Posts

Showing posts from October, 2024

Washukiwa wa kundi la madhehebu ya kidini waua 10 Uganda

Image
  Washukiwa wa kundi la madhehebu ya kidini waua 10 Uganda Chanzo cha picha, POLISI UGANDA Polisi walisema washukiwa wawili pia waliuawa walipokuwa wakijaribu kushambulia vikosi vya usalama. Takribani watu 10 wamethibitishwa kufariki,na wengine 8 wamelazwa hospitali baada ya kujeruhiwa katika shambulizi lililotekelezwa katika Wilaya ya Kigadi,Magharibi mwa Uganda, Polisi na Jeshi la Uganda UPDF limethibitisha jumatano. ‘’Taarifa za awali zinaonesha kwamba wanakikundi cha madhehebu ya kidini,ambacho jina lake halijafahamika walishambulia familia ambazo wengi wao ni jamaa zao kwa kuwakata kwa kifaa chenye ncha kali na kusababisha vifo na majeruhi’’alieleza Mejaj Bilal Katamba baada ya shambulizi la saa tatu usiku katika Kijiji cha Muzizi. Kwa mujibu wa Meja Katamba Jeshi la Uganda na Polisi wameanza msako kuwabaini washukiwa wa shambulizi hilo wakati uchunguzi unaendelea. Katika taarifa nyingine,msemaji wa polisi katika mkoa wa Albertine SP Julius Allan Hakiza aliwataja ...

Ndege zisizo na rubani za Urusi zinaua raia, ushahidi unaonyesha

Image
  Ndege zisizo na rubani za Urusi zinaua raia, ushahidi unaonyesha Kabla ya saa sita, siku moja Serhiy Dobrovolsky, mfanyabiashara wa vifaa vya nyumbani, alikuwa akirejea huko Kherson kusini mwa Ukraine. Alipoingia ndani ya eneo lake, akawasha sigara na kuanza kuzungumza na jirani yake wa karibu. Ghafla, walisikia sauti ya ndege isiyo na rubani nje. Angela, mke wa Serhiy wa miaka 32, anasema alimuona mumewe akikimbia na kujificha huku ndege isiyo na rubani ikidondosha guruneti kumlenga. "Alifariki kabla ya gari la wagonjwa kufika. Niliambiwa alikuwa na bahati mbaya kwa sababu kipande cha guruneti kilimchoma moyoni," anasema, huku akibubujikwa na machozi. Serhiy ni mmoja wa raia 30 waliouawa katika mashambulizi ya ghafla ya ndege zisizo na rubani za Urusi huko Kherson tangu Julai 1, utawala wa kijeshi wa jiji hilo uliambia BBC. Wamerekodi zaidi ya mashambulizi 5,000 ya ndege zisizo na rubani katika kipindi hicho, huku zaidi ya raia 400 wakijeruhiwa. Lakini BBC imesikia ushuhu...

'Wanawake wapende wasipende nitawalinda' - Trump

Image
  'Wanawake wapende wasipende nitawalinda' - Trump Chanzo cha picha, EPA Donald Trump aliambia mkutano wa hadhara jana usiku kwamba "Wanawake wapenda wasipende nitawalinda. Nitawalinda dhidi ya wahamiaji wanaoingia. Nitawalinda dhidi ya mataifa ya kigeni ambayo yanataka kutupiga kwa makombora." Akizungumza na umati wa watu karibu na Green Bay, Wisconsin, Trump aliwaambia wafuasi wake kwamba washauri wake walimwambia "haifai" kuzungumza juu ya kulinda wanawake. Kamala Harris alijibu kwenye mtandao wa X, kwamba "Donald Trump anafikiri anapaswa kufanya maamuzi kuhusu nini cha kufanya na mwili wako upende usipende. Katika kura za maoni, Donald Trump ana uungwaji mkono kwa kiasi kikubwa na wanaume, huku wanawake wengi wakisema wanampendelea Kamala Harris.

