Sababu za Serikali ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina kufuata muelekeo sawa na wa utawala wa Kizayuni dhidi ya HAMAS
Serikali ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina imeendelea kufuata muelekeo sawa na wa utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS kwa kutoa amri ya kufungwa Chaneli ya Televisheni ya Al Jazeera ya Qatar huko Ramallah. Siku ya Jumatano usiku, Mamlaka ya Ndani ya Palestina ilitangaza kuwa imepiga marufuku shughuli za Al Jazeera kwa sababu ya ilichokiita "kukiuka sheria na kanuni za ndani na kutangaza maudhui za kichochezi". Kutokana na uamuzi huo, shughuli zote za ofisi ya Al Jazeera ndani ya Palestina, ikiwa ni pamoja na utangazaji wa vipindi na shughuli za wanahabari na maripota wa chaneli hiyo zimesimamishwa. Ofisi ya Al Jazeera, Ramallah, Ukingo wa Magharibi Hatua hiyo iliyochukuliwa na Mamlaka ya Ndani ya Palestina inaweza kuchambuliwa kwa kuzingatia nukta kadhaa. Kwanza ni kuwa, hatua hiyo imechukuliwa...