Rais Yoon aliidhinisha jeshi kufyatua risasi Bungeni, yafichua Ofisi ya Mwendesha Mashtaka
Nchini Korea Kusini, rais aliidhinisha jeshi kufyatua risasi kuingia Bungeni, kulingana na ofisi ya mwendesha mashtaka wa Korea Kusini. Mnamo Desemba 3, mkuu wa nchi, aliyesimamishwa kazi kwa sasa, alijaribu kuweka sheria ya kijeshi nchini humo. Wakati huo huo alipeleka jeshi katika Bunge la taifa. Sasa yamejulikana mengi zaidi kuhusu kile kilichotokea usiku huo. Rais wa Korea Kusini Yoon Suk-yeol wakati akitangaza sheria ya kijeshi kwenye televisheni, Desemba 4, 2024. © Soo-hyeon Kim / REUTERS ...