiyo na rubani ya MQ-9 Reaper mapema siku hiyo ilipokuwa ikiruka angani katika jimbo la kati la Marib. "Operesheni ya kulenga shabaha ilifanywa kwa kombora lililotengenezwa nchini kutoka ardhini hadi angani," ilisema taarifa hiyo, na kuongeza kuwa video ya ufyatuaji huo itachapishwa hivi karibuni. Ilikuwa ni mara ya pili kwa siku ambapo Wayemeni waliiangusha MQ-9 Reaper, ndege nzito na ya kisasa yenye thamani ya karibu dola milioni 30. Jumla ya ndege sita zisizo na rubani za aina hii zimesambaratishwa na Yemen tangu mwaka jana wakati nchi hiyo y...

Naibu waziri wa fedha wa Marekani amewasili Ukrain

Image
  Adeyemo alisema Marekani inapanga kuchukua hatua zaidi ili kuweka shinikizo kwa uchumi wa Russia. Naibu Waziri wa Fedha wa Marekani Wally Adeyemo amewasili Kyiv siku ya Jumatano kukutana na maafisa wa Ukraine kwa mazungumzo kuhusu kuimarisha vikwazo dhidi ya Russia pamoja na msaada wa kifedha kwa Ukraine. Alisema Marekani inapanga kuchukua hatua zaidi ili kuweka shinikizo kwa uchumi wa Russia. Uchumi wa Russia umekuwa uchumi wa wakati wa vita, ambapo kila njia ya uzalishaji na viwanda sasa imejikita katika kujenga silaha za kupambana na vita vyao ilivyovichagua na uvamizi hapa Ukraine, Adeyemo alisema Jumatano katika mji mkuu wa Ukraine. “Tunahitaji kufanya kila tuwezalo ili tufanikiwe baada ya hapo”. Adeyemo amesema kipaumbele cha Hazina ni kupunguza mapato ya Russia na kuizuia Russia kupata bidhaa inazozihitaji ili kuzisaidia ngome zake za viwanda vya ulinzi, ikijumuisha bidhaa za matumizi ya nchi mbili kutoka China.