‘Tunaomba Malkia wa urembo Muheto afungwe mwaka mmoja’ - Mwendesha Mashtaka

Image
  ‘Tunaomba Malkia wa urembo Muheto afungwe mwaka mmoja’ - Mwendesha Mashtaka Chanzo cha picha, Miss Rwanda Ofisi ya Mwendesha Mashtaka nchini Rwanda amemuombea Malkia wa urembo wa Rwanda Divine Muheto kifungo cha mwaka mmoja na miezi minane kwa makosa ya kuendesha gari akiwa amekunywa pombe kupita kiasi, na kugonga miundombinu kisha kutoroka eneo la tukio. Bi Muheto, 21, alifikishwa mahakamani mapema Alhamisi asubuhi, saa chache kabla ya kesi kuanza kusikilizwa. Chumba kidogo cha Mahakama ya mtaa ya Kicukiro kilijaa wanahabari wengi na watu walioonekana kuwa marafiki na wanafamilia wake. Baada ya kusomewa mashtaka yanayomkabili, Divine Muheto ambaye alikuwa akiwakilishwa na mawakili watatu, alisema anakiri kosa la kuendesha gari akiwa mlevi na kugonga na kukimbia. Kwa sauti ndogo, akionekana kuwa mwenye hofu, alisema: “Lakini siamini kwamba nilitoroka kwasababu gari nililiacha hapo. Niliogopa kwa sababu watu wengi walikusanyika na kuhofia kwamba wangeniumiza. Polisi walipofika nil...

Shughuli za uokoaji zinaendelea huku Uhispania ikiomboleza vifo vya takriban watu 100

Image
  Shughuli za uokoaji zinaendelea huku Uhispania ikiomboleza vifo vya takriban watu 100 Chanzo cha picha, EPA Uhispania inakabiliana na athari mbaya ya mafuriko ambayo yaliathiri jamii za kusini katika saa 24 zilizopita. Taarifa ya mwisho kutoka kwa mamlaka ya Valencia saa 19:30 CET (18:30 GMT) ilisema idadi ya waliofariki katika eneo hilo ni 92, na watu wengine wawili waliuawa katika eneo jirani la Castilla-La Mancha. Muingereza mwenye umri wa miaka 71 pia alifariki saa chache baada ya kuokolewa kutoka nyumbani kwake Alhaurin de la Torre, huko Malaga, kulingana na kiongozi wa eneo la Andalusia. Mwanahabari wetu Nicky Schiller ametua tu Valencia na anasema mvua imepungua, lakini hapo awali, Waziri Mkuu Pedro Sanchez aliwataka wakaazi katika eneo hilo, na pia wa Andalusia na Catalonia, kuwa waangalifu kwani maonyo ya hali ya hewa bado yanaendelea katika maeneo mengi. Waziri wa sera za eneo Ángel Víctor Torres alisema bado haijulikani ni watu wangapi walipoteza maisha baada ya mvua k...

Mahakama ya rufaa yakataa ombi la Gachagua la kusitisha Mahakama Kuu kusikiliza kesi yake

Image
  Mahakama ya rufaa yakataa ombi la Gachagua la kusitisha Mahakama Kuu kusikiliza kesi yake Chanzo cha picha, EPA Naibu Rais aliyeondolewa madarakani Rigathi Gachagua amepata pigo lingine baada ya mahakama ya rufaa kukataa kutoa maagizo ya kusimamisha Mahakama Kuu kuendelea kusikiliza kesi yake ya kuondolewa madarakani. Gachagua alikwenda mahakama ya rufaa akisema kuwa hajaridhishwa na uamuzi uliotolewa wiki jana na jopo la majaji watatu iliyoidhinisha uamuzi wa Naibu Jaji Mkuu Philomena Mwilu wa kuunda jopo la majaji hao kusikiliza kesi za Gachagua. Rigathi Gachagua alikuwa amesema Naibu Jaji Mkuu Philomena Mwilu hana mamlaka ya kuunda jopo hilo, isipokuwa jopo kama hilo linaweza kuundwa tu na Jaji Mkuu. Hatima ya Gachagua sasa iko kwa Mahakama Kuu ambayo kwa sasa inaendelea kutoa uamuzi juu ya kesi ya kuzuia kuapishwa kwa Naibu Rais mteule Kithure Kindiki. Jopo la majaji hao ni pamoja na Jaji Anthony Mrima, Eric Ogola na Fredah Mugambi.

