Mtanziko wa ANC katika kuamua mustakabali wa Afrika Kusini
Chama tawala nchini Afrika Kusini cha African National Congress (ANC), kinakabiliwa na kizungumkuti juu ya mustakabali wa nchi hiyo baada ya kupoteza idadi kubwa ya wabunge katika uchaguzi wa wiki iliyopita. Kimeshinda kwa asilimia 40 ya kura, ANC inahitaji kupata mshirika ili kupata wingi wa wabunge ambao wataunga mkono rais atakae chaguliwa – ama iamue kwenda peke yake na serikali ya wachache. Chaguo moja litakuwa, ni kufanya makubaliano na chama cha pili kwa ukubwa, chama cha mrengo wa kati cha Democratic Alliance (DA), ambacho kilipata 22% ya kura. Wapo wenye matarajio ya kuona muungano wa ANC-DA, hasa kwa vile unapendelewa na sekta binafsi kama chaguo bora zaidi la kuhakikisha uthabiti wa kiuchumi. Hata hivyo hilo linaweza kuwa hatari kisiasa, kwani wakosoaji wa DA wanakishutumu kwa kujaribu kulinda uchumi wa wazungu wachache – walioupata wakati wa mfumo wa ubaguzi wa rangi - madai ambayo chama hicho kinakanusha. Vinginevyo, ANC inaweza kufanya kazi na vyama viw