Posts

Rais Yoon aliidhinisha jeshi kufyatua risasi Bungeni, yafichua Ofisi ya Mwendesha Mashtaka

Image
  Nchini Korea Kusini, rais aliidhinisha jeshi kufyatua risasi kuingia Bungeni, kulingana na ofisi ya mwendesha mashtaka wa Korea Kusini. Mnamo Desemba 3, mkuu wa nchi, aliyesimamishwa kazi kwa sasa, alijaribu kuweka sheria ya kijeshi nchini humo. Wakati huo huo alipeleka jeshi katika Bunge la taifa. Sasa yamejulikana mengi zaidi kuhusu kile kilichotokea usiku huo. Rais wa Korea Kusini Yoon Suk-yeol wakati akitangaza sheria ya kijeshi kwenye televisheni, Desemba 4, 2024. © Soo-hyeon Kim / REUTERS ...

Syria: Kiongozi mpya akutana na wawakilishi wa serikali ya magharibi mwa Libya

Image
  Kiongozi huyo mpya wa Syria amekutana Jumamosi na maafisa wa serikali ya umoja wa kitaifa ya Libya inayotambuliwa na Umoja wa Mataifa, ujumbe wa hivi punde zaidi wa kidiplomasia kuzuru Damascus tangu kuondolewa madarakani kwa Bashar Al Assad karibu wiki tatu zilizopita. Kiongozi wa kundi la wapiganaji wa Kiislamu nchini Syria Hayat Tahrir al-Sham (HTS) aliyeongoza mashambulizi makubwa na kunyakua Damascus kutoka kwa udhibiti wa serikali, Abu Mohammed al-Jolani, akiwasili ndani ya Msikiti wa Umayyad katika mji mkuu wa Syria kuhutubia umati uliokusa...

Gaza: Hospitali kuu ya Kamal Adwan sasa 'haifanyi kazi'

Image
Huko Gaza, hospitali muhimu kwa wakazi wa kaskazini mwa eneo hilo imeharibiwa sana wakati wa shambulio la Israeli. Kulingana na Shirika la Afya Duniani, WHO, imebidi kufungwa. Huko Gaza, hospitali ya Kamal Adwan imeharibiwa vibaya wakati wa shambulio la Israeli. Hapa, ilikuwa Oktoba 31, 2024. AFP - - ...

India: Waziri mkuu wa wa zamani Singh azikwa

Image
  India siku ya Jumamosi imetoa heshima za mwisho kwa Waziri Mkuu wa zamani Manmohan Singh, anayejulikana kwa mageuzi yake ya kiuchumi yaliyoifanya nchi hiyo kuwa kubwa duniani. Dakika 2 Bwana Singh amekuwa mkosoaji mkubwa wa sera za kiuchumi za Waziri Mkuu Modi, pia akionya juu ya hatari zinazoletwa na kuongezeka kwa mivutano ya kijamii kwa demokrasia ya India. Reuters/路透社 ...

Serge Atlaoui aliyehukumiwa kifo nchini Indonesia, Ufaransa yadai rasmi arejeshwe nyumbani

Image
Kwa miaka kumi na minane, Serge Atlaoui ameishi kwenye orodha ya wafungwa wanaotakiwa kunyongwa. Mfaransa huyu mwenye umri wa miaka 61 alihukumiwa kifo nchini Indonesia mwaka wa 2007, nchi inayojulikana kwa ukali wa sheria zake za kupinga dawa za kulevya. Lakini Ufaransa imeomba rasmi "uhamisho" wake ili kumruhusu kujiunga na Ufaransa. Dakika 3 Awali Serge Atlaoui alihukumiwa kifungo cha maisha jela. Lakini mwaka wa 2007, Mahakama Kuu iliongeza hukumu yake, na kumhukumu kifo, pamoja na wanachama wen...