Jaribio la Gachagua kuzuia kuapishwa kwa Kindiki lagonga mwamba

Image
  Jaribio la Gachagua kuzuia kuapishwa kwa Kindiki lagonga mwamba Chanzo cha picha, Getty Images Mahakama Kuu nchini Kenya imeondoa amri zinazomzuia Naibu Rais Mteule Kithure Kindiki kuapishwa. Wakati wakitoa uamuzi huo, jopo la majaji watatu wakiongozwa na Jaji Eric Ogola, Anthony Mrima na Fredah Mugambi walisema kuwa afisi ya kikatiba ya naibu rais haiwezi kuachwa wazi. David Munyi Mathenge na Peter Gichobi Kamotho walitaka mahakama kuweka maagizo ya kusitisha kuapishwa kwa Kindiki Kithure kama Naibu Rais mpya baada ya Bunge la Kitaifa kuidhinisha uteuzi wake, siku moja baada ya Bunge la Seneti kupiga kura ya kumtimua Rigathi Gachagua. David Munyi Mathenge na Peter Gichobi Kamotho walitaja suala hilo kuwa la "umuhimu mkubwa na udharura wa kitaifa." Wakitoa uamuzi wao, jopo la majaji watatu waliendelea kusema kwamba kesi hiyo itatajwa Novemba 7, 2024, na kuongeza kuwa Gachagua yuko huru kuwasilisha rufaa dhidi ya uamuzi huo. "Maombi ya maagizo yakumzuia Naibu Rais Mt...

'Sote tunajua mtu ambaye amefariki dunia – hili ni jinamizi'

Image
  'Sote tunajua mtu ambaye amefariki dunia – hili ni jinamizi' Chanzo cha picha, EPA Hapa Paiporta, Valencia, ambapo makumi ya watu waliuawa katika mafuriko ya ghafla, maduka, nyumba na biashara zimeharibiwa. Katika mtaa mmoja naona watu wakiopoa maiti. Akiwa amesimama nje ya mabaki ya duka lake la dawa, mfamasia Miguel Guerrilla ananiambia: "Sote tunamfahamu mtu ambaye amefariki dunia." "Hili ni jinamizi," anasema. Watu waliojitolea wamefika kusaidia kusafisha lakini ni kazi ya kutisha. Ninapotembea kijijini, nimeona gari la huduma ya mazishi limefika kuchukua mwili mwingine.

Urusi yatoza Google faini ya thamani ya pesa isiyoweza kuhesabika

Image
  Urusi yatoza Google faini ya thamani ya pesa isiyoweza kuhesabika Chanzo cha picha, Getty Images Mahakama ya Urusi imeitoza Google faini ya thamani isiyoweza kuhesabika - mbili zikifuatwa na sufuri 36 - kwa kuzuia vituo vya habari vya serikali ya Urusi kwenye YouTube. Kwa dola hiyo inamaanisha kuwa kampuni hiyo kubwa ya kiteknolojia ameambiwa alipe $20,000,000,000,000,000,000,000,000,000,000,000. Licha ya kuwa moja ya kampuni tajiri zaidi duniani, hiyo ni zaidi ya dola trilioni 2 za thamani ya Google. Kwa hakika, ni kiasi kikubwa zaidi kuliko jumla ya Pato la Taifa la dunia, ambalo linakadiriwa na Shirika la Fedha la Kimataifa kuwa $110 trilioni. Faini hiyo imefikia kiwango cha juu sana kwa sababu - shirika la habari la serikali Tass linasema - inaongezeka maradufu kila siku ambayo haijalipwa. Kulingana na Tass, msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov alikiri "hawezi hata kutamka nambari hii" lakini akahimiza "wasimamizi wa Google kuzingatia." Kampuni hiyo haijatoa maoni...

