Biden: Ni 'Uzembe' kwa Trump kusema kesi yake ilipangwa
Rais wa Marekani Joe Biden amesema ilikuwa "uzembe" kwa mtangulizi wake, Donald Trump, kuitaja kesi yake kuwa na udanganyifu, siku moja baada ya kupatikana na hatia na kuweka kihistoria nchini humo. Akizungumzia maoni ya kwanza kwa umma ya Trump kuhusu kupatikana na hatia kwa makosa 34 ya kughushi rekodi za biashara, Bw. Biden alitetea mfumo wa sheria wa Marekani. "Kanuni ya Marekani kwamba hakuna mtu aliye juu ya sheria ilithibitishwa tena," Bw Biden alisema kuhusu kilichotokea. Mapema siku ya Ijumaa, Trump alitoa maneno makali kwenye mkutano na wanahabari katika jengo la Trump Tower huko Manhattan, akimtaja jaji kuwa "mpotovu", kesi hiyo ni "uzushi" na "majambazi" wa Democrats. Maoni ya Bw Biden siku ya Ijumaa alasiri yanawadia mwanzoni mwa mkutano wa waandishi wa habari wa White House ambapo alijadili Mashariki ya Kati na pendekezo jipya la Israel kwa Gaza. Bw Biden alisema mpinzani wake wa chama cha Republican katika uchaguzi wa r...