Real Madrid wanamtaka Van de Ven - Tetesi za Soka Ulaya Jumapili

Image
  Chanzo cha picha, Getty Images Dakika 12 zilizopita Real Madrid wanataka kumsajili Micky van de Ven kutoka Tottenham huku kukiwa na tatizo la majeraha kwenye safu ya ulinzi, wakati Barcelona ikiwa katika uwezekano wa kuondokewa na Dani Olmo na Frenkie de Jong mnamo mwezi Januari kipindi ambacho miamba hao wa La Liga wanakabiliwa na tatizo la kupunguza gharama. Beki wa Tottenham na Uholanzi Micky van de Ven, 23, analengwa na Real Madrid Januari kufuatia msururu wa majeraha kwa wachezaji wa safu ya ulinzi wa klabu hiyo ya Uhispania. (Relevo - in Spanish) Chanzo cha picha, Getty Images Lakini mchezaji huru na nahodha wa zamani Sergio Ramos, 38, anataka ndoto irejee Real Madrid kufuatia majeraha ya Mhispania mwenzake, Dani Carvajal, 32, David Alaba, 32, Mbrazil Eder Militao, 26. (AS - in Spanish) Chanzo cha picha, Getty Images Mshambulizi wa Barcelona Dani Olmo, 26, yuko tayari kuhamia kwa mkopo katika Ligi ya Primia mwezi Januari ikiwa klabu yake haiwezi kumsajili mch...

Iran: Marekani inalenga kuwapora Waislamu, haitafanikiwa chochote nchini Syria

Image
  Jeshi la Iran linasema kutimuliwa kwa Rais Bashar al-Assad wa Syria na wanamgambo wanaoungwa mkono na mataifa ya kigeni ni njama ya Wamarekani na Wazayuni, lakini Marekani haitafanikiwa lolote katika nchi hiyo ya Kiarabu. Kamandi Kuu ya Majeshi ya Iran imesema katika taarifa: " Matukio ya hivi karibuni katika eneo hilo, bila kusahau matukio ya Syria, yanaonyesha kuendelea kwa uovu, ukosefu wa usalama na kina cha uadui wa kiburi cha ulimwengu, kinachoongozwa na uovu mkubwa ya Marekani ya uhalifu, dhidi ya mataifa yanayotafuta uhuru." Taarifa hiyo imebainisha kuwa: “Pasiwe na shaka kwamba yaliyotokea Syria ni zao la njama ya pamoja ya Marekani na Kizayuni. Ni dhahiri kwamba mfumo wa kivita unaoongozwa na Marekani katika eneo la Asia Magharibi unalenga kufikia malengo yake maovu, ikiwa ni pamoja na kupora rasilimali na kuwafanya Waislamu kuwa watumwa . " Kamandi Kuu ya Majes...

Iran: Shambulio la Israeli katika Hospitali ya Kamal Adwan ni 'uhalifu mbaya wa kivita'

Image
  Iran imekemea shambulio la kikatili la utawala wa Israel kwenye Hospitali ya Kamal Adwan katika eneo la kaskazini mwa Gaza kama “uhalifu mbaya wa kivita” na sehemu ya mauaji ya kimbari yanayoendelea kwenye ardhi za Palestina zilizokaliwa kwa mabavu na kusema kimya cha taasisi muhimu za kimataifa kuhusu suala hilo kama “hakikubaliki.” Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje, Esmaeil Baghaei, katika taarifa iliyotolewa Jumamosi, alilaani uvamizi wa kikatili wa Israeli kwenye hospitali hiyo na uharibifu mkubwa wa sehemu nyingi zake kama mfano wa hivi karibuni wa uhalifu wa kivita, uhalifu dhidi ya ubinadamu, na ukiukaji wa wazi wa sheria na kanuni za kimataifa. Alisema kwamba ukatili huu ulitekelezwa kwa lengo la kuharibu kabisa mfumo wa huduma za afya katika Gaza, na kuwanyima watoto, wanawake, watu waliojeruhiwa na wagonjwa ufikiaji wa huduma za matibabu za hali ya chini. Baghaei alisis...

Maulamaa wa Kiislamu duniani wataka hatua za dharura kusitisha jinai za Israel huko Gaza

Image
  Katibu mkuu wa Umoja wa Kimataifa wa Wanazuoni wa Kiislamu (IUMS) amesema kwamba ukatili wa utawala wa Kizayuni wa Israel katika Ukanda wa Gaza hauwezi kuvumiliwa na jamii ya kimataifa lazima ichukue hatua haraka ili kuweka mwisho wa mauaji ya kimbari ya Kizayuni katika eneo hilo. Ali Muhammad Al-Sallabi aliiambia tovuti ya Arabi21: "Mauaji makali na ya kutisha yanayofanywa na utawala wa Kizayuni wa Isarel dhidi ya watu wa Palestina hayawezi kuvumiliwa. Ameongeza kuwa: “kile ambacho hakika hakiingii akilini  ni kwamba watu wasiokuwa na kinga wa Palestina, ambao wamewekwa katika mzingiro Ukanda wa Gaza kwa karibu miongo miwili, na ambao wamekuwa wakikabiliwa na vita vya mauaji ya kimbari tangu Oktoba mwaka jana, sasa wanakabiliwa na njaa inayoua kwa kukosa chakula, na baridi inayoua kwa kukosa makao.” Amesema, "Haya ni makosa yanayofanywa si tu na [kikosi] cha Israeli na washir...

UN kuanza kusambaza misaada ya chakula Sudan leo

Image
  Msafara mkubwa zaidi uliobeba chakula cha misaada umefika katikak mji mkuu  wa Sudan, Khartoum tangu kuanza kwa mzozo mwezi Aprili 2023. Msafara huo unajumuisha usaidizi wa chakula wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani (WFP) na misaada mingine ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia watoto (UNICEF) na misaada kwa wadau wengine . Msaada huo wa chakula kwa sasa unashushwa baada ya msafara unaoongozwa na WFP wa malori 28 umepanga kusambaza chakula siku ya Jumapili, 29 Desemba, na chakula hiki kinakusudiwa kwa takriban watu 78,000 . “ Msafara huu pia ni wa mara ya kwanza tangu kuanza kwa mzozo ambapo msaada wa chakula wa WFP unafikishwa Mayo na Alingaz kusini mwa Khartoum. Maeneo yote mawili yako katika hatari ya njaa, kulingana na uainishaji wa viwango vya njaa (IPC).” Ameeleza Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa . WFP imekuwa ikifanya kazi ya k...

'Kuanguka kwa Assad kulivyofungua sehemu ya maisha ya mume wangu ambayo sikuijua'

Image
  Maelezo ya picha, Abdullah Al Nofal (kushoto) na mkewe Douna Haj Ahmed 28 Disemba 2024 'Kuanguka kwa Assad kumenifanya kufahamu maisha ya zamani ya mume wangu ambayo nilikuwa sifahamu.' Ilikuwa mwanzoni mwa mwezi Desemba pale Douna Haj Ahmed, mkimbizi kutoka Syria alipogundua taarifa mbaya zinazohusiana na kushikiliwa kwa mume wake katika gereza lenye sifa mbaya la Al-Khatib, linalofahamika kama "Jehanam ya Duniani". Alikuwa akitazama jinsi wafungwa waliochanganyikiwa wakijaribu kuondoka katika moja ye eneo lenye ulinzi mkali, akiwa nyumbani kwake mjini London, baada ya vikosi vya waasi kumuondoa rais Bashar al-Assad kwenye nafasi yake kama rais. Akiwa analia, Abdullah Al Nofal, mume wake wa miaka nane alikaa pembeni yake, na kumuangalia akisema "Hapa ndipo nilipokamatwa, Ni eneo hili." Douna, ambaye kaka zake pia walikamatwa wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa muda wa miaka 13, anasema alikuwa ana uelewa wa kile ambacho mum...

Senegal kufunga vituo vyote vya kijeshi vya kigeni, ni vilivyosalia vya Ufaransa vilivyoko nchini humo

Image
Waziri Mkuu wa Senegal Ousmane Sonko amesema, nchi hiyo itafunga kambi zote za kijeshi za kigeni katika ikiwa ni sehemu ya juhudi za serikali za kupitia upya sera ya ulinzi na kuimarisha mamlaka ya kitaifa. Sonko alitangaza uamuzi huo katika Bunge la Taifa hapo jana wakati wa uwasilishaji sera kuu, ambapo alielezea mkakati wa mabadiliko ya taifa hilo la Afrika Magharibi katika miaka 25 ijayo.   "Rais wa Jamhuri ameamua kufunga kambi zote za kijeshi za kigeni katika siku za usoni," Sonko alisema.   Waziri Mkuu wa Senegal hakutaja nchi maalumu, lakini Ufaransa ndiyo nchi pekee ya kigeni yenye wanajeshi nchini humo.   Rais wa Senegal Bassirou Diomaye Faye, ambaye amekuwa madarakani kwa muda wa chini ya mwaka mmoja, alitangaza kwa mara ya kwanza uamuzi wake wa kuondoa jeshi la Ufaransa nchini mwake katika mahojiano na shirika la habari la AFP mwishoni mwa mwezi uliopita....

Serikali ya Al-Joulani yatoa agizo la siri: Picha zozote za mauaji na uporaji zisisambazwe

Image
  Kufuatia kusambazwa picha na video za mauaji na uporaji unaofanywa na wanachama wa Tahrir al-Sham nchini Syria, utawala mpya wa Al-Joulani umetoa agizo la siri la kupiga marufuku usambazaji wa picha na video hizo. Maafisa walio chini ya Al-Joulani, mkuu wa kundi la Hayat Tahrir al-Sham, wamepokea waraka wa siri, unaopiga marufuku kurekodi video za aina yoyote za operesheni za ukamataji watu, mapigano na mauaji ya hadharani yanayofanywa nchini Syria.   Waraka huo unajumuisha miji 30 ya nchi hiyo.   Inasemekana kuwa, kusambazwa video zinazohusiana na kuwatia nguvuni watu, kuwaua na kuwanyonga hadharani na kuchoma moto maeneo matakatifu nchini Syria kunakofanywa na wafuasi wa Al-Joulani kumezikasirisha fikra za umma ndani ya nchi hiyo na hata katika nchi zingine.   Kwa mujibu wa ripoti, 95% ya vitendo vya kinyama vinavyofanywa na mawakal...

Rais wa Kenya aahidi kukomesha utekanyaji nyara ili vijana wa nchi hiyo waishi kwa amani

Image
Rais William Ruto wa Kenya ameahidi kukomesha utekaji nyara, kufuatia visa vya hivi karibuni vya watu kutoweka ambavyo vimelaaniwa na mashirika ya kutetea haki za binadamu, mawakili na wanasiasa. Vikosi vya usalama katika taifa hilo la Afrika Mashariki vimeshutumiwa kwa kuwashikilia watu kadhaa kinyume cha sheria tangu yalipofanyika maandamano yaliyoongozwa na vijana dhidi ya serikali katika miezi ya Juni na Julai. Polisi wamekanusha kuhusika lakini wanaharakati wamehoji ni kwa nini wanaonekana kutochunguza kupotea kwa watu hao. Utowekaji wa hivi karibuni wa watu umehusisha hasa vijana ambao wamemkashifu Ruto mtandaoni, huku mashirika ya kutetea haki ya binadamu yakikanusha madai ya polisi kutohusika na kutaka hatua zichukuliwe. Akizungumza na umati wa watu jana Ijumaa huko Homa Bay, mji ulioko magharibi mwa Kenya, Rais Ruto aliahidi kukomesha utekaji nyara huo lakini pia aka...

2024 watajwa kuwa mwaka mbaya zaidi kwa watoto kwenye mizozo duniani katika historia ya UNICEF

Image
Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF limesema, zaidi ya watoto milioni 473, sawa na zaidi ya mtoto mmoja kati ya sita duniani kote anaishi kwenye vita, huku dunia ikigubikwa na mizozo mingi zaidi tangu kumalizika kwa Vita Kuu vya Kwanza vya Dunia. Taarifa iliyotolewa leo na UNICEF imebainisha kuwa, asilimia ya watoto wanaoishi kwenye mizozo imeongezeka maradufu kutoka asilimia 10 miaka ya 1990 hadi asilimia 19 hivi sasa. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mwaka huu kuliko wakati wowote ule, watoto wengi zaidi wanakadiriwa kuwa wanaishi kwenye maeneo yenye mizozo au wamelazimika kukimbia makwao kutokana na mizozo. “Idadi kubwa ya watoto waliodhurika na mizozo, haki zao zinakiukwa, ikiwemo kuuawa au kujeruhiwa, hawaendi skuli, wanakosa chanjo muhimu, na hawana lishe ya kutosha,” imesema taarifa hiyo ikisisitiza kuwa 2024 ni mwaka ambao UNICEF katika historia yake haijawahi k...

Mkuu wa IRGC: Wayemeni hatimaye wataibuka washindi

Image
Kamanda Mkuu wa Jeshi la Iran la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amelipongeza taifa la Yemen kwa kulitetea kwa ushujaa taifa la Palestina wakati huu wa hujuma ya umwagaji damu ya Israel dhidi ya Wapalestina wa Gaza na kueleza kuwa Wayemen hatimaye wataibuka washindi. Meja Jenerali Hossein Salami aliyasema hayo katika mahojiano na kanali ya televisheni ya al-Masirah ya Yemen yenye lugha ya Kiarabu siku ya Jumamosi . Ameongeza kuwa: " Wayemeni, kwa vile wamepinga kwa utu na heshima hadi leo, wataendeleza upinzani wao kwa neema ya Mwenyezi Mungu na hatimaye wataibuka washindi." Aliongeza, “The Mrengo wa Muqawama haujadhoofika; na kila mtu anashuhudia jinsi Wayemen wanavyoilinda Palestina kwa umahiri na kufanya maandamano kila Ijumaa kuunga mkono Gaza . " Jeshi la Yemen lilitangaza siku ya Ijumaa kwamba lilirusha "kombora la balestiki la hypersonic" ambalo lilile...

Trump aitaka Mahakama ya Juu ya Marekani kuchelewesha marufuku ya TikTok

Image
  Chanzo cha picha, Getty Images Maelezo ya picha, Rais mteule wa Marekani Donald Trump Rais mteule wa Marekani Donald Trump ameiomba Mahakama ya Juu ya Marekani kuchelewesha marufuku inayokuja ya TikTok huku akifanyia kazi "azimio la kisiasa". Wakili wake aliwasilisha muhtasari wa kisheria siku ya Ijumaa na mahakama ambayo inasema Trump "anapinga kupigwa marufuku kwa TikTok" na "anatafuta uwezo wa kutatua masuala yaliyopo kupitia njia za kisiasa mara tu atakapoingia madarakani". Tarehe 10 Januari, mahakama inatazamiwa kusikiliza hoja kuhusu sheria ya Marekani inayomtaka mmiliki wa TikTok Mchina, ByteDance, kuiuza kampuni hiyo ya mitandao ya kijamii kwa kampuni ya Kimarekani la sivyo apigwe marufuku ifikapo Januari 19 - siku moja kabla ya Trump kuchukua madaraka. Maafisa wa Marekani na wabunge walikuwa wameshutumu ByteDance kwa kuhusishwa na serikali ya China - jambo ambalo kampuni hiyo inakanusha. Madai hayo ya programu ambayo ina watumiaji milioni 170 n...

Nigeria yakanusha kushirikiana na Ufaransa kuyumbisha Niger

Image
  Chanzo cha picha, AFP Maelezo ya picha, Kiongozi wa Niger, Abdourahmane Tchiani, alshutumu jirani yake Nigeria kwa kujaribu kuyumbisha nchi yake. Nigeria imekanusha shutuma kutoka kwa kiongozi wa kijeshi wa Niger, Brig Jenerali Abdourahmane Tchiani, kwa kushirikiana na Ufaransa kulivuruga taifa hilo linaloongozwa na junta. Katika mahojiano ya Siku ya Krismasi, Jenerali Tchiani aliishutumu Ufaransa kwa kushirikiana na makundi ya wanamgambo katika eneo la Ziwa Chad ili kudhoofisha usalama wa Niger, ikidaiwa kuwa Nigeria inafahamu. "Mamlaka za Nigeria hazijui kuhusu hatua hii ya kizembe," Jenerali Tchiani alinukuliwa akisema na AFP. kijibu, Mshauri wa Usalama wa Taifa wa Nigeria, Nuhu Ribadu, aliiambia BBC Hausa kwamba madai hayo "hayana msingi" na "uongo". Bw Ribadu alisema Nigeria kamwe "haitahujumu Niger au kuruhusu maafa yoyote kuikumba". Waziri wa Habari wa Nigeria, Mohammed Idris, alisema madai hayo hayana msingi na "mbinu ya kitofauti ...

Je, Urusi itawaachilia maelfu ya wanajeshi wa Ukraine kwa mwaka mpya?

Image
  Afisa mmoja wa Ukraine ameiambia BBC wanatumai mabadilishano ya wafungwa ya Mwaka Mpya na Urusi yatafanyika "siku yoyote," ingawa mipango inaweza kuafikiwa dakika za mwisho. Petro Yatsenko, kutoka Makao Makuu ya Ukraine kwa ajili ya Matibabu ya Wafungwa wa Vita, alisema mazungumzo na Moscow kuhusu kubadilishana wafungwa yamekuwa magumu zaidi katika miezi ya hivi karibuni tangu majeshi ya Urusi yaanze kufanya kupiga hatua kubwa katika mstari wa mbele. Kulikuwa na mabadilishano 10 pekee mwaka 2024, ikiwa ni idadi ya chini kabisa tangu uvamizi wa wa Urusi nchini Ukraine uanze. Ukraine haichapishi idadi ya wafungwa wa vita wanaoshikiliwa na Urusi, lakini jumla inadhaniwa kuwa zaidi ya 8,000. Urusi imepata mafanikio makubwa katika medani ya vita mwaka huu, na kuzua hofu kwamba idadi ya raia wa Ukraine wanaokamatwa inaongezeka.

Putin aomba radhi kwa ajali ya ndege, bila kusema Urusi ina makosa

  Rais wa Urusi Vladimir Putin ameomba radhi kwa rais wa nchi jirani ya Azerbaijan kwa kudungua ndege ya kubeba raia katika anga ya Urusi, ambapo watu 38 waliuawa - lakini akaacha kusema Urusi ilihusika. Katika maoni yake ya kwanza juu ya ajali ya siku ya Krismasi, Putin alisema "tukio la kusikitisha" lilitokea wakati mifumo ya ulinzi wa anga ya Urusi ilipokuwa ikifukuza ndege zisizo na rubani za Ukraine. Ilikuwa imeripotiwa kuwa ndege hiyo ilishambuliwa na mifumo ya ulinzi ya anga ya Urusi ilipojaribu kutua Chechnya - na kuilazimisha kuvuka bahari ya Caspian. Ilianguka huko Kazakhstan, na kuua 38 kati ya 67 waliokuwemo.