Uingereza na nchi nyingine nane 'zasikitishwa' na visa vya utekaji nyara nchini Kenya

  Uingereza na nchi nyingine nane 'zasikitishwa' na visa vya utekaji nyara nchini Kenya Mabalozi tisa na makamishna wakuu wa balozi za kigeni nchini Kenya wameelezea wasiwasi wao kutokana na visa vya hivi majuzi vya utekaji nyara kote nchini. Denmark, Finland, Ujerumani, Ireland, Uholanzi, Norway, Uswidi, Uswizi na Uingereza katika taarifa ya pamoja siku ya Alhamisi zilisema kila Mkenya ana haki na uhuru wa kimsingi zilizolindwa katika katiba. "Kulinda haki za binadamu kunaleta utulivu na ustawi. Kwa hivyo, tuna wasiwasi juu ya ripoti zinazoendelea za kukamatwa kwa watu kiholela na kutoweka licha ya maamuzi ya Mahakama Kuu," "Ni muhimu kuhakikisha utawala wa sheria unatawala na maamuzi ya mahakama yanafuatwa." Mabalozi na makamishna wakuu walirejelea ahadi ya mara kwa mara ya Rais William Ruto tangu ashike wadhifa wake mwaka wa 2022 kwamba visa vya watu kutoweka havitafanyika chini ya uangalizi wake. Huku wakipongeza Kenya kwa kuchaguliwa kwake katika Baraz...

Je hiki ndicho kilichomponza Gachagua?

Image
  Je hiki ndicho kilichomponza Gachagua? Chanzo cha picha, AFP Mahakama Kuu nchini Kenya imeamua kuwa Kithure Kindiki anaweza kuapishwa kuwa Naibu Rais Mpya baada ya kutupilia mbali ombi la Naibu wa Rais aliyeondolewa madarakani Rigathi Gachagua. Wakati likitoa uamuzi huo, jopo la majaji watatu lilisema kuwa afisi ya kikatiba ya naibu rais haiwezi kuachwa wazi. Mgombea mwenza wa Rais William Ruto katika uchaguzi uliopita Rigathi Gachagua alitimuliwa na bunge la Kenya mapema mwezi huu. Baadaye, Rais Ruto alimteua Waziri wa Mambo ya Ndani Kithure Kindiki kama Naibu Rais mpya na Bunge la kitaifa likapiga kura kuunga mkono uteuzi wake. Imeelezwa kwamba Naibu Rais wa Kenya Rigathi Gachagua ameng’olewa madarakani kwasababu ya kuhujumu idara ya ujasusi na mahakama, kukiuka kiapo chake na Katiba na kuchochea siasa za ukabila. Lakini inawezekana hata bila kukusudia, Gachagua mwenyewe ameeleza umma vyema kiini cha kung’olewa kwake madarakani, pegine vyema zaidi kuliko wachambuzi...

'Mimi sio mpiga kura wa suala moja, lakini hili ni kubwa': Utoaji mimba uliamua kura za wanawake hawa

Image
  'Mimi sio mpiga kura wa suala moja, lakini hili ni kubwa': Utoaji mimba uliamua kura za wanawake hawa Maelezo kuhusu taarifa Author, Rachel Looker Nafasi, BBC News, Washington Saa 5 zilizopita Uchaguzi wa urais wa 2024 ni wa kwanza tangu Mahakama ya Juu ilipobatilisha uamuzi wa Roe v Wade, ambao ulilinda haki ya kitaifa ya kutoa mimba. Mgawanyiko wa kijinsia umekuwa mkubwa katika uchaguzi huu, huku kura za maoni zikionyesha Kamala Harris ana uongozi miongoni mwa wanawake na Rais wa zamani Donald Trump anaongoza kwa upande wa wanaume. BBC imekuwa ikizungumza na wapiga kura wanawake kuhusu jinsi wanavyozingatia jinsia na uavyaji mimba huku wakipiga kura katika siku za mwisho za kampeni. Michelle anafanya kazi kama mhandisi wa ubora huko Arizona. Ana umri wa miaka 38 na ni mwanachama wa chana cha Republican , lakini anapanga kumpigia kura Kamala Harris. Matangazo Nina wasiwasi kuhusu haki za wanawake na afya ya wanawake. Mimi si mpiga kura wa suala moja, lakini h...

'Nadhani tuko mashakani' - je, ni kweli Man City ina wachezaji 13 pekee wasio na majeraha?

Image
  'Nadhani tuko mashakani' - je, ni kweli Man City ina wachezaji 13 pekee wasio na majeraha? Chanzo cha picha, Getty Images Maelezo ya picha, Manchester City ilipoteza wachezaji wengine wawili kutokana na majeraha dhidi ya Tottenham Jumatano usiku Saa 4 zilizopita Pep Guardiola anasema Manchester City ina "wachezaji 13" na wako "mashakani" baada ya timu yake kupata majeraha zaidi kwenye mechi ya Kombe la Ligi dhidi ya Tottenham Jumatano. City ambao tayari hawakuwa na wachezaji sita wa kikosi cha kwanza kwenye mchezo huo, walimpoteza mlinzi Manuel Akanji kutokana na tatizo la mguu wakati wa maandalizi. Mshambulizi Savinho kisha alitolewa nje kwa machela katika dakika ya 63 ya mchezo baada ya kuonekana kuumia kifundo cha mguu. Guardiola pia alisema beki Ruben Dias, ambaye alitoka mapumzikoni, "anatatizika" wakati mwingine. "Tuna wachezaji 13, tuko kwenye matatizo makubwa," Guardiola alisema. "Wanaocheza, wanamaliza wengi wao waki...

Mustakabali usiojulikana wa mgogoro wa Iran na Israeli

Image
  Mustakabali usiojulikana wa mgogoro wa Iran na Israeli Chanzo cha picha, Getty Images Saa 7 zilizopita Mgogoro kati ya Iran na Israel haujawahi kutokea katika historia ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili na umesababisha eneo la Mashariki ya Kati kukabiliwa na hofu ya vita vya maangamizi. Lakini wakati huo huo, maelezo ya kile kilichotokea yanaonyesha jinsi ushindi wa mwisho wa kijeshi usivyoweza kupatikana katika mapambano haya. Iran haina uwezo wa kuishambulia Israel na kuiangamiza serikali ya nchi hiyo, wala Israel haiwezi kuiteka Tehran. Kila moja ya nchi hizi ina sababu tofauti za kutenda kwa umakini. Hata hivyo, nchi zote mbili zinaogopa kupoteza sifa zao, na kwasababu hii, haziwezi kukaa muda bila kufanya shambulio lolote dhidi ya upande mwingine, na mvutano huu unaendelea. Kutokana na hilo nchi hizo mbili zinatumia makombora ya masafa marefu na ndege za kivita za F-35, na zana nyingine za kivita. Vita vya historia Kama migogoro yote ya kimataifa, pande hi...

Korea Kaskazini yarusha kombora linaloshukiwa kuwa la masafa marefu

Image
  Korea Kaskazini yarusha kombora linaloshukiwa kuwa la masafa marefu Chanzo cha picha, Reuters Korea Kaskazini imerusha kombora linalodaiwa kuwa la masafa marefu (ICBM) kuelekea baharini katika pwani yake ya mashariki, jeshi la Korea Kusini lilisema. Tukio hilo linakuja wakati uhusiano kati ya Korea mbili hizo mbili unavyozidi kuwa mbaya. Kombora hilo lilirushwa mwendo wa takribani saa 07:10 za huko siku ya Alhamisi (22:10 GMT Jumatano). Korea Kusini ilikuwa imeonya Jumatano kwamba Kaskazini ilikuwa inajiandaa kuirusha ICBM yake wakati wa uchaguzi wa urais nchini Marekani tarehe 5 Novemba. Mara ya mwisho Korea Kaskazini ilirusha kombora la ICBM mwezi Disemba mwaka jana, kinyume na vikwazo vya muda mrefu na vile vile vya Umoja wa Mataifa. Nchi jirani ya Japan ilisema kuwa ilifuatilia urushaji wa kombora wa Alhamisi, na kuongeza kuwa kombora hilo lilitarajiwa kuanguka baharini ifikapo 08:40 saa za huko. Tukio hilo la Alhamisi linakuja baada ya Korea Kusini na Marekani kuishu...

Israel yashambulia mji wa kihistoria wa Baalbek nchini Lebanon

Image
  Israel yashambulia mji wa kihistoria wa Baalbek nchini Lebanon Chanzo cha picha, AFP Mashambulizi ya Israel yamesababisha watu 19 kupoteza maisha, wakiwemo wanawake wanane, karibu na mji wa Baalbek mashariki mwa Lebanon, wizara ya afya ya nchi hiyo imesema. Hilo limejiri saa chache baada ya makumi ya maelfu ya wakazi kukimbia kutokana na maagizo ya kuwahamisha yaliyotolewa na jeshi la Israel. Meya Mustafa al-Shell aliiambia BBC zaidi ya mashambulizi 20 yaliripotiwa Jumatano alasiri katika eneo la Baalbek, na matano ndani ya jiji lenyewe, ambapo kuna jumba la hekalu la kale la Kirumi lililotambuliwa na Unesco. Jeshi la Israel lilisema kuwa limeshambulia vituo vya amri na udhibiti vya Hezbollah na miundombinu huko Baalbek na Nabatiyeh, kusini mwa Lebanon. Jeshi pia lilisema lililenga vituo vya mafuta vya Hezbollah katika Bonde la Bekaa, ambako Baalbek ipo. Halikutoa maelezo yoyote, lakini shirika la habari la serikali ya Lebanon lilisema matangi ya dizeli yalipigwa kat...

Mithili ya tsunami': Wahispania wasimulia athari ya mafuriko mabaya

Image
  Mithili ya tsunami': Wahispania wasimulia athari ya mafuriko mabaya Chanzo cha picha, Reuters "Maji yalipoanza kupanda, yalikuja kama wimbi," Guillermo Serrano Pérez alisema. "Ilikuwa kama tsunami." Kijana huyo mwenye umri wa miaka 21 kutoka Paiporta, karibu na Valencia, ni mmoja wa maelfu ya watu waliokumbana na mafuriko ya Jumanne usiku ambayo yalikumba eneo hilo na kuua takriban watu 95. Alikuwa akiendesha gari kwenye barabara hiyo na wazazi wake Jumanne jioni wakati maji yalipoingia ndani. Walinusurika kwa kupanda daraja na kuliacha gari lao kutokana na nguvu ya maji ya mafuriko. Mvua kubwa ilikuwa inanyesha eneo hilo kwa saa nyingi, wengi, kama vile Guillermo Serrano Pérez na familia yake, walipatwa na mafuriko bila kutarajia. Hata hivyo dalili zilikuwepo. Siku ya Jumanne asubuhi yapata saa 07:00 (06:00 GMT), wakala wa hali ya hewa wa Uhispania Aemet alionya kuwa mvua kubwa ilikuwa inatabiriwa katika eneo la Valencia. "Kuwa mwangalifu san...

Waziri wa Ulinzi wa Marekani asema wanajeshi wa Korea Kaskazini wamevalia sare za kijeshi za Urusi

Image
  Waziri wa Ulinzi wa Marekani asema wanajeshi wa Korea Kaskazini wamevalia sare za kijeshi za Urusi Chanzo cha picha, KCNA/Uriminzokkiri Maelezo ya picha, . Mawaziri wa ulinzi wa Marekani na Korea Kusini, Lloyd Austin na Kim Yong Hyun, walifanya mkutano na waandishi wa habari mjini Washington. Wakizungumza juu ya Korea Kaskazini, haswa utumaji wake wa wanajeshi kwenda Urusi ambapo Moscow na Pyongyang hawakatai hatua hiyo, ingawa hawakubali moja kwa moja. Austin alisema wanajeshi wa Korea Kaskazini waliotumwa Urusi wamebadilika na kuanza kuvaa sare za kijeshi za Urusi, taarifa iliyotolewa mapema Jumatano kwenye kikao na Baraza la Usalama la Kitaifa la Korea Kusini. Austin pia alisema hata kwa msaada wa Korea Kaskazini, Urusi haitaishinda Ukraine. Marekani na washirika wake wataihamasisha Pyongyang kutotumia wanajeshi hao katika shughuli za kijeshi, lakini aliweka bayana kuwa hii inaweza kutokea hata hivyo. Kim Yong Hyun alitoa wito kwa Korea Kaskazini "kuondoa mara moja" wan...

Wanawake waliobakwa nchini Sudan, hufa kwa kujiua, wanaharakati wanasema,

Image
  Wanawake waliobakwa nchini Sudan, hufa kwa kujiua, wanaharakati wanasema , Chanzo cha picha, AFP Habari hii ina maelezo ambayo baadhi yanaweza kuhuzunisha. Wanawake kadhaa wamejitoa uhai katika jimbo la kati la Gezira nchini Sudan baada ya kubakwa na wapiganaji wa kijeshi katika vita vya kikatili vya wenyewe kwa wenyewe vinavyoendelea nchini humo, makundi ya kutetea haki za binadamu na wanaharakati wamesema. Ripoti hizo zinakuja baada ya wanamgambo wa RSF kushutumiwa na Umoja wa Mataifa kwa "uhalifu wa kikatili", ikiwa ni pamoja na mauaji ya halaiki, katika jimbo hilo wiki iliyopita. Huku wapiganaji wa RSF wakiendelea kusonga mbele, shirika moja la kutetea haki za binadamu limeiambia BBC kuwa linawasiliana na wanawake sita ambao wanafikiria kujiua huku wakihofia kudhulumiwa kingono. Lakini RSF imetupilia mbali ripoti ya hivi karibuni ya Umoja wa Mataifa inayolaumu kuongezeka kwa unyanyasaji wa kingono kwa wapiganaji wake, ikiiambia BBC kwamba shutuma hizo ...

Je, Trump anafanya nini kuwavutia wapiga kura Waislamu?

Image
  Je, Trump anafanya nini kuwavutia wapiga kura Waislamu? Chanzo cha picha, Getty Images Maelezo ya picha, Trump ajaribu kuwavutia Waarabu Wamarekani na Waislamu Saa 2 zilizopita Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump aliwaalika viongozi wengi wa Kiislamu katika mkutano wake wa hadhara mjini Michigan. Trump amesema katika mkutano huo kwamba wapiga kura wa Kiarabu na Waislamu wamekasirishwa na sera ya kigeni ya Marekani kuhusu Israel na Gaza. "Waislamu hapa wanaweza kugeuza uchaguzi wa Marekani," Trump alisema Jumamosi katika vitongoji vya Detroit na Novi vilivyopo Dearborn, Michigan. Mwaka jana, mji wa Marekani wa Dearborn ulikuwa mji wenye Waislamu wengi zaidi nchini Marekani. Asilimia 55 ya watu wanaoishi hapa ni wa asili ya Mashariki ya Kati au Afrika Kaskazini. Idadi ya Waislamu nchini Marekani ni asilimia 1.1. Ziara ya viongozi wa dini ya Kiislamu katika Michigan Chanzo cha picha, Getty Images Maelezo ya picha, Viongozi wa Kiislamu walikuwepo jukwaani